Halafu ukichunguza maswali ya Kibatala, utagundua kabisa kwamba, kuna hila na inda zilizofichika moyoni mwa huyo ASP. Lakini maswali yanalazimisha kilichofichwa moyoni kwa hila, kianikwe hadharani.
Mtu hata akuropokee jambo linalohusu hujuma fulani mahala pa kazi, hauwezi kuanzisha upelelezi wako kwa kubweteka jinsi hiyo kwa kumwita mropokaji ili "akueleze vizuri"! Hatua hiyo tayari inahatarisha usalama wa "raia mwema."
Cha muhimu kilichotakiwa kufanyika pale, ni kufuatilia sehemu iliyotuhumiwa kwanza ili kuupata ukweli wa jambo linalotolewa tuhuma.
Waliotakiwa kulalamika na kushitaki katika kesi hii, labda kwa kuharibiwa jina na biashara ni hao oil com. Ambao hawaonekani popote kulalamika katika kesi hii.
Cha kujiuliza, iweje walalamishi wa kesi wawe polisi?
Kuna nini kilichojificha kwenye "sosi" ya kesi hii?
Wanaoisaidia polisi kwa kuwapa "tip", leo ndiyo walalamikiwa na ni washitakiwa.
Ninashukuru maswali yote yanayosumbua vichwa vya watu kuhusu weledi wa utendaji kazi wa polisi yameulizwa.
Baada ya kesi hii kuisha kuna watu watakaobaki "uchi" na kushindwa kuoata sehemu ya kuficha aibu zao.