Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 28,722
- 20,610
Ndugu zangu Watanzania,
Siku ya Kesho panapo Majaliwa ya Mwenyezi Mungu nimepanga kuleta andiko zito sana kama Kimondo cha Ndolezi Mbozi Mkoani Songwe kuwausia wakuu wa Wilaya na Mikoa. Ni andiko la kuwakumbusha mambo mbalimbali, kuwakumbusha dhamana kubwa waliyoibeba ,kuwakumbusha wajibu wao katika Masuala mbalimbali wanayoshiriki ama kuongoza ama kuyafahamu.
Ikumbukwe ya kuwa viongozi hawa ni wenyeviti wa kamati za ulinzi na usalama katika maeneo yao.na hivyo kushiriki katika vikao mbalimbali nyeti vyenye kujadili ,kupitisha na kufanya maamuzi ya masuala mbalimbali mazito kwa maslahi mapana ya wilaya na Mikoa yao.
Ni watu wenye kujuwa na kufahamu siri mbalimbali za kiusalama na Masuala mbalimbali.hivyo ni nafasi zinazohitaji na kumhitaji mtu kuwa na kifua, usiri, hekima, busara, subira na kuchunga ulimi wake kama mboni ya jicho lake. Ni nafasi zinazohitaji mtu kuchuja Maneno na kujuwa yapi na maneno gani yaongelewe wapi na yapi UFE nayo kifuani pako..
Ni nafasi ambazo zinahitaji misuli ya kiakili ,ni nafasi ambazo zinahitaji utulivu wa hali ya juu kabisa.hazihitaji mtu mropokaji,mwenye mihemuko,mkurupukaji,jazba na ulevi au ulimbukeni wa cheo. Ni nafasi zinazohitaji kuwa mtu wa kuwa mbele ya wakati kwa mambo mbalimbali.
Ni nafasi ambazo kuna mambo mengi yanapaswa kuishia ofisini pasipo kwenda kumsimulia hata mkeo au watoto wako au watu wako wa karibu,kwa sababu hao watu unaowasimulia kumbuka kuwa hawajaapishwa wala hawajala kiapo chochote kile cha kutunza siri yoyote ile.hivyo wanaweza kwenda kuropoka popote pale bila hofu wala wasiwasi.wengine wanaweza kuropoka hata bar au hata kwenye ma group yao ya whatssap.
Ndio maana nimeona kesho muda fulani hasa nyakati za jioni baada ya mihangaiko ya hapa na pale ya kutwa nzima nije na andiko zito sana kwenda kwa viongozi hao.naamini kwa litakao wafikia litawasaidia kwa kiasi chake. Kumbuka tu kuwa Elimu haina Mwisho.
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.