Tetesi: Kesho kuvaa nguo za CHADEMA ni jinai.

Tetesi: Kesho kuvaa nguo za CHADEMA ni jinai.

Kwani nikiwajibu nimevaa kwa sababu nilinunua kwa pesa halali nitakua nimekosea?. Sitawajibu kwanza hilo ni swali la kiuchochezi.
 
Basi ni vyema taifa zima likatangaziwa leo kwani kama watu wanavaa mitumba na wengine hawana nguo za kutosha wakipewa hizo nguo bure kwa condition ya kuzivaa kesho na baadae kuwa yake - kwa wenye hali ngumu - watavaa; kama vile ilivyo kwenye kampeni za uchaguzi mkuu; kwani mpaka leo watu wana nguo za kampeni za uchaguzi mkuu na zimechakaa na bado wanazivaa.
 
tetesi???
Kwani kwa vigezo vya JF unajua maana ya "Tetesi"? maana yake linaweza kuwa ni jambo la kweli lakini haliwezi kuthibitishwa na mamlaka husika kutokana na sababu mbali mbali. Kesho watakaovaa vipeperushi vya CHADEMA ndiyo watajua maana ya tetesi hii.
 
Bado ni hisia za kutunga tu
Kutunga kwa sababu wewe unataka ziwe za kutunga. kwani waliokatazwa kuandamana ni nani hapo kesho, na jee vipeperushi vya CHADEMA haviwatambulishi na kwa mfano watu wanne wakiwa wameongozana wamevaa hivyo vipeperushi wakikutana na Polisi unadhani kitatokea nini? Kama ilitokea Dodoma mpaka Nyumba za Wageni kupekuliwa itakuwa kesho?
 
Kuna tetesi kwamba kesho mtu yeyote atakayeonekana amevaa Nguo au vipeperushi vya CHADEMA atakamatwa na kutakiwa kujieleza ni kwa nini amevaa nguo hizo.
hili serikali ya JPM wanachofanya kuwaweka wananchi kwenye wasiwasi hadi kuwachagulia nguo za kuvaa amini msiamini litawafanya wananchi kuichukia serikali yao hata kama itawafanyia vizuri hakuna kitu kibaya kama kuminya demokrasia ya mtu,hana uwezo wa kukujibu wala kukutukana ila kidonda kilicho moyoni mwake majibu yake na athari zake ni kubwa sana,ipo siku madhara yataonekana
 
Kutunga kwa sababu wewe unataka ziwe za kutunga. kwani waliokatazwa kuandamana ni nani hapo kesho, na jee vipeperushi vya CHADEMA haviwatambulishi na kwa mfano watu wanne wakiwa wameongozana wamevaa hivyo vipeperushi wakikutana na Polisi unadhani kitatokea nini? Kama ilitokea Dodoma mpaka Nyumba za Wageni kupekuliwa itakuwa kesho?
Hapo sasa umefunguka, hata leo ukibeba vipeperushi hutaachwa!Kwa hiyo siyo lazima kesho!Hapa kuna vuguvugu ambalo ni lazima lipoe kwanza ili maisha yaendelee, haina maana kumiminia petroli, moto unaweza kuwaka
 
Kuvaa nguo za CHADEMA ni kosa?
 
Back
Top Bottom