Sasa mbona huonekani kuunga mkono maandamano ya wafanyabiashara yasio na kikomo?
Msimamo wangu ni kuwa serikali iandae mpango wa Watu wote nchi nzima kulipa kodi kuanzia tajiri wa kwanza hadi Maskini wa mwisho.
Walipe kulingana na kipato chao
Kiongozi namba moja mpaka yule wa chini kabisa.
Taasisi zote zilipe kodi mpaka zile za kidini.
Watu ambao hawapaswi kulipa kodi ni wanafunzi, watoto na wazee
Sheria kali iundwe ya wezi na mafisadi watakaoiba pesa za umma wanyongwe.
Walipa kodi Wakiwa wengi utitiri wa kodi utapungua.
Hapo hao wafañyabiashara wanapoteza muda wao tuu. Hakuna kitakachotatuliwa
Kwa sababu serikali inachukua kodi kwa watu wachache ambao ni watumishi wa umma, wafanyakazi wa sekta binafsi wenye kazi shughuli rasmi na hao wafañyabiashara ambao nao ni vile wapo eneo wasiloweza kukimbia hizo kodi
Sio haki kuwa na utitiri wa kodi.
Sio haki pia kundi dogo kutozwa kodi huku kundi kubwa likiwa halitoi kodi ( Direct tax)
Sio haki viongozi kuwa wabadhirifu wa fedha za umma.