Kesi dhidi ya JamiiForums: Shahidi adai waliomba taarifa za mteja bila kutaja ni kwa mujibu wa sheria gani

Kesi dhidi ya JamiiForums: Shahidi adai waliomba taarifa za mteja bila kutaja ni kwa mujibu wa sheria gani

TZ TZ nakupenda kwa moyo wote lakini kwenye law enforcement units ni hakuna kitu wote yaani wote nivilaza sana!

Bora Hakimu atupilie mbali hii kesi!
 
Halafu ukichunguza maswali ya Kibatala, utagundua kabisa kwamba, kuna hila na inda zilizofichika moyoni mwa huyo ASP. Lakini maswali yanalazimisha kilichofichwa moyoni kwa hila, kianikwe hadharani.

Mtu hata akuropokee jambo linalohusu hujuma fulani mahala pa kazi, hauwezi kuanzisha upelelezi wako kwa kubweteka jinsi hiyo kwa kumwita mropokaji ili "akueleze vizuri"! Hatua hiyo tayari inahatarisha usalama wa "raia mwema."

Cha muhimu kilichotakiwa kufanyika pale, ni kufuatilia sehemu iliyotuhumiwa kwanza ili kuupata ukweli wa jambo linalotolewa tuhuma.

Waliotakiwa kulalamika na kushitaki katika kesi hii, labda kwa kuharibiwa jina na biashara ni hao oil com. Ambao hawaonekani popote kulalamika katika kesi hii.

Cha kujiuliza, iweje walalamishi wa kesi wawe polisi?
Kuna nini kilichojificha kwenye "sosi" ya kesi hii?
Wanaoisaidia polisi kwa kuwapa "tip", leo ndiyo walalamikiwa na ni washitakiwa.

Ninashukuru maswali yote yanayosumbua vichwa vya watu kuhusu weledi wa utendaji kazi wa polisi yameulizwa.

Baada ya kesi hii kuisha kuna watu watakaobaki "uchi" na kushindwa kuoata sehemu ya kuficha aibu zao.
 
Sheria ya kiislamu inasema kuwa ushahidi wa mwanaume mmoja ni sawa na ushahidi wa wanawake wawili, sasa wale wanaotafakari wanajua nimemaanisha nini na hapo sheria yetu tukufu ya kiislamu imeprove nini.

Haya sasa, hapo mawakili wa utetezi wameenda wanamkoroga huyo mama na yeye anaenda anajaa tu!
 
Peter Kibatala unavyomfanyia huyo Fatuma sio poa kabisa, Mungu anakuona ujue.

Kumbuka huyo ni Mtu ana familia inayomtegemea na ndugu zake pia wanaomuamini.

Na tukiachana kuwa kambi tofauti katika hii kesi, lakini huyo ni Mtanzania mwenzako ndugu yangu.

Usimfanye aonekane si kitu wakati kwenye kitengo chake anategemewa na cheo kapandishwa.

Halafu ni mtoto wa kike, kumbana bana na maswali namna hiyo sio poa aisee. Inawezekana hata hujui anaumwa nini waweza kumsababishia msongo wa mawazo mdada wa watu ikawa shida kaka.

Sidhani kama Barcelona wanaweza kupanga kikosi kamili pale wanapocheza na Lipuli FC au RTC Kagera utadhani wanaenda kucheza na Real Madrid, hii mechi ni ndogo sana na in fact ilishaisha kabla hata haijaanza, msamehe tu dada wa watu hatorudia tena nadhani.
 
Hiv kwa maswali hayo hua mnapaga hata maji ya kunywa kwanza hao viherehere wanaojiita mashahidi ? maana si kwa maswali hayo aise
 
yaani hapo tu ndo shahidi unapotoka baruti mahakani na kutokomea kusikojulikana
 
Kwa maswali ya kibatala sijui kama uyo mama ajaingia kwenye period.
I am proud to be JF expert member
 
Kibatalaaaa dah alivyomchambua kama karanga Askari wa watu mpaka aibu mama yupo hoi hapo
 
Halafu ukichunguza maswali ya Kibatala, utagundua kabisa kwamba, kuna hila na inda zilizofichika moyoni mwa huyo ASP. Lakini maswali yanalazimisha kilichofichwa moyoni kwa hila, kianikwe hadharani.

Mtu hata akuropokee jambo linalohusu hujuma fulani mahala pa kazi, hauwezi kuanzisha upelelezi wako kwa kubweteka jinsi hiyo kwa kumwita mropokaji ili "akueleze vizuri"! Hatua hiyo tayari inahatarisha usalama wa "raia mwema."

Cha muhimu kilichotakiwa kufanyika pale, ni kufuatilia sehemu iliyotuhumiwa kwanza ili kuupata ukweli wa jambo linalotolewa tuhuma.

Waliotakiwa kulalamika na kushitaki katika kesi hii, labda kwa kuharibiwa jina na biashara ni hao oil com. Ambao hawaonekani popote kulalamika katika kesi hii.

Cha kujiuliza, iweje walalamishi wa kesi wawe polisi?
Kuna nini kilichojificha kwenye "sosi" ya kesi hii?
Wanaoisaidia polisi kwa kuwapa "tip", leo ndiyo walalamikiwa na ni washitakiwa.

Ninashukuru maswali yote yanayosumbua vichwa vya watu kuhusu weledi wa utendaji kazi wa polisi yameulizwa.

Baada ya kesi hii kuisha kuna watu watakaobaki "uchi" na kushindwa kuoata sehemu ya kuficha aibu zao.
Asante Sana Mkuu,
Nimekuelewa Vyema.
 
Back
Top Bottom