Kesho naondoka, siwezi endelea kukaa hapa. Siwezi acha anielewe vibaya ila nimeshindwa mimi...

Komeo Lachuma

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2014
Posts
7,926
Reaction score
17,030
Jamaa yangu zamani alikuwa vizuri tu kichwani. Mnakaa mnaongea mambo ya akili. Nimekuja mkoani kaniomba nisifikie lodge nifikie kwake. Nikasema huyu mwana toka kitambo ngoja nifikie tu kwake.

Maana ananisaidia pia huko hotel nisilale na vicheche. Tumekula tumemaliza. Mlo wenyewe tunaanza kula saa nne. Kweli? Tumemaliza nadhani tutapata wasaa wa kuongea mambo ya maana jamaa ndo anawasha TV kuangalia Tamthiliya ya Azam. Yaani aibu nimeona mimi.

Jamaa amekuwa fala, bwege na kanjanja sana. Anaangalia tamthiya za Azam. Na movies za kipuuzi tu za wabongo na wanaijeria.
 
Ondoka apo usiendelee kukaa na mtu wa hivyo na wewe utakuwa mjinga
 
Hiki cheo cha JF-Expert Member kinafanya mtu ajione mwaaaamba, Sasa siku ataanzisha Uzi Wa Kiboya mpaka nyote mliokuwa kwenye cheo hicho mnajiona Maboya...!
We umefika kwa Mtu unataka Umpangie TV Awashe saa Ngapi? Dinner atenge Saa ngapi?
Kweli..?
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
yani na hiyo kesho ikifika kimbia fasta, toka nduki wewe kimbia usiangalie nyuma... kimbia tu, ukiangua ukiumia inuka vumilia, toka nduki wewe kimbia kwa watu
 
Sasa ufala wake uko wapi hapo! Wew kama una yamaana yakumueleza siuyaanzishe?
Pia usimpime mtu kwa siku moja nakumuona fala siku azifanani...kama nimshiji naona amebadilika kiasi chakukushtua muulize kulikoni yaweza kuwa kuna mambo anayapitia unaweza ukawa msaada kwake kwa hata kwa ushauri.
 
Masikini Mtanzania akipata kielimu kidogo tu au kakipato fulani basi anawaona wengine mafala kinoma.

Kwaiyo kwako wewe angonekana mjanja kama angeangalia tamthilia tofati na za Azam si ndio? Alafu huko unakokusudia yeye aangalie pengine content ni zilezile sawa na izo zinazooneshwa Azam..

Yani wewe uliekusudia kufanya uzinzi lodge unamuita mwenzio mjinga? Mzee we nifala wa mwezi
 
Maisha mafupi kama inamfurahisha acha atazame.
Kila binadu ana vitu vyake navyopenda.
Kwa kuangalia tamthlia za Azam kwani kumemfanya ashindwe timiza majukumu yake?
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ n'toto n'jinga huyo.
 
Inaelekea wewe una matatizo flan flan kila mtu ana uhuru wake ww kalale ulitaka muanze story uanze kujisifia.
 
Ukizani baada ya kula atakwambia twende kugonga gambe?
 
Mkuu hapo hapafai

Mwingine ampandishe hasira huyu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…