Kesho ni kufa na kupona uwanja wa Mkapa, tuhamishie waganga wote wa jadi uwanja wa Taifa ili tusidhalilike

Leonel Ateba Mbinda

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2023
Posts
644
Reaction score
2,695
Kesho kwetu ni fainali, naiona safari ya Morocco kama kila mtanzania mwenye uchungu na uzalendo na nchi hii ataomba dua na sala kwa ajili ya wachezaji wetu na nchi kwa ujumla.

Kiukweli umoja na mshikamano wa watanzania kesho ni muhimu sana kuliko wakati wowote ule, silaha zote kesho zihamishiwe uwanja wa mkapa tukaishangilie stars mwanzo mwisho.

Ndugu yangu Hemed Morroco na Juma Mgunda, nyie wote watu wa Pwani, kule Zanzibar ndiko Simba na Yanga waliko watu wao, watu wa nje ya uwanja wako huko, Zanzibar ndio kwenye wataalamu wa kweli, leteni watu kutoka Pemba, leteni watu kutoka kwetu kule Mwakidila, Mwahako, Mabokweni, Mkinga nk.

Guinea ameshangilia sana alipomfunga DRC akidhani amemaliza, kesho mapema tu tunamaliza shughuli.

Tafadhalini makocha, golini Manula, kulia Kapombe, kushoto Zimbwe, Nne Bacca, Tano Job, Sita kesho axcheze Mudathir, winga Kibu, winga Msuva, Nane Feitoto, Tisa Samatta, Kumi Mzize.

Naiona safari ya Morocco, Naiona Safari ya Morocco, Mungu ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Tanzania, Inshaaallah mapema tu niko uwanjani na wataalamu wangu wawili.
 
Kwa hayo tunaweza sana, nashauri, mageti yote tufunge tutumie usafiri wa babu na bibi zetu kutua uwanjani.Ila pia kwakuwa tumebobea kwenye mambo haya viwango hivi hata kwenye zile sii hasa zetu za chafuzi situache sasa tutumie njia za asili na mambo yatunyookeee?
 
Kesho kwetu ni fainali, naiona safari ya Morocco kama kila mtanzania mwenye uchungu na uzalendo na nchi hii ataomba dua na sala kwa ajili ya wachezaji wetu na nchi kwa ujumla.

Kiukweli umoja na mshikamano wa watanzania kesho ni muhimu sana kuliko wakati wowote ule, silaha zote kesho zihamishiwe uwanja wa mkapa tukaishangilie stars mwanzo mwisho.

Ndugu yangu Hemed Morroco na Juma Mgunda, nyie wote watu wa Pwani, kule Zanzibar ndiko Simba na Yanga waliko watu wao, watu wa nje ya uwanja wako huko, Zanzibar ndio kwenye wataalamu wa kweli, leteni watu kutoka Pemba, leteni watu kutoka kwetu kule Mwakidila, Mwahako, Mabokweni, Mkinga nk.

Guinea ameshangilia sana alipomfunga DRC akidhani amemaliza, kesho mapema tu tunamaliza shughuli.

Tafadhalini makocha, golini Manula, kulia Kapombe, kushoto Zimbwe, Nne Bacca, Tano Job, Sita kesho axcheze Mudathir, winga Kibu, winga Msuva, Nane Feitoto, Tisa Samatta, Kumi Mzize.

Naiona safari ya Morocco, Naiona Safari ya Morocco, Mungu ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Tanzania, Inshaaallah mapema tu niko uwanjani na wataalamu wangu wawili.
Imani za kishirikina zanakwamisha hili taifa, kama team haikujiandaa itafungwa tu hakuna kona kona kwenye modern football
 
Hakuna kufa na kupona,kuna kufa au kupona.
Kwahiyo tushinde timu ifuzu au tufungwe timu ishindwe kufuzu.
 
Tuna hazina kubwa ya wachawi nchi hii, lazima kesho tuwatumie ili tupate ushindi
 
Hao waganga wapelekeni Kariakoo kuokoa maisha ya watu
 
Natamani kesho tulambwe ili kelele za mama anaupiga mwingi tusizisikie
 
Back
Top Bottom