PreGE2025 Kesi iliyofunguliwa na Saidi Issa na wenzake wawili (2) dhidi ya CHADEMA yaahirishwa. Jaji ashindwa kufika mahakamani

PreGE2025 Kesi iliyofunguliwa na Saidi Issa na wenzake wawili (2) dhidi ya CHADEMA yaahirishwa. Jaji ashindwa kufika mahakamani

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Ni kwa kuchapana na kuuana tu. Baada ya hapo ndiyo tutapata katiba mpya itakayoua mifumo kandamizi.

.Maana prof. Anna Tibaijuka alishasema, "kupata katiba mpya ktk mazingira ya amani tutasubiri sana"
Watanzania wengi Bado ni mashujaa ndani ya box hivyo hizo levo Bado sana. Kitu kinachotuasiri ni Nyerere kukopi kutoka u Soviet namna ya kudeal na vuguvugu lolote likiwa Bado kwenye comfort zone na kuliteketeza.
 
Mahakama bongo sijawahi iamini. I'm definitely right ✅️
Nikiwa yanki mdogo naanza kujitafuta, kuna mshikaji alinitenda vibaya sana kibiashara, nikaenda mahakamani nikaangukia pua, akapeleka mkono basi haki ile sikupewa. Nimepiga kimya mpaka leo.

Mahakama bongo inaweza najisiwa kifedha au kisiasa. Tuna safari ndefu sana bongo hii.
 
Wakuu,

Siku ya leo ndo ile siku ambayo Mahakama itaanza kusikiliza kesi ya CHADEMA baada ya kushtakiwa na wanachama wao wa Zanzibar kwamba wanatumia mali za chama vibaya

==============
Alichoandika Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, John Heche

Kesi ya kina Said Issa ni Kesi ya kisiasa kujaribu kuzuia chama chetu kufanya shughuli zake halali..
Jaji aliepanga Kesi leo anakosaje kuwepo mahakani siku ya Kesi tena Kesi muhimu kama hii kwa Nchi?

Jaji aliefanya maamuzi ya haraka na kutoa maamuzi tena bila hata upande wetu kuwa na uwakilishi wa wanasheria!!

Mahakama ya Tanzania isikubali kutumiwa na wanasiasa ambao wameshindwa kufanya kazi za siasa za kushawishi umma.


==========================
Shauri ambalo limetoa zuio kwa Chadema kufanya siasa limeahirishwa ikidaiwa Jaji ana majukumu mengine

Kesi namba 8323/2025 ambayo imetoa zuio la muda kwa Chama cha Chadema kufanya shughuli zozote zile kiutendaji na oparesheni mpaka pale kesi ya msingi iliyofunguliwa itakapoanza kusikilizwa, imeahirishwa mpaka Julai 10, 2025 kutokana na Mh. Jaji Hamidu Mwanga anayesikiliza kutokuwepo.

Katika kesi hiyo ambayo imetajwa leo June 24, 2025 kwa ajili ya kusikilizwa, ilifunguliwa na aliyewahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Zanzibar, Saidi Issa Mohamed na wenzake wawili (2) dhidi ya Baraza la Wadhamini na Katibu Mkuu wa CHADEMA.

Akizungumzia shauri hilo baada ya shauri kuahirishwa Wakili Utetezi, Hekima Mwasipu amesema kuwa Jaji hajatokea Mahakamani ikidaiwa kuwa yupo na majukumu mengine.

Ikumbukwe Shauri hilo lilikuja kufuatia maombi yaliyowasilishwa Mahakamani hapo na Mawakili wa waleta maombi wakiongozwa na Wakili Gido Thomas Simfukwe ambao waliiomba Mahakama kuweka zuio hilo hadi kesi ya msingi itakapoanza kusikilizwa.

Kwenye kesi ya msingi waleta maombi wamewasilisha madai kuwa CHADEMA imekuwa ikiitenga Zanzibar katika masuala mbalimbali ikiwemo mgawanyo wa raslimali fedha n.k .

Pia soma Pre GE2025 - Mnyika ashangazwa na kitendo cha Jaji kutokufika mahakamani
Namna waislamu wanavyo tumika kipumbavu na mafisadi na mabeberu
 
Hii ni aibu jamani kwa mahakama na jaji aliyekimbia kesi
 
Shida ya CHADEMA ni kutofanyia ushauri kwa wakati mnaopewa humu. Huyo hakimu yupo kwa ajili ya kuidhoofisha CHADEMA hivyo harakati za kupambana nao zinatakiwa kuwa za papo kwa hapo. CHADEMA imfungulie kesi huyo hakimu, na hao viongozi kutoka Zanzibar ilmradi nao wapate usumbufu wa kwenda mahakamani kusikiliza kesi Yao. Similar CHADEMA imfungulie kesi yule hakimu na mawakili wa serikali kwa kuchelewesha kesi ya Tundu Lissu ilmradi kwa majina Yao na wao wapate usumbufu wa kwenda mahakamani kusikiliza kesi zao. Kwa kesi hizi lazima watumishi wa mahakama wataanza kuwa na adabu. CHADEMA isikubali Kila siku TU yenyewe ndio inakuwa mhanga wa kupelekwa mahakamani na kuzungushwa kwa kupigwa tarehe.
Wewe sio CDM??kwa Nini???,😂😂😂😂😂😂
 
Tangu majuzi tulijua hatafika so sio big deal, wanatabirika sana sisiemu na majaji wao
 
Back
Top Bottom