Kesi ambayo Mahakama Kuu Nchini Tanzania iliamua kwamba mtoto aliyezaliwa nje ya ndoa ana haki ya kurithi

Kesi ambayo Mahakama Kuu Nchini Tanzania iliamua kwamba mtoto aliyezaliwa nje ya ndoa ana haki ya kurithi

Joined
Apr 26, 2022
Posts
83
Reaction score
128
Ni kesi ya “JUDITH PATRICK KYAMBA versus (dhidi ya) TUNSUME MWIMBE AND 3 OTHERS, PROBATE AND ADMINISTRATION CAUSE (Shauri la Mirathi) NO. 50 OF 2016.”

Kutokana na upekee na umuhimu wa hii mada, nitakuwa natafsiri kwa kiswahili ili jamii kubwa zaidi iweze kuelewa.

This was a probate and administration cause in respect of the estate of the late Patrick Saul Kyamba, who died intestate. The deceased left eight issues. Among which, five issues were born out of wedlock.

(Hili lilikuwa shauri la mirathi ya marehemu Patrick Saul Kyamba, ambaye alifariki bila kuacha wosia, katika Hospitali ya Kairuki, Wilaya ya Kinondoni, Mkoa wa Dar es Salaam, tarehe 19, April, 2016. Marehemu aliacha watoto nane (8). Ambapo, watano kati yao walizaliwa nje ya ndoa).

The clan meeting proposed two names, Judith Patrick Kyamba and Tunsume Mwimbe to administer the estate. However, Judith Patrick Kyamba (a legitimate daughter & first born of the deceased) who was also an Advocate by profession, she secretly filed the petition, contending that she was the sole proposed administratrix.

(Kikao cha familia/ukoo kilipendekeza majina ya watu wawili kusimamia mirathi ya marehemu, Judith Patrick Kyamba na Tunsume Mwimbe. Lakini, Judith Patrick Kyamba (mtoto halali wa ndoa na wa kwanza katika familia ya marehemu, ambaye pia ni Wakili Msomi kitaaluma), akafungua kwa siri shauri la mirathi Mahakamani, akidai alikuwa msimamizi pekee wa mirathi aliyependekezwa).

Although it was found that the deceased left behind other issues, the petitioner told the court that, the said issues must have been born out of wedlock and hence illegitimate children. It was the contention of the Petitioner that, under the law, illegitimate children have no right to inherit.

(Hata baada ya kugundua kweli Marehemu alikuwa na watoto wengine aliowazaa nje ya ndoa, Judith aliiambia Mahakama kuwa, hao watoto wamezaliwa nje ya ndoa hivyo ni watoto haramu. Na kwamba, kisheria, watoto haramu hawana haki ya kurithi).

The Court (His Lordship Mlyambina, J.) held that: “With profound respect, I don't agree with the argument of the Petitioner that children born out of wedlock are illegitimate and they have no right to inherit the deceased estate. I find the Petitioner's arguments to be far away and out of touch of justice and realities. In fact, such argument is barbaric and discriminative in nature. The Constitution of the United Republic of Tanzania, 1977 guarantees equality of all human being under its Article 12 (1) and equality before the law under its Article 13 (1) and (2).

Mahakama Kuu, (kupitia Mheshimiwa Jaji Mlyambina) ikasema, “Sikubaliani na hoja za mfungua shauri kwamba watoto waliozaliwa nje ya ndoa ni haramu na hawana haki ya kurithi mali za marehemu. Hizo hoja ni za kizamani na haziafiakiani na haki na uhalisia. Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ya 1977 inasema binadamu wote ni sawa, chini ya Ibara ya 12(1) na kwamba watu wote ni sawa mbele ya sheria, chini ya Ibara ya 13(1) & ibara ndogo ya 2.”

Further, “Section 5(i) of the Law of the Child Act, 2009 prohibits discrimination to the child. Equally, section 10 of the law of the child guarantees a child a right to property of the parent. (Pia, kifungu cha 5(i) cha Sheria ya mtoto, ya mwaka 2009 kinakataza ubaguzi kwa mtoto. Vivyo hivyo, kifungu cha 10 cha sheria hiyo hiyo, kinampa mtoto haki ya kunufaika na mali za mzazi wake).

Pia Tanzania imeridhia na kusaini sheria au mikataba ya kimataifa ya haki za binadamu ambayo inalinda haki za mtoto. (Tanzania has ratified International Human Rights Instruments that guarantee the rights of the child).

Hivyo Mahakama ikasema, “kutokana na maendeleo hayo ya sheria za ndani na kimataifa, watoto waliozaliwa nje ya ndoa hawaitwi tena “MWANAHARAMU.” Ila ni watoto kama watoto wengine waliozaliwa ndani ya ndoa, wana haki sawa ikiwemo haki ya kurithi.

(With the afore development of national and international law, children born out of wedlock are no more referred to as “BASTARD”. They are equal children like those born in wedlock sharing equal rights including inheritance rights.”

Mahakama ikaendelea kusema “the issues born out of wedlock are innocent creatures. There is a Swahili phraseology “kitanda hakizai haram” which literally means there are no BASTARD children. But there are bastard parents. The child is not culpable for its parents’ shortcomings nor can he or choose the situation they are born into.

Thus, it is not a child's fault being born in the situation. Children born out of wedlock are the biological children just like those born within the matrimonial home. They are entitled to equal shares of their common father with fellow siblings.”

Kwamba, “Watoto waliozaliwa nje ya ndoa ni viumbe wasio na hatia. Kuna msemo wa Kiswahili unasema, ‘Kitanda hakizai haramu. Maana yake HAKUNA MTOTO (mwana) HARAMU, ILA KUNA WAZAZI HARAMU.

Mtoto hawezi kulaumiwa kwa makosa ya wazazi wake wala hawezi kuchagua hali anayozaliwa nayo. Hivyo sio makosa ya mtoto kuzaliwa katika hali hiyo. Watoto waliozaliwa nje ya ndoa ni watoto kibayolojia kama wale waliozaliwa ndani ya ndoa. Wanastahili mgao sawa wa baba yao pamoja na ndugu zao.

-THE END-

Imeletwa kwako nami Zakaria. (0754575246).
 
Back
Top Bottom