kesho udsm mgomo kwenda mbele

kesho udsm mgomo kwenda mbele

menyidyo

JF-Expert Member
Joined
Oct 9, 2010
Posts
1,339
Reaction score
194
Muda huu tayari mabibo kumewaka. na pia wamefunga barabara ya mandela kwa dakika 10. sehemu ya mabibo hostel. kesho barabarani rasmi.
 
Amakweli vyuo vikuu vimecharuka!kama UDSM watalianzisha kesho serikali ya JEYKEY ijichunguze kwan kunataarifa za kuaminika kuwa UDOM wataendelea na mgomo wao mpaka kieleweke toka kwa Mh. PINDA a.k.a mtoto wa mkulima!!
 
leo saa nne tamko rasmi litatoka. hoja ni nyingi. mojawapo bumu. nitaendelea kuwaupdate!
 
hili bumu mbona kero kila mahali? inaonesha JK alitafuna hazina yote kwenye kampeni! manake MUHAS postgraduate wengine hadi leo hawajapewa hilo bu na watu wanaishi kwa mashaka sana!
 
Haya jamani makubwa tena? Mbona vyuo vikuu migomo tena?? Kulikoni?? Au jamaa wamekanusha HAZINA katika kampeni za kuchakachua na kuwapatia wadanganyika viji-Tisheti vya chama cha XYZefgHI!! Msikimbie kivuli chenu, solve matatizo ya watoto wa wakulima hao!! Wenu, wako majuu, mkiwaandaa eti waje wawe watawala wetu!! MMELAMBA GALASA!! Watatawala makaburi yenu, pambafu wakubwa!! Wash#$#@^&*!%^$# wakubwa majizi na mafisadi nyie!!
 
Yaani Jeykey mtu wa ajabu aliamuru wanafunzi wasipige kura, na leo hataki wapate pesa kwa wakati kwasababu pesa nyingi ilitumika kuwalipa vijana wa usarama wa taifa katika kusimamia kuteuliwa kwake na tume ya uchaguzi regardless ameshinda au hajashinda. zidumu fikra za baba ridhiwan
 
Hela zilipelekwa kwenye kampeni halafu huyu Shukuru yuko kimya tu sijui ndio staili yao mpya kukaa kimya kama bosi wao likitokea jambo.
 
In order to solve students crisis in Institutions of Higher Learning, you better use the win-win negotiation tactic rather than win-lose [a very unpopolar] negotiation tactic! It is a high time now the goverment through the responsible ministry should sit down and negotiate with students and faculy members of the said university(ies)!!

Use of very uncivilized way [POLICE FORCE!!] always triggered the situation to the worse ever!!

Always, patience, sense of responsibility, commitment and mutual respect to each other should prevail.

I advice both parties involved should strive to achieve a win-win situation!!!
 
leo saa nne tamko rasmi litatoka. Hoja ni nyingi. Mojawapo bumu. Nitaendelea kuwaupdate!

kwenye bumu nawapa mia. Wanavyuo wanataabika sana kwa posho kidogo hadi wasio na ustahimilivu wanaanza kufanya mambo ya aibu usiku ilimradi tu wajikimu na hali ngumu.
 
hili bumu mbona kero kila mahali? Inaonesha jk alitafuna hazina yote kwenye kampeni! Manake muhas postgraduate wengine hadi leo hawajapewa hilo bu na watu wanaishi kwa mashaka sana!

sasa itamtokea puani wasomi wanataka haki yao.
 
Kufanya mambo ya ajabu ni wanawake na wanaume au kina nani hasa? maana wote wanapewa bum sawa. Kuna aliyesema JK wamekausha hazina, me nakataa kwa sababu wale wote waliosubmit all requirements on time wamepata bum mtu anaambiwa asign hasign akiambiwa jaza form hajazi kwa wakati. Hivyo pamoja na matatizo ya kiufundi ya bodi ya mikopo wanafunzi wanajitakia matatizo. wanafunzi wanapewa 5000 kwa sasa lakini wataka 10,000/- na wanachohitaji ni kuishinikiza serikali iliangalie hilo before bonge la bajeti.

Mimi napenda kuwashauri wanafunzi kuwa makini na matumizi ya bum maana hata wakipewa 30,000/= per day alafu plan less hazitatosha. Serikali naishauri ifute kabisa bodi ya mikopo kwa sasa maana sisi tuligoma wakati ilipokuwa inajadiliwa bungeni ianzishwe tukaishia kula mabom na marungu, waachane na swala la idadi bila tija. watu wachache walipiwe na serikali waliofaulu vizuri na wengine walipiwe na wazazi wao.

Watu wengi wanawalipia watoto wao wa darasa la kwanza more than 1.6mln a year kwanini ashindwe kulipia 1.5 chuo kikuu?? The issue is sera na siyo maswala ya vyama vya siasa.
 
Kudai haki zenu kama wanafunzi wengine si shida, ni haki yenu ila maandamano yasiishei kudai pesa tu, kama wasomi mnatakiwa kudai maslahi ya Taifa. Walalahoi tunategemea wasomi kutuwakilisha katika matatizo yetu.
 
Fblukuwi said:
Wanasubiri nini? Sasa haki haipatikani mpaka itafutwe. Waingie mtaani tu!

Mkuu wakifanya hivyo nchi itakuwa haitawaliki!!
 
dah, hii nchi tutafute tu uraia wa nchi mbili ili iwe rahisi kwenda kwingine kama raia badala ya kuwa wakimbizi manake tunakoelekea, moto huu hapa!
 
Averos umenena, hilo ndio la muhimu. Kuhusu mgomo wa UDSM leo nimefanya utafiti issue kuu ni maswala ya katiba, issue ya arusha na bum. Mbaya zaidikuna msukumo mkubwa wa vyama vya sias.
 
Wanafunzi wanadai bum kujinusuru na njaa wanaambiwa hakuna hle lakini za kumlipa DOWANS zipo analazimishwa alipwe, Huu mchezo mchafu wa serikali wauache mara moja ili kuepusha fujo na mifarakano
 
Mgomo sikukuu!
Aaah wasubiri keshokutwa au j3 ili usije ukakosa hamasa.
 
Katika hali ya kusikitisha na kusononesha chuo kikongwa hapa nchini UDSM wanafunzi wake wanaendelea kuishi katika maisha magumu hii ni kutokana na serikali kuu na serikali yao DARUSO kutowajali wanafunzi wake. DARUSO imekaa kimya muda wote huku wanafunzi wakiangaika wenyewe na maisha magumu. Chuo hiki kina wanafunzi kama 19000 lakini mpaka sasa waliopewa mkopo ni 4138 22% ya wanafunzi wote.


Hii sio haki hata kidogo serikali ya KIkwete inatengeneza BOMU ambalo litakuja kuripuka soon.

Serikali inaongeza nguvu zake UDOM na kuiacha UDSM ikichakaa. Hii inaongeza chuki kwa Serikali ya kikwete kwa wasomi hawa.

Juzi nilikuwa chuo nikakutana na wadada kama watano wakasema wameenda LOAN BOARD kuulizia mikopo maana tokea waapply mwezi wa saba hawajapata mikopo, nikawauliza kwani loan board wamewaambiaje? eti wameambiwa kuwa waandike barua kwanin wapewe mikopo?


Source:Tanzania HESLB Website

Nilishajua kuwa hili litatokea
 
Back
Top Bottom