Time will tell. Sasa tunaongozwa na walioko nje ya magogoni .wanaotaka miradi ya gas na bandari ya bagamoyo kuanzishwa.
Sasa nchi isipokuwa na wafanyabiashara wakubwa wanaokuja na mitaji yao ya madola toka nje, hizo kodi za kuajiri ,kulipa mishahara, kutoa Bima ya afya kwa watu wote itatoka wapi?
Au tuendelee kujenga tu majumba ya serikali na masoko na stand kwa ajili ya kukusanya pesa za maskini kama sadaka ,huku wasomi wakikosa ajira.
Elimu ya msingi Bure ,Chuo kikuu wengi wanakosa mikopo wakati inarudishwa kwa riba.
Dubai ni matokeo ya wawekezaji.
Bila uwekezaji wa watu wenye mitaji tutabaki kuwashangilia wezi wanaokula na kushiba na kutembea na mabegi ya pesa kununa mapapai na kugawa pesa barabarani kwa watu waliozuiwa kwa makusudi wasije wakajitambua ukawa mwisho wa wezi wa mali za umma.
Hivi unadhani wabaya ni wawekezaji au ni wanaosimamia mikataba wanaweka mbele maslahi yao.
Mwekezaji anawekeza pesa zake nyingi halafu anageuzwa kuwa mitaji ya watawala. Wanasiasa wanamfanya ATM ,Idara za Polisi wanamtegemea, anaambiwa ajenge hospitali,mara shule ,mara maji ,mara CCM wana kampeni wanamuomba pesa halafu mnasema wawekezaji ni wabaya.
Miradi yote inayofanywa na serikali inalenga kuwanufaisha wachache huku wengi wakiwa hawana kitu . Yaani tunatumia kodi ya nchi kunufaisha wezi, ni bora mtu aje na pesa zake atulipe kodi na hisa zetu za kumiliki rasilimali na ardhi.
Kuliko kuchukua pesa za umma na kwenda kuwalipa Wachina ili ajenge mradi huku pesa zikipitia kwa wezi walioliibia Taifa hili kwa nusu karne.
Kwa Kweli Mungu ndiye mwamuzi wa nani awatawale na kuwaongoza watu wake.
Kwa tulipokua tunaelekea kama Taifa tulikua tumepotea kabisa ndio maana tulibaki kuteka matajiri na kukamata pesa za watu na kuwabambiakia watu kesi za uhujumu uchumi. Hatukua na dira ya kimapato. Ingefikia mahali biashara zote rasmi zingefungwa na kubaki na wamachinga.
Maamuzi ya Mungu yaheshimiwe. Hakuna mtu aliyepinduliwa bali ni mapenzi ya Mungu Mama Samia atupeleke mbele kwa usalama mkubwa na utulivu wa mioyo yetu.
Kama wewe ulikua unafurahiya yote waliyokuwa wanayafanya kama vile walikua ni miungu basi ni zamu yako kula uovu wako.
Mama yetu atatupeleka mbele sana. Kazi inaendelea. Nchi haiwezi kuwa ni mali ya ukoo. Ni lazima usikilize watu na kuheshimu maoni yao.