Mdogo wangu alikua ameajiriwa na jamaa anaitwa richard kwenye kibanda cha tigo pesa
amepata short katika hiyo biashara, kulingana na maelezo yake, hiyo short aliipata kutokana na network mbovu ya mtandao wa tigo
anasema, alituma pesa kwa mtu, mtandao ukamjibu kuwa hiyo transaction haijafanikiwa, akarudia rudia badae akafanikiwa, lakini kumbe pale alipokua anajaribu afu inashindikana pesa ilikua inakwenda, sasa huyu mwenye kibanda, (aliyemuajiri dogo) amekwenda polisi na sasa kesho atapelekwa mahakani, tena kwa criminal charge
Dogo amelala Polisi Jumamosi, Jumapili tumeweza kumuwekea dhamana lakini ilikua shughuli pevu, Kuna dalili zote za rushwa! Mazingira yanaonesha kuna mtu kapewa pesa ili amfundishe adabu dogo.
Toka asubuhi tuko polisi, waliokuwepo wanasema hiyo issue anaishughulikia afande Nuru (ni mwanamke) afande nuru kapigiwa simu asubuhi saa mbili kasema yuko njiani anakuja, hadi saa nne hajafika, saa nne akapigiwa akasema nyie endeleeni na shughuli njooni saa saba, ilipofika saa saba akapigiwa simu akasema yupo njiani anakuja, hadi saa tisa alikua hajafika!
Alipofika kitu cha kwanza anasema tumsubiri Richard (huyo bwana aliyeshtaki), baada ya kueleweshana na kujiridhisha kwamba dhamana kwa mtu anayetuhumiwa sio lazima anayetuhumu awepo (sio requirement ya kisheria) Afande Nuru akasema anataka huyo Richard aje ili kuepusha majungu!
Tuliendelea kumsubiri huyo Richard hadi karibu saa kumi na moja jioni! Afande anasita kutoa dhamana kwa sababu anaogopa majungu.
Kitu kingine cha ajabu, dogo alipokamatwa jumamosi, hakuchukuliwa hata maelezo ya awali, Kwa maelezo niliyoyapata polisi ni kwamba Richard alimpigia simu afande kwamba kuna mtu kamdhulu, afande bila ushahidi wowote wa awali, bila hata kuchukua maelezo kutoka upande wa pili akafanya maamuzi ya kumkata dogo na kumtupa rumande, Jana (baada ya kuwa dogo kuwa amelala rumande tayari) Afande Nuru ndio kachukua kamwandikisha maelezo (hiyo ilikua saa tisa mchana)
Msaada kutoka kwenu
1. Nilifikiri hii ni kesi ya madai lakini kama nilivosema nafikiri kuna influence ya askari mmoja, na wanafungua criminal case, Je hii ni sahihi? kama sio tufanyaje?
2. Nitegemee nini kesho? ni wakati gani nahitaji kumhusisha mwanasheria? Je kuna mtu anaweza kusimamia hii case, kama ndio naomba aniPM
3. Huyu mtu alikuwa anasema hasara aliyopata ni laki nne lakini alipofika polisi akabadilisha ikawa laki saba, ni wazi anadanganya, lakini pia ni wazi anatumia rushwa, Nini nifanye kuzuia influence ya pesa anayotumia?