malaika wa habari njema
New Member
- Jun 20, 2024
- 1
- 0
KESHO YA TANZANIA INATEGEMEA MAENDELEO YA TEKNOLOJIA.
1.0. Utangulizi.
Teknolojia, kulingana na ensaiklopedia ya Britannica inaamanisha utumiaji wa maarifa ya kisayansi kwa vitendo kwaajili ya maisha ya mwanadamu au, kama inavyosemwa wakati mwengine, kwa mabadiliko na uendeshaji wa mazingira ya mwanadamu. Kati ya vitu vya msingi katika ulimwengu wa sasa ni teknolojia kupuuzia teknolijia katika zama hizi ni kufanya jaribio la kujiua. Maana kila kitu kinategemea teknolojia. Hivyo nchi ya Tanzania kama moja ya nchi zinazoendelea, Tukichukulia mfano wa gari kama maendeleo basi teknolojia ni kama injini. Teknolojia ni moja ya nyezo muhimu sana itakayoleta kasi kubwa sana katika safari ya maendeleo ya Tanzania. Serikali ya Tanzania imefanya mambo kadhaa katika jitihada za kukuza teknolijia baadhi ni kuwa na sekta inayotambulika rasmi kama sekta ya Teknolojia Habari na Mawasiliano (TEHAMA) Ikiendeshwa na Wizara ya Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari pia kuwepo na sera ya taifa ya TEHAMA iliyopitishwa 2003 (NICTP 2003) pia serikali ikaja na sera ya Taifa ya TEHAMA ya 2016.
2.0. Nafasi ya serikali katika kukuza teknolojia Tanzania.
Kuna uhitaji wa serikali kufanya mambo ya msingi kadhaa katika kukuza teknolojia ya nchi na kuongeza kasi ya maendeleo, mambo hayo ni kama yafuatayo,
Kuanzishwa kwa mtiririko wa tafiti shirikishi ili kuleta uvumbuzi wa kina. Tafiti ni moja wapo ya mambo muhimu sana katika ukuzi wa maarifa katika nyaja tofauti. Maarifa ni mapana hIvyo uhitaji tafiti za kina ilikuja na maarifa yenye masuluhisho katika jamii zetu. Tanzania inahitaji mtiririko wa tafiti katika eneo la sayansi na teknolojia hivyo basi serikali yahitaji kutoa msaada wa kifedha kwa wasomi watafiti ili kutoa motisha muhimu katika kuleta jitihada za wasomi hawa kwa madhumuni ya maendeleo ya kiteknolijia. Hizi tafiti zinabidi ziwe shirikishi kuhusianisha mabadilishano ya maarifa. mfano Japani ni moja ya nchi iliyofanikiwa sana katika teknolijia moja ya njia katika kufanikisha jambo hili kati ya miaka ya 1970 na 1980 wakaja na repoti zilizoitwa MITI ambazo zilianzisha programu maalumu ya kufadhili tafiti katika maeneo husika kama teknolojia ya viwanda na mawasiliano ya simu hivyo kuleta uvumbuzi mkubwa maeneo hayo.
Ubunifu katika kuingiza na kuboresha teknolojia kutoka nje ya nchi. Japani ni mfano wa nchi kubwa katika uwanda wa teknolojia, teknolojia nyingi za japani hazikutoka japani kwa asili lakini Japani ilikuwa kupaombele katika kutumia vyema teknolojia kutoka Marekkani na kuiboresha teknolojia hiyo kwa faida yao mfano katika Nyanja ya kujenga meli, katika ufundi huu wa meli baada ya vita ya pili ya dunia, Japani ilichukua teknolojia hiyo pale serikali ya Japan iliporuhusu kampuni ya Marekani ya ujenzi wa meli National Bulk Carrier Company kutumia kwa mda eneo la jeshi la maji la Japan katika sehemu iliyoitwa Kure kwa makubaliano ya kwamba wajenzi wa meli za Japani watapata teknolojia hizo bila kuzuiliwa. Tanzania pia tunanafasi ya kukuza teknolojia yetu kwa kuingia makubaliano ya faida na nchi mbali mbali ambazo zinaweza kuuza teknolojia na pia kwa ubunifu na utafiti kuwa na uwezo wa kuendeleza teknolojia hizo.
Uboreshaji wa elimu kwa vitendo, elimu ya Tanzania kwa asilimia kubwa imetawaliwa na elimu nadharia, wanafunzi kukaa madarasani nakujifunza bila vitendo, sasa ili kukuza teknolojia ya Tanzania inabidi serikali iwekeze katika kuboresha miundo mbinu ya elimu vitendo kwa kujenga mahabara nyingi husika na vifaa vya kutosha katika mafunzo, hili lifanyike katika ngazi zote za elimu kwanzia2 shule za msingi mpaka elimu ya juu, hii itawafanya wanafunzi kuifahamu teknolojia kwa undani na hata kuwa wabunifu, kuboresha elimu kunaweza kusaidia kukuza kizazi kitakachofanya mapinduzi ya teknolojia kwa sababau hawajifunzi kwa nadaharia lakini wanajifunza teknolojia halisi ili kutatua matatizo halisi yanayoikumba jamii.
3.0. Nafasi ya jamii katika ukuzaji wa teknolojia Tanzania.
Kesho ya Tanzania haijabebwa tu na serikali bali hata wananchi wa Tanzania wanajukumu la kuiendeleza nchi yao inapokuja, zifuatazo ni moja wapo za njia zinazoweza kutumiwa na jamii kuuza teknolojia ya nchi,
Kuibua kizazi cha uvumbuzi, ni jukumu la wanajamii kuibua kizazi ambacho kitakuwa na mtazamo chanya katika maswala ya sayansi na taknolojia kwa kuondoa dhana ya kuiona sayansi kama ni ngumu, mtazamo huo waweza kutolewa kupitia mafunzo ya wanajamii kwa watoto pia malezi, wazazi wanasehemu katika kuwalea watoto kwenye mazingira ya teknolojia ili Watoto wafahamu teknolojia kwa undani na kuleta ubunifu na uvumbui wa kina
Matumizi mazuri ya mtandao, Jamii ina nafasi ya kulaani matumizi mabaya ya mtandao na kuhamasisha matumizi mazuri ya mtandao kwenye jamii,matumiziz mazuri ya mtandao yanaweza kufanya vijana na Watoto kujifunza utashi na maarifa tofauti tofauti yanayoweza kuleta mabadiliko na kutatua ma
Kuhamasisha matumizi ya teknolojia katika kila nyaja ya jamii, jambo lolote lisipotumiwa huuoza au hufa, hivyo taasisi binafsi kama wadau wa teknolojia, viongozi katika jamii ikiwemo viongozi wa kifamilia, kijadi na wakidini kuhimiza matumizi ya kiteknolojia katika nyaja tofauti, mfano matumizi ya teknolojia katika mihadhara na mikutano ya dini na pia matumizi ya teknolojia katika shughuli tofauti tofauti zinazohiusisha jamii.
4.0. Hitimisho.
Teknolojia ni kiungo muhimu katika maendeleo ya Tanzania hivyo basi teknolojia inabidi uwe mwimbo wa Watanzania wote, si wale walio katika miji tu pia hata walio vijijini, hivyo basi serkali na wadau wa teknolojia bado wanajukumu kubwa la kupeleka teknolojia katika sehemu zote za nchi kupitia kuboresha elimu pia upatikanaji rahisi wa vifaa vya kiteknolojia. Licha ya teknolojia kuwa na matokeo chanya pia yanaweza leta changamoto kama uharifu wa mitandao, maadili kupolomoka, kupunguza fursa za ajira laikini kwa sera sahihi na uwekezaji mzuri hizi chngamoto zaweza kutatuliwa na kuifanya teknolojia kuwa nguvu kubwa ya maendeleo ya nchi.

Upvote
5