chai ya rangi
JF-Expert Member
- Mar 7, 2026
- 1,042
- 3,095
Tar 1 mwezi wa 4, dunia hua inaadhimisha sikukuu ya wajinga, ambapo watu wengi wanaitumia siku hii kuwafanyia watu utani au kuwadanganya ili waisherehekee vizuri siku ya wajinga wakiwa kama wajinga waliodanganyika.
Je katika sikukuu ya wajinga uliwahi kudanganywa nini ? au kama ulipata fursa uliwahi kuwadanganya nini wajinga wako?
Mimi nakumbuka kwenye siku kama hii ya mwaka 2022 kipindi nipo chuo nilienda venue au darasani na nilikuta kuna wanafunzi wa kozi fulani wanamsubiria Lecturer wao aje kuwafundisha,
Sasa nilivowakuta pale bado wanamsubiria hajaja nikawasalimia kisha nikajitambulisha nikawaambia mimi ni lecturer sifundishagi kozi yao ndo maana hawanijui, kisha nikawaambia nimeshaongea na mwalimu wenu amesema leo hatakuja kwaiyo nyie muendelee na ratiba zenu zingine.
Sasa wanafunzi wakishasikiaga pindi limeahirishwa ni shangwe tu kwaiyo hata hawakuaendelea kunisikiliza sana wakaanza makelele huku wakiondoka kurudi hostel na kwenye mishe zao zingine,
Nami nikawatazama vijana wangu wakishangilia na kuondoka kisha nami nikatokomea na kupotea maeneo ya madarasani, huku nikiwa najua vijana wangu wameisherehekea vyema sikukuu ya wajinga tena kwa kushangilia sana.