Una haki kabisa lakini ukienda kiwepesi hivi watakushinda vibaya sana. Kwanza kabisa hapo wenye makosa siyo huu mtandao wa TiGO Tanzania peke yao, bali hata mamlaka za usimamizi za kiserikali nazo inabidi zishitakiwe. Hivyo itakubidi ushitaki wahusika wengi kidogo.
Pia, hutakiwi kufungua hii kesi ukiwa peke yako, itakuwa haina uzito sana maana walioumia ni watu wengi zaidi yako, hivyo mahakama inaweza kukutaka kuthibitisha kwamba wewe ndiyo umeumia zaidi kuliko wateja wengine wote nchini Tanzania. Hivyo hili litakueletea changamoto, labda utufahamishe zaidi unataka kufungua kesi ya aina gani.
Binafsi nadhani kesi kama hizi, ili kuwashinda hawa maharamia wa mali zetu, inabidi utumie mwanya wa KIKATIBA hasahasa chini ya kipengele cha Haki za Binadamu (Basic Rights and Duties), tena ikiwezekana utafute wateja wenzako waliopata hasara halafu mnafungua kesi ya pamoja (A Representative Suit).
Ukijipanga na kutulia, unaweza kufungua kesi nzuri sanaa.