Mchochezi
JF-Expert Member
- Feb 29, 2012
- 10,962
- 7,830
Habari za muda huu wana JF, Naomba tupeane habari kuhusu baadhi ya kesi maarufu zilizowahi kutokea ndani ya Tanzania ambazo kwa kiasi fulani zilitikisa na sasa zinatumika katika maamuzi ya kesi nchini.
Mfano:
Saidi Mwamwindi vs Republic (1972) HCD, Ambayo mkulima Saidi Mwamwindi alimuua mkuu wa mkoa Iringa Dr. Kleruu na kuhukumiwa kifo.
Bi Hawa Mohamed Vs Ally Sefu [1983] TLR 32,
Ni hukumu muhimu na maarufu kuliko zote pale linapokuja suala la migogoro ya wana-ndoa wanaotaka kutalikiana na pia suala zima la ugawanaji mali pale mahakama inaporidha talaka itolewe na ndoa hiyo ihesabike kwamba imeshindwa kuhimi mikikimikiki ya kutoelewana. nazungumzia hapo tamu inayogeuka kuwa shubiri baadaye.
Hukumu huu ilitolewa mwaka 1983 na Jopo la Majaji Watatu wa Mahakama ya Rufaa Tanzania (Jaji Mkuu Nyalali, kama alivyokuwa wakati ule, Jaji Lewis Makame na Jaji Robert Kisanga). Mengi yalizungumzwa humo na kinachoskikitisha hata baadhi ya wanasheria wameilewa vibaya hukumu hii kwa kutoisoma kwa umakini neno kwa neno, aya kwa aya. Inatosha tu kusema kuwa kikubwa kilichoelekezwa hapo ni kwamba mama wa nyumbani anastahili kupata mgawo katika mali iliyochumwa na wanandoa hata kama kazi alizofanya ni za nyumbani tu na mumewe haijalishi alikuwa akikesha akirusha ndege, katika vikao vya mawaziri, kwenye dili kubwa ama safari za ki-biashara ana kazi nyinginezo, iweza kitaalam ama za suluba. Nikumbushe tena, jambo hili lisieleweke kijumla jumla tu hivyo, mahakama ilitoa ufafanuzi zaidi katika hili na sitaweza kutazungumza yote hapa.
Kesi hii ni muhimu kwa vile Mahakama hii ikiwa ni ya Juu zaidi Kikatiba na ambayo hukumu zake zapaswa kufuatwa na mahakame zote chini yake (katika tafsiri ya sheria husika). Ndiyo kusema,Jaji wa Mahakama Kuu, Hakimu wa Mahakama ya Wilaya au Ilala na wengineo wanatarajiwa kuzingatia msingi uliwekwa hapo.
Wakuu naomba tuongeze nyingine.