Kesi kifo cha Kanumba yaingia sura mpya

Kesi kifo cha Kanumba yaingia sura mpya

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440
Jipya! Baada ya kimya cha muda mrefu, imefichuka kwamba kesi ya kuuawa kwa aliyekuwa staa mkubwa wa sinema za Kibongo, marehemu Steven Charles Kanumba ' The Great' imechukua sura mpya baada ya kuanza kusikilizwa kimyakimya, Ijumaa Wikienda limenasa kinachoendelea .

Staa wa sinema za Kibongo , Lulu Elizabeth Michael , ' Lulu ".

WATU WANATAKA KUJUA KINACHOENDELEA

Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kwamba watu wengi wana kiu ya kujua kinachoendelea katika kesi hiyo ambapo ilidaiwa kwamba imehamishwa eneo la wazi ( open) na kusikilizwa kimyakimya katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, huku usikilizwaji wa kesi hiyo ukiwa tofauti kama ilivyozoeleka.

Kwa mujibu wa shushushu wetu anayependa kufuatilia maisha ya mastaa wa tasnia tofauti tofauti Bongo ndani ya mahakama hiyo, chombo hicho cha kusimamia sheria kimeamua kubadili aina ya usikilizaji wa kesi hiyo. Wakili maarufu Bongo anayemtetea ' Lulu ' , Peter Kibatala .

YAHAMISHIWA BARAZA LA KESI ZA MAUAJI

Habari zilieleza kwamba, kwa sasa kesi hiyo itakuwa ikisikilizwa kwenye kikao cha baraza la kusikiliza kesi za mauaji kwenye mahakama hiyo, kwa lugha ya kigeni kinaitwa High Court Murder Session . "Kama ukienda pale mahakamani ili kufuatilia mwenendo wa kesi hiyo, huwezi kufanikiwa kupata chochote kwa sababu ipo kwenye baraza la kusikiliza kesi za mauaji yaani High Court Murder Session ambalo huwa linasikiliza kesi kimyakimya tofauti na kesi nyingine zinazosikilizwa kwenye kizimba, " kilisema chanzo chetu hicho.

ETI LULU HAJUI KINACHOENDELEA

Uchunguzi wetu ulibaini kwamba wakati hayo yakiendelea kortini hapo, aliyekuwa mwandani wa Kanumba aliyekuwa naye chumbani siku ya kifo, Elizabeth Michael ' Lulu' hajui chochote kinachoendelea na wala hajaitwa mahakamani. Mama mzazi wa marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa. "Tangu imeanza kusikilizwa hakuna siku Lulu ameitwa na sidhani kama anajua kinachoendelea . "Labda anayejua kinachoendelea ni mama Kanumba ( Flora Mtegoa ) ambaye hupenda kuulizia kuhusu hatima ya mwanaye," kilisema chanzo hicho.

WAKILI KIBATALA ANASEMAJE?

Baada ya kujikusanyia data hizo , Ijumaa Wikienda lilimtafuta wakili maarufu Bongo anayemtetea Lulu, Peter Kibatala ili kupata ufafanuzi wa aina hiyo ya usikilizwaji wa kesi ya mteja wake ambapo alifichua siri hiyo juu ya kesi ya kifo cha Kanumba. Wakili Kibatala alikiri kwamba kesi ya kifo cha Kanumba ambayo Lulu ni mshitakiwa wa kwanza akituhumiwa kuua bila kukusudia, imebadilishwa aina ya uitwaji huku akigoma kuingia kiundani kwani bado kesi hiyo ni mbichi na hairuhusiwi kwa wakili kuzungumza nje ya mahakama.

Aliyekuwa staa mkubwa wa sinema za Kibongo , marehemu Steven Charles Kanumba ‘The Great' enzi za uhai wake. "Ni kweli inaitwa hivyo, huyo aliyekueleza hajakosea na tunategemea mwezi huu wa nane kikao cha baraza hilo la usikilizaji kitaendelea lakini nisingependa kuongea sana kwani mimi siyo msemaji wa Lulu bali ni wakili na si maadili ya kazi yangu kuzungumza nje ya mahakama.

Hata Lulu haruhusiwi kuzungumza chochote nje ya mahakama, " alisema Kibatala aliyewahi kuwa wakili wa mwigizaji Kajala Masanja na mwanahip - hop , Waziri Makuto ' Lord Eyez ' . TUMGEUKIE LULU Mwanahabari wetu alipomtafuta Lulu ili kujua kama anajua chochote juu ya kesi hiyo, mkali huyo wa sinema za Kibongo aligoma kuzungumza chochote kama aliyoelekezwa na wakili wake, Kibatala .

TUJIKUMBUSHE

Kanumba aliyewatoa mastaa wengi wa filamu unaowaona kwa sasa , alifariki dunia April 7, 2012 nyumbani kwake, Vatican- Sinza jijini Dar . Kifo cha Kanumba kilidaiwa kwamba kilitokana na kuangukia sehemu ya nyuma ya kichwa ambapo alipata mtikisiko wa ubongo kisha kuzikwa kwenye Makaburi ya Kinondoni, Dar.
 
Lulu alimkatili Kanumba aisee sasa hivi tungekua tunaangalia filamu kibaooo
 
Yaani lulu bwana......mwanaume kakasirika yy anamsukuma badala yakumpa kitu roho inapenda.
 
Acha basi kunichekesha,je na jini akivuka barabara et anageuka kuangalia gari ndio avuke halaf eti ni jinii

umeona eeenh kisha tunanunua muvi zao ukikutana nao full maringo mara cjui wametafna rambirambi ni sheeeeder aisee kwa sasa naangalia seriez ya arrow/green garnet karibu sana
 
Shangaaa badala angeinama tu kanumba akapitiliza kwenye mlango wa joto unadhan yote hayo yangetokeaa, hasira chumban wakati humo ni raha tu

Hajiwez huyo.......me ningevua nguo zangu ningeanza kufanya mazoezi,mwenye angenijoin!!!
 
Kesii hii ilishaisha kitambo..mie naona tu wanatupumbaza..mama kanumba yuko peace na lulu jamanii..sasa sijui huyo anayemshtaki nanii..nahisi hapo wanakamilisha taratibu za kesi tu..R.I.P Kanumba
 
Lulu alimkatili Kanumba aisee sasa hivi tungekua tunaangalia filamu kibaooo

TEAM KANUMBA hatukubali mpaka bibie afie jela, maana mwenyew kanumbe wetu kafa yeye kutwa yupo instagram anajipiga ma selfies, roho zinatuuma katuulia jembe letu mbwa huyu
 
TEAM KANUMBA hatukubali mpaka bibie afie jela, maana mwenyew kanumbe wetu kafa yeye kutwa yupo instagram anajipiga ma selfies, roho zinatuuma katuulia jembe letu mbwa huyu

Yaan mi tokea hapo sikapendi ka Lulu bora kangededi kenyewe tu mfyuuuuuuuuu
 
Kesii hii ilishaisha kitambo..mie naona tu wanatupumbaza..mama kanumba yuko peace na lulu jamanii..sasa sijui huyo anayemshtaki nanii..nahisi hapo wanakamilisha taratibu za kesi tu..R.I.P Kanumba

Lulu anashtakiwa na Jamhuri, mama Kanumba hausiki kwa lolote kwenye kesi hii.

Bahati ya Lulu kwenye kesi hii hakuna eye witness na hiyo ni fursa ya kuieleleza mahakama Kanumba alitaka kumbaka au kula tigo kinguvu na tukio limetokea Lulu akiwa under 18. kimsingi kesi imekwisha hapo.
 
Usihukumu na usipende kupita kiasi ukasahau hata wewe unaweza kupatwa na mkasa ule, Lulu hakupiga risasi wala kisu jiulize mtu anadondoka kutoka gorofani na anapona Kanumba kala mweleka tu kwenye floor kafa hapohapo, Think big

Hako kalimpiga na rungu Kanumba amekufa na yake moyoniii sema wanakaziba ziba ili kaonekane hakana hatiaa ingekua US kangeozea jela sema Tanzania kila sehemu rushwaa
 
Back
Top Bottom