Kesi kuhusu kujiuzulu Spika: Mbatia atabezwa, lakini ana hoja

Mwenyekiti wa Taifa wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia ametinga Mahakama Kuu ya Tanzania na ameshafungua kesi ya kikatiba kuhusu kujiuzulu kwa Spika Job Yustino Ndugai. Kwa taarifa nilizonazo binafsi, tayari kesi husika imeshasajiliwa na imepangiwa jopo la Majaji watatu la kuisikiliza kesi hiyo. Wakati kesi hiyo ikiwepo mahakamani, tayari CCM na ADC wameshawapitisha wagombea wao wa nafasi ya Spika wa Bunge.

Nimekuwa nikifuatilia maoni ya watanzania na wasio watanzania kwenye mitandao ya kijamii, mitaani, runingani na redioni kuhusu kesi iliyofunguliwa na Mbatia. Wengine wanamuona Mbatia akitaka Ndugai abaki kuwa Spika wa Bunge kwa njia ya Mahakama. Wapo wanaomuona Mbatia kama anayepoteza muda na 'fedha' zake kwa jambo lisilo na maana na kuwa jambo hilo limeshapitwa na wakati. Wapo wanaompongeza. Lakini, wengi wanambeza.

Suala la utetezi wa Katiba ni suala kubwa na la muhimu kwa kila mmoja wetu. Kila mtanzania, kwakuwa Katiba ni sheria yetu mama, anapaswa kuilinda na kuitetea katiba yetu. Katiba inapotoa masharti ya kufuatwa, lazima yafuatwe. Katiba imetoa masharti ya kufuatwa na Spika anayetaka kujiuzulu. Ni lazima yafuatwe. Mbatia ameona hayakufuatwa. Amekwenda mahakamani kuitetea na kuilinda Katiba yetu iliyotoa masharti ambayo ameona yamekiukwa. Ni haki yake na anafanya jambo jema.

Viongozi wetu, wanapoapishwa, huapa kuilinda na kuitetea Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Sheria zote nyinginezo ( zinazotungwa na Bunge na zile Ndogondogo) hazipaswi kukinzana na Katiba. Pale zinapokuwa kimya, Katiba hutumika. Haipendezi kushabikia viongozi ambao hawaifuati Katiba yetu kwa minajili ya kuilinda na kuitetea kama walivyoapa. Tena, viongozi wenyewe ni wale wanaotokea kwenye Bunge ambalo ndilo linalotunga sheria.

Si sawa Athumani, aliyedhaminiwa na Musa kupata kazi kwa Ally, kuandika barua yake ya kuacha kazi akiielekeza kwa Musa huku akitoa nakala tu kwa Ally-mwajiri wake. Hapo, aliyepaswa kuandikiwa barua husika ni mwajiri ambaye ni Ally na nakala inaweza kuelekezwa kwa Musa ikimpendeza Athumani. Kimsingi, Mbatia ana haki na hoja za kufungua shauri lake Mahakama Kuu ya Tanzania kupata tafsiri ya kikatiba juu ya suala hilo. Atabezwa lakini atabaki na hoja yake.
Nakuunga mkono.
Kuna maswali mengi sana.Je ni wakati sasa wa Spika kulindwa na sheria kwama hata chama chake kikimfukuza ado awe na uwezo na haki ya kuendelea kuwa spika?
Sisi werevu tunaamni kwamba Mbatia anayo HOJA.Ni suala la muda tu.Ni wajibu wetu kutetea lkatia yetu
 
Something somewhere is boilling....Mbatia aka mama tanzania ni nani kamtuma kufanya hivyoo
Wepi waliochangia pesa
Naona kama vile wabunge wengi hawamtaki Tulia,choice yao ni Kashilila/Chenge ndiyo maana wakachukua fomu.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Mwenyekiti wa Taifa wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia ametinga Mahakama Kuu ya Tanzania na ameshafungua kesi ya kikatiba kuhusu kujiuzulu kwa Spika Job Yustino Ndugai. Kwa taarifa nilizonazo binafsi, tayari kesi husika imeshasajiliwa na imepangiwa jopo la Majaji watatu la kuisikiliza kesi hiyo. Wakati kesi hiyo ikiwepo mahakamani, tayari CCM na ADC wameshawapitisha wagombea wao wa nafasi ya Spika wa Bunge.

Nimekuwa nikifuatilia maoni ya watanzania na wasio watanzania kwenye mitandao ya kijamii, mitaani, runingani na redioni kuhusu kesi iliyofunguliwa na Mbatia. Wengine wanamuona Mbatia akitaka Ndugai abaki kuwa Spika wa Bunge kwa njia ya Mahakama. Wapo wanaomuona Mbatia kama anayepoteza muda na 'fedha' zake kwa jambo lisilo na maana na kuwa jambo hilo limeshapitwa na wakati. Wapo wanaompongeza. Lakini, wengi wanambeza.

Suala la utetezi wa Katiba ni suala kubwa na la muhimu kwa kila mmoja wetu. Kila mtanzania, kwakuwa Katiba ni sheria yetu mama, anapaswa kuilinda na kuitetea katiba yetu. Katiba inapotoa masharti ya kufuatwa, lazima yafuatwe. Katiba imetoa masharti ya kufuatwa na Spika anayetaka kujiuzulu. Ni lazima yafuatwe. Mbatia ameona hayakufuatwa. Amekwenda mahakamani kuitetea na kuilinda Katiba yetu iliyotoa masharti ambayo ameona yamekiukwa. Ni haki yake na anafanya jambo jema.

Viongozi wetu, wanapoapishwa, huapa kuilinda na kuitetea Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Sheria zote nyinginezo ( zinazotungwa na Bunge na zile Ndogondogo) hazipaswi kukinzana na Katiba. Pale zinapokuwa kimya, Katiba hutumika. Haipendezi kushabikia viongozi ambao hawaifuati Katiba yetu kwa minajili ya kuilinda na kuitetea kama walivyoapa. Tena, viongozi wenyewe ni wale wanaotokea kwenye Bunge ambalo ndilo linalotunga sheria.

Si sawa Athumani, aliyedhaminiwa na Musa kupata kazi kwa Ally, kuandika barua yake ya kuacha kazi akiielekeza kwa Musa huku akitoa nakala tu kwa Ally-mwajiri wake. Hapo, aliyepaswa kuandikiwa barua husika ni mwajiri ambaye ni Ally na nakala inaweza kuelekezwa kwa Musa ikimpendeza Athumani. Kimsingi, Mbatia ana haki na hoja za kufungua shauri lake Mahakama Kuu ya Tanzania kupata tafsiri ya kikatiba juu ya suala hilo. Atabezwa lakini atabaki na hoja yake.
Mbatia yuko sawa na hapa ndipo tutaona kama majaji wanasimama kwenye nafasi yao bila woga. Tunajua jinsi viongozi wanaweza kupuuza katiba. Mzee ruksa enzi zake badala ya kuangalia katiba aliruhusu znz kuingia oic. Juzi hapa tumeona samia kinyume na kiapo cha urais anaruhusu vigogo kula hela ya umma kwa kiasi mradi wasivimbiwe.
Hili la spika limeelekezwa kwenye katiba akijiuzulu anajiuzulu kwa nani.
Wengi tulistaajabu kuona spika mtumishi wa serikali anapeleka barua kujiuzulu kwa katibu wa chama chake. Kuweka nakala kwa katibu wa bunge haimanishe ameandika barua kwake.
Kama nikuheshimu utawala wa sheria kiti cha spika hakiko wazi kwa sababu ndugai bado hajajiuzulu.
 
Katika hili, mimi naona kama Mh. Mbatia amekosea focus, kama kweli nia yake ni hiyo. Yeye alitakiwa akafungue kesi ya kuzuia mchakato wa kumpata spika mpya, kama anaona yule wa zamani hajajiuzulu, na si kwenda kumtaka aliyejiuzuru ajiuuzulu kisahihi; akigoma je? Huyu mtu ameshaachia ngazi na hiyo post haihitaji, kama amekosea utaratibu wa kujiuzulu basi anaweza akaamua atakavyo.

Iwapo Mbatia angefungua kesi ya kuzuia mchakato wa kumpata spika mpya, mamlaka husika zingemgeukia yule aliyejiuzulu na kumtaka ajiuzulu kulingana na utaratibu. Mh. Mbatia hana mamlaka yoyote kisheria ya kumlazimisha Mh. Ndugai ajiuzulu kwa kufuata Katiba. Unless kama anatarjia hukumu ya Mahakama ya kumlazimisha Mh. Ndugai ajiuzulu kwa kufuata utaratibu, asuming kweli utaratibu haukufuatawa
 
Upuuzi kama huu alioufanya Mbatia inapaswa mahakama itakapo tupilia mbali upuuzi huu wa kesi imuonye vikali na pia alipe gharama kwa upuuzi wake wa kuisumbua mahakama na majaji kwa upuuzi wake.
 
Suppose speaker akufuata katiba kwenye kujiudhuru. What outcome is Mbatia seeking iwapo Ndugai hana interest ya kuwa speaker tena?

Anataka Ndugai aandike barua kwa taratibu sahihi? and then what?

The only logical explanation of going through all this trouble iwapo Ndugai angekuwa interested.

Otherwise maamuzi yoyote ya mahakama speaker atakuwa Dr Tulia mwisho wa siku I do not see CCM kurudia mchakato wa kupendekeza jina la speaker, hakuna mtu atafukuzwa kazi, hakuna sheria itabadilishwa, and so forth it changes nothing in the end. Zaidi ya speaker kujiudhuru kama wanavyotaka.

Now that is a waste of court time and resources kusikiliza case kama hizo.
Suala la kutetea katiba halitegemei matokeo yanayotamaniwa. Hapa kuna mising ya ki precedent inajengwa kwa mahitaj ya haki na utawala bora leo na baadae. Ndo maana hata wapinzan hawampend ndugai lakin wanashikiria hoja za kikatiba. Ukimwangalia ndugai hutaelewa Mbatia. Ukiangalia kwa jicho la kuheshim sheria utaelewa. Hakuna anayemtetea Ndugai kwanza kachelewa kutoka. Inatetewa sheria ya nchi.
 
Mwenyekiti wa Taifa wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia ametinga Mahakama Kuu ya Tanzania na ameshafungua kesi ya kikatiba kuhusu kujiuzulu kwa Spika Job Yustino Ndugai. Kwa taarifa nilizonazo binafsi, tayari kesi husika imeshasajiliwa na imepangiwa jopo la Majaji watatu la kuisikiliza kesi hiyo. Wakati kesi hiyo ikiwepo mahakamani, tayari CCM na ADC wameshawapitisha wagombea wao wa nafasi ya Spika wa Bunge.
Ngoja kidogo, spika Ndugai alikuwa right kabisa, katiba inasema barua ya kujiuzulu ataiwasilisha kwenye bunge na alifanya hivyo,kayiba haisemi barua ataikabishi kwenye mkutano wa bunge, sasa asingeweza kuipeleka kwenye kikao cha bunge wakati kikao cha bunge hakijaitwa
 
Mwenyekiti wa Taifa wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia ametinga Mahakama Kuu ya Tanzania na ameshafungua kesi ya kikatiba kuhusu kujiuzulu kwa Spika Job Yustino Ndugai. Kwa taarifa nilizonazo binafsi, tayari kesi husika imeshasajiliwa na imepangiwa jopo la Majaji watatu la kuisikiliza kesi hiyo. Wakati kesi hiyo ikiwepo mahakamani, tayari CCM na ADC wameshawapitisha wagombea wao wa nafasi ya Spika wa Bunge.
Wakati ndugai akiwapa ubunge wale kovid 19, Mbatia alikuwa wapi kwenda mahakamani HAKUJUA KUWA NDUGAI KAVUNJA KATIBA.BUNGE bila ndugai litakuwa bora.mtenda hutendwa .MTOA MAADA UNAUNAFIKI NDANI YAKO
 
Suppose speaker akufuata katiba kwenye kujiudhuru. What outcome is Mbatia seeking iwapo Ndugai hana interest ya kuwa speaker tena?
Kila mtu ana wajibu wa kuilinda katiba...

So, this is not about Ndugai aendelee kuwa spika or otherwise. Mbatia anatekeleza wajibu wake kujaribu kila njia kuitetea na kuilinda katiba kama RAIA...

Mbatia yuko kwenye right track. Sisi kama hatuwezi kuungana naye huko mahakamani, tumuunge mkono hata kimoyo moyo tu...

Kumbeza ua kunyamaza kimya ni kukimbia wajibu wetu muhimu ni wa haki..
Anataka Ndugai aandike barua kwa taratibu sahihi? and then what?
Atimize matakwa ya kikatiba. Atimize HAKI na TARATIBU yote...
The only logical explanation of going through all this trouble iwapo Ndugai angekuwa interested.
This not about Ndugai's interests. It's about protecting the constitution...!
Otherwise maamuzi yoyote ya mahakama speaker atakuwa Dr Tulia mwisho wa siku I do not see CCM kurudia mchakato wa kupendekeza jina la speaker,
Haijalishi mahakama itaamua nini. Haijalishi wenye mamlaka watatii maamuzi ya mahamakama au la. Kinachojalisha hapa ni kuweka kumbukumbu sawa kwa upcoming generations kuwa, the mistake was made. The court corrected it. The decision makers ignored and continued to their corruption...!
hakuna mtu atafukuzwa kazi
It does not matter. Soma hapo juu...
hakuna sheria itabadilishwa, and so forth it changes nothing in the end. Zaidi ya speaker kujiudhuru kama wanavyotaka.
Again, it does not matter. What matters, is that, jamii ijue na itambue kuwa pamoja na makosa ya kijinga na kipumbavu ya wàtawala wa kizazi hiki, bado walikuwepo watu wenye akili walioyapinga na kuyakataa makosa yao. Ni kuweka precedence kwa usahihi...
Now that is a waste of court time and resources kusikiliza case kama hizo.
Really?

It's because you àre built and accustomed to the "very bad and danger socio - cultural practices" like this one. Ndiyo maana una ujasiri wa kutetea makosa kwa kisingizio cha "..ili iweje?"

It's because you always (may be) used to get anything cheaply...!!
 
Mwenyekiti wa Taifa wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia ametinga Mahakama Kuu ya Tanzania na ameshafungua kesi ya kikatiba kuhusu kujiuzulu kwa Spika Job Yustino Ndugai. Kwa taarifa nilizonazo binafsi, tayari kesi husika imeshasajiliwa na imepangiwa jopo la Majaji watatu la kuisikiliza kesi hiyo. Wakati kesi hiyo ikiwepo mahakamani, tayari CCM na ADC wameshawapitisha wagombea wao wa nafasi ya Spika wa Bunge.

Athumani. Kimsingi, Mbatia ana haki na hoja za kufungua shauri lake Mahakama Kuu ya Tanzania kupata tafsiri ya kikatiba juu ya suala hilo. Atabezwa lakini atabaki na hoja yake.
Ni kweli viongozi wanaoikanyaga katiba hawastahili na hawakustahili kuwa viongozi maana wanatoa mfano mbaya kwa wafuasi wao au watu wanaowaamini. Spika anapaswa, kama mkuu wa muhimili wa dola, kuwa mstari wa mbele kuifuata katiba na sheria zingine za nchi. Sijui kama alifanya makusudi kutofuata utaratibu ambao katiba imeweka au amezoea kutoifuata au ameona kwa vile kulikuwa na mgogoro wa wale wabunge 19 sasa akifuata katiba watu watamkosoa au alilenga nini hasa, sijui. Na ni miongoni mwa wale wenye kinga (kwa mujibu wa ile sheria iliyotungwa 'fastafasta'). It's a pity!
 
Katika hili, mimi naona kama Mh. Mbatia amekosea focus, kama kweli nia yake ni hiyo. Yeye alitakiwa akafungue kesi ya kuzuia mchakato wa kumpata spika mpya, kama anaona yule wa zamani hajajiuzulu, na si kwenda kumtaka aliyejiuzuru ajiuuzulu kisahihi; akigoma je? Huyu mtu ameshaachia ngazi na hiyo post haihitaji, kama amekosea utaratibu wa kujiuzulu basi anaweza akaamua atakavyo.

Iwapo Mbatia angefungua kesi ya kuzuia mchakato wa kumpata spika mpya, mamlaka husika zingemgeukia yule aliyejiuzulu na kumtaka ajiuzulu kulingana na utaratibu. Mh. Mbatia hana mamlaka yoyote kisheria ya kumlazimisha Mh. Ndugai ajiuzulu kwa kufuata Katiba. Unless kama anatarjia hukumu ya Mahakama ya kumlazimisha Mh. Ndugai ajiuzulu kwa kufuata utaratibu, asuming kweli utaratibu haukufuatawa
Mkuu, Mbatia analenga kupata tafsiri ya kikatiba kutoka mahakamani kuhusu uhalali wa Spika kujiuzulu. Hivyobasi, mchakato wa kumpata mwingine waweza kusimamishwa.
 
Kuna post iko humu kuna jamaa hadi ameweka kifungu cha Katiba. ambacho kinawahusu Spika au Naibu Spika wanapojiuzulu; wanatakiwa KUTOA TAARIFA BUNGENI, kitu ambacho Ndugai amefanya. Mh. Mbatia yeye anataka Mh. Ndugai amwandikie barua ya kujiuzulu, KATIBU WA BUNGE, kifungu ambacho kwenye Katiba hakipo. Kwa hiyo kama Katiba inasema kuwa Mh. Ndugai anatakiwa kutoa taarifa bungeni, hata PRESS RELEASE tu kwenye mojawapo ya notisi boad za ukumbi wa bunge ilikuwa inatosha
 
Suppose speaker akufuata katiba kwenye kujiudhuru. What outcome is Mbatia seeking iwapo Ndugai hana interest ya kuwa speaker tena?

Anataka Ndugai aandike barua kwa taratibu sahihi? and then what?

The only logical explanation of going through all this trouble iwapo Ndugai angekuwa interested.

Otherwise maamuzi yoyote ya mahakama speaker atakuwa Dr Tulia mwisho wa siku I do not see CCM kurudia mchakato wa kupendekeza jina la speaker, hakuna mtu atafukuzwa kazi, hakuna sheria itabadilishwa, and so forth it changes nothing in the end. Zaidi ya speaker kujiudhuru kama wanavyotaka.

Now that is a waste of court time and resources kusikiliza case kama hizo.
Tulia akichaguliwa tu, kesi nyingine itafunguliwa kwa yeye kugombea nafasi ya spika, akiwa naibu speaker.
 
Naona mnanichanganya mr wenu hapa
040603b97c1e80663c631d14469975b5.jpg
 
Mwenyekiti wa Taifa wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia ametinga Mahakama Kuu ya Tanzania na ameshafungua kesi ya kikatiba kuhusu kujiuzulu kwa Spika Job Yustino Ndugai. Kwa taarifa nilizonazo binafsi, tayari kesi husika imeshasajiliwa na imepangiwa jopo la Majaji watatu la kuisikiliza kesi hiyo. Wakati kesi hiyo ikiwepo mahakamani, tayari CCM na ADC wameshawapitisha wagombea wao wa nafasi ya Spika wa Bunge.
Athumani. Kimsingi, Mbatia ana haki na hoja za kufungua shauri lake Mahakama Kuu ya Tanzania kupata tafsiri ya kikatiba juu ya suala hilo. Atabezwa lakini atabaki na hoja yake.
Mama Tanzania anajisumbua tu haya mafisi yakitaka jambo linatimia hata huko alikoenda yapo.
 
Rais kushinikiza spika kujiuzulu yenyewe tu inavunja katiba, kwani inaondoa dhana nzima ya kujitegemea kwa mihimili kiutendaji ili kuleta checks and balance.............the only way forward ni rais kuvunja bunge nchi irudi kwenye uchaguzi.
 
Mbatia yuko sawa na hapa ndipo tutaona kama majaji wanasimama kwenye nafasi yao bila woga. Tunajua jinsi viongozi wanaweza kupuuza katiba. Mzee ruksa enzi zake badala ya kuangalia katiba aliruhusu znz kuingia oic. Juzi hapa tumeona samia kinyume na kiapo cha urais anaruhusu vigogo kula hela ya umma kwa kiasi mradi wasivimbiwe.
Hili la spika limeelekezwa kwenye katiba akijiuzulu anajiuzulu kwa nani.
Wengi tulistaajabu kuona spika mtumishi wa serikali anapeleka barua kujiuzulu kwa katibu wa chama chake. Kuweka nakala kwa katibu wa bunge haimanishe ameandika barua kwake.
Kama nikuheshimu utawala wa sheria kiti cha spika hakiko wazi kwa sababu ndugai bado hajajiuzulu.
Maraisi waliokosea na kuvunja katiba ni waislamu tuu!?
 
Back
Top Bottom