Thabit Madai
Member
- Oct 8, 2024
- 54
- 140
Simba kwa sasa haifungwi kwa makosa ya kiufundi ya Timu nzima bali inafungwa kwa makosa ya kibinadamu ya mchezaji mmoja mmoja kitu ambacho timu yoyote inaweza kupitia hiyo hali.
Tazama magoli yaliyoikesha alama 2 za Coastal Union kisha tazama bao la jana utagundua kwamba magoli waliyofungwa sio ya kitimu.
Hii ni hatua nzuri kwa ujenzi wa Timu na wanapaswa kutulia na kuongeza wachezaji wachache sana kwenye usajili dirisha lijalo.
Ukitoa bao la kujifunga hakuna moment ambayo Simba walionekana kuzidiwa na kuonesha utofauti wa daraja la ubora kati yao na Yanga ambao wana kikosi kilichokaa pamoja kwa muda mrefu.
Wakati Simba wanaanza kushuka na Yanga kutawala soka la Tanzania hivi karibuni dalili zilikuwa hizi hizi...kutoka kushinda kwa mbwembwe hadi kuomba Mungu mechi iishe.
Siku za mashabiki wa Simba kufurahi haziko mbali...na siku za mashabiki wa Yanga kutoka kinyonge Lupaso zipo karibuni.
Inaweza isiwe leo au kesho lakini hata Yanga wenyewe wanajua kuwa Simba hii sio ya miaka miwili nyuma...wameimarika sana!
✍️Sospeter Ilagila.