Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 376,316
- 871,876
Kesho ni Sikukuu ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Muungano usioeleweka!
Kuna mambo mengi yasioeleweka kwenye Muungano huu!
Kwa uchache tu; Umewahi kuona Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano ya Tanzania akifanya chochote kwa mamlaka yake akiwa Zanzibar? Ni Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano ya Tanzania ambaye hana mamlaka yoyote upamde mmoja wa Muungano.
Vipi kuhusu Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano ya Tanzania? Umewahi kuona hata akikagua miradi Zanzibar? Huyu pia ni makamu ambaye hana mamlaka upande mmoja wa muungano. Kwann sasa viongozi hawa waitwe wa Muungano?
Pili, kuna mambo ya Muungano mambo yasio ya Muungano. Afya, Michezo, Elimu ya Msingi, Sekondari na Vyuo Vidogo, Nishati ni miongoni mwa mambo yasio ya Muungano. Lkn umewahi kujiuliza Mawaziri wa Wizara zinazoshughulikia masuala haya yasio ya muungano wanatumia alama gani na rasilimali za nchi gani? Wanatumia alama za Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, pia wanaingia kwenye Baraza la Mawaziri wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwanini? Kwa sababu Muungano haueleweki.
Tatu, kuna Bunge la Jamuhuri ya Muungano lenye wabunge kutoka pande zote. Ndani ya hilo bunge kunajadiliwa mambo ya Muungano na yasio ya muungano na wote wanashiriki mijadala. Yaani kuna Profesa wa Sheria Mh. Kabudi Paramagamba ambaye ni Waziri wa Michezo ambayo sio jambo la Muungano, ingawa Wizara yake inatumia alama na rasilimali za Muungano, na ambaye ni mjumbe wa Baraza la Mawaziri la Muungano. Yaani mambo ni shaghalabaghala!
Sasa kubwa kuliko. Si tuna Rais wa Jamuhuri ya Muungano? Yeye si ndio Mkuu wa Nchi wa Jamuhuri ya Muungano? Umewahi kujiuliza nguvu zote na madaraka yote makubwa ambayo Rais amepewa na katiba ya Jamuhuri ya Muungano, je! Nguvu hizo anazo Zanzibar?
Zanzibar ina Rais ambaye kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar amepewa mamlaka yote ndani ya Zanzibar kama vile Rais wa Jamuhuri alivyopewa mamlaka na katiba ya Jamuhuri. Kwa mantiki hiyo, Rais wa Jamuhuri akitekeleza majukumu yake ndani ya Zanzibar
Credit: FB mwandishi sikumzingatia jina