Benjamini Netanyahu
JF-Expert Member
- Aug 7, 2014
- 95,871
- 116,627
Kweli tupuRais kushinikiza spika kujiuzulu yenyewe tu inavunja katiba, kwani inaondoa dhana nzima ya kujitegemea kwa mihimili kiutendaji ili kuleta checks and balance.............the only way forward ni rais kuvunja bunge nchi irudi kwenye uchaguzi.
Halafu walishika vitabu vya Mungu kuapa.Inakera kuona katiba inaminywa na hawahawa tuliowapa ridhaa kuilinda katiba!
Basi tuachane na katiba na sheria tuendeshe nchi kwa mapenzi ya kila mtu na logic.Labda tusaidie what outcome from the will please Mbatia? And what will change given the circumstances kuzuia Dr Tulia kuwa speaker.
Hapa ndipo nilipokuwa nampendea Magufuli ujinga ujinga kama huu alikuwa aupi nafasi kabisa zaidi ya kucheleweshana kwenye kazi tu kwa tafsiri yake.
Mwenyekiti wa Taifa wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia ametinga Mahakama Kuu ya Tanzania na ameshafungua kesi ya kikatiba kuhusu kujiuzulu kwa Spika Job Yustino Ndugai. Kwa taarifa nilizonazo binafsi, tayari kesi husika imeshasajiliwa na imepangiwa jopo la Majaji watatu la kuisikiliza kesi hiyo. Wakati kesi hiyo ikiwepo mahakamani, tayari CCM na ADC wameshawapitisha wagombea wao wa nafasi ya Spika wa Bunge.
Nimekuwa nikifuatilia maoni ya watanzania na wasio watanzania kwenye mitandao ya kijamii, mitaani, runingani na redioni kuhusu kesi iliyofunguliwa na Mbatia. Wengine wanamuona Mbatia akitaka Ndugai abaki kuwa Spika wa Bunge kwa njia ya Mahakama. Wapo wanaomuona Mbatia kama anayepoteza muda na 'fedha' zake kwa jambo lisilo na maana na kuwa jambo hilo limeshapitwa na wakati. Wapo wanaompongeza. Lakini, wengi wanambeza.
Suala la utetezi wa Katiba ni suala kubwa na la muhimu kwa kila mmoja wetu. Kila Mtanzania, kwakuwa Katiba ni sheria yetu mama, anapaswa kuilinda na kuitetea katiba yetu. Katiba inapotoa masharti ya kufuatwa, lazima yafuatwe. Katiba imetoa masharti ya kufuatwa na Spika anayetaka kujiuzulu. Ni lazima yafuatwe. Mbatia ameona hayakufuatwa. Amekwenda mahakamani kuitetea na kuilinda Katiba yetu iliyotoa masharti ambayo ameona yamekiukwa. Ni haki yake na anafanya jambo jema.
Viongozi wetu, wanapoapishwa, huapa kuilinda na kuitetea Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Sheria zote nyinginezo (zinazotungwa na Bunge na zile Ndogondogo) hazipaswi kukinzana na Katiba. Pale zinapokuwa kimya, Katiba hutumika. Haipendezi kushabikia viongozi ambao hawaifuati Katiba yetu kwa minajili ya kuilinda na kuitetea kama walivyoapa. Tena, viongozi wenyewe ni wale wanaotokea kwenye Bunge ambalo ndilo linalotunga sheria.
Si sawa Athumani, aliyedhaminiwa na Musa kupata kazi kwa Ally, kuandika barua yake ya kuacha kazi akiielekeza kwa Musa huku akitoa nakala tu kwa Ally-mwajiri wake. Hapo, aliyepaswa kuandikiwa barua husika ni mwajiri ambaye ni Ally na nakala inaweza kuelekezwa kwa Musa ikimpendeza Athumani. Kimsingi, Mbatia ana haki na hoja za kufungua shauri lake Mahakama Kuu ya Tanzania kupata tafsiri ya kikatiba juu ya suala hilo. Atabezwa lakini atabaki na hoja yake.
Ndugai hawezi kulazimishwa kuwa Spika na mchakato wa CCM wa kumpata mgombea uspika siyo suala la kikatiba au sheria za nchi. Kitendo cha Ndugai kuondoka kienyeji bila kufuata katiba na sheria za nchi kunaweza kutafsiriwa kama ame-abscond na hivyo kuchukuliwa hatua za kisheria ikiwa na pamoja na kufukuzwa kazi na kukosa stahiki zake zote za uspika!Katika hayo maelekezo yao awawezi mlazimisha Ndugai kuwa speaker tena kama ataki. If anything ataandika hiyo barua wanavyotaka kama hakuna manufactured copy to date huko bungeni.
Na awawezi lazimisha CCM kurudia mchakato wao wa kupendekeza jina la speaker kwa sababu it internal process.
So regardless of the court decision in the end the whole thing is waste of time.
Viongozi wetu wameapa kuilinda katiba ya nchi na si vinginevyo, akikiuka Katiba anakuwa mhaini na anaweza kushtakiwa na kuhukumiwa kwa mujibu wa sheria.Katika hili, mimi naona kama Mh. Mbatia amekosea focus, kama kweli nia yake ni hiyo. Yeye alitakiwa akafungue kesi ya kuzuia mchakato wa kumpata spika mpya, kama anaona yule wa zamani hajajiuzulu, na si kwenda kumtaka aliyejiuzuru ajiuuzulu kisahihi; akigoma je? Huyu mtu ameshaachia ngazi na hiyo post haihitaji, kama amekosea utaratibu wa kujiuzulu basi anaweza akaamua atakavyo.
Iwapo Mbatia angefungua kesi ya kuzuia mchakato wa kumpata spika mpya, mamlaka husika zingemgeukia yule aliyejiuzulu na kumtaka ajiuzulu kulingana na utaratibu. Mh. Mbatia hana mamlaka yoyote kisheria ya kumlazimisha Mh. Ndugai ajiuzulu kwa kufuata Katiba. Unless kama anatarjia hukumu ya Mahakama ya kumlazimisha Mh. Ndugai ajiuzulu kwa kufuata utaratibu, asuming kweli utaratibu haukufuatawa
Hakuna katiba iliyokiukwa,nikikuuliza wewe hebu nipe kifungu cha katibu kilichokiukwa hukijuiSuala hapa halimhusu Ndugai. Hapa tunazungumzia utamaduni wa kufuata sheria kuu- Katiba.
Hata ungukuwanwewe ndio umekiuka tungeenda mahakamani.
amechukua fomu ya kugombea u-spika?Katiba inasemaje kuhusu yeye kugombea akiwa ndiye naibu spika ambaye kwa sasa ndiye Spika wa mpito??
Ndo wasomi wa Tanzania mlivyowajinga.awe/asiwe spika tulia,lkn katiba ifuatwe.ndo logic ya ya mtoa madaSuppose speaker akufuata katiba kwenye kujiudhuru. What outcome is Mbatia seeking iwapo Ndugai hana interest ya kuwa speaker tena?
Anataka Ndugai aandike barua kwa taratibu sahihi? and then what?
The only logical explanation of going through all this trouble iwapo Ndugai angekuwa interested.
Otherwise maamuzi yoyote ya mahakama speaker atakuwa Dr Tulia mwisho wa siku I do not see CCM kurudia mchakato wa kupendekeza jina la speaker, hakuna mtu atafukuzwa kazi, hakuna sheria itabadilishwa, and so forth it changes nothing in the end. Zaidi ya speaker kujiudhuru kama wanavyotaka.
Now that is a waste of court time and resources kusikiliza case kama hizo.
Ungejitahidi kusoma hoja iliyoenda mahakamani kuliko kuwa na tabia ya kukurupuka kama uharo ndugu.Ni mwehu tu ndio atambeza Mbatia
Interest anayo ndio maana aliomba msamaha Ila vishoka wakaibuka kumshambulià.Suppose speaker akufuata katiba kwenye kujiudhuru. What outcome is Mbatia seeking iwapo Ndugai hana interest ya kuwa speaker tena?
Anataka Ndugai aandike barua kwa taratibu sahihi? and then what?
The only logical explanation of going through all this trouble iwapo Ndugai angekuwa interested.
Otherwise maamuzi yoyote ya mahakama speaker atakuwa Dr Tulia mwisho wa siku I do not see CCM kurudia mchakato wa kupendekeza jina la speaker, hakuna mtu atafukuzwa kazi, hakuna sheria itabadilishwa, and so forth it changes nothing in the end. Zaidi ya speaker kujiudhuru kama wanavyotaka.
Now that is a waste of court time and resources kusikiliza case kama hizo.
Tena mwenye Akili hiziView attachment 2094840