Kesi namba 456 ya 2016 JamiiForums vs Jamhuri, Kisutu: Maxence Melo ahukumiwa Mwaka jela au faini ya Tsh. Mil 3. Mwenzake aachiwa huru

Kesi namba 456 ya 2016 JamiiForums vs Jamhuri, Kisutu: Maxence Melo ahukumiwa Mwaka jela au faini ya Tsh. Mil 3. Mwenzake aachiwa huru

Not really ! It shows how people are coward, selfish, unconfident and insecure of themselves!
right minded people don’t care how people define them and treat them!
our county is full of hypocrites, untrusted, coward , selfish individuals no matter their status and position. The country is full of weird people!
Mfano wewe ni bosi wangu na kuna ufisadi unaufanya nataka niwe whistle Blower nifanyaje ili usinitambue kama ni mie

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni habari njema Kwetu Wadau kama Kesi hii imeisha salama na Faini imeshalipwa kwani ilikuwa inatuweka roho juu juu na angalau sasa wengine tunaweza hata Kuagiza ' Kichuri ' na Kukilia kwa Ugali wa Udaga na Ulezi kwa amani kabisa huku tukiamini kwamba Mtandao Wetu huu ambao kwa Sisi wengine akina GENTAMYCINE ndiyo Kilevi chetu Kikubwa na Starehe yetu iliyotukuka.

Poleni sana Uongozi mzima wa Jamii Media Company kwa Changamoto zote za hii Kesi na poleni hasa Wadau Wakuu Maxence Melo na Mike Mushi ila Washukuriwe mno wale Wadau wote ambao muda mwingi walikuwa wakiipambania JamiiForums kwa namna moja au nyingine juu ya hii Kesi yao hadi leo hii imemalizika rasmi.

Mwenyezi Mungu awatie nguvu, Maisha yaendelee na JamiiForums izidi Kuchanja Mbuga katika Mapambano ya Uhuru wa Habari.
Kesi imeisha mkuu ila implication yake ndio mbaya kwetu JF.

Max kahukumiwa kwa kosa la kuzuia polisi kufanya kazi yao (kuficha taarifa za mteja wa JF). Kwa hiyo kwakuwa kashindwa ina maana inabidi awe anatoa taarifa za wateja coz kuzificha ni kosa kama ilivyoamuliwa leo.

Ni kama mwenye nyumba kuzuia polisi kumchukua mpangaji wake. Polisi wakimshtaki mwenye nyumba then akashindwa basi kesho wakija tena kumchukua mpangaji inabidi asizuie.
 
GENTAMYCINE,
Kesi imeisha mkuu ila implication yake ndio mbaya kwetu JF.

Max kahukumiwa kwa kosa la kuzuia polisi kufanya kazi yao (kuficha taarifa za mteja wa JF).

Kwa hiyo kwakuwa kashindwa ina maana inabidi awe anatoa taarifa za wateja coz kuzificha ni kosa kama ilivyoamuliwa leo.
Wawaache watu wateme nyongo kwa uhuru bhana
 
Watoa taarifa za ufisadi ndio wanapigwa faini haya sawa kila lenye mwanzo lina mwisho...
 
Kesi imeisha mkuu ila implication yake ndio mbaya kwetu JF.

Max kahukumiwa kwa kosa la kuzuia polisi kufanya kazi yao (kuficha taarifa za mteja wa JF). Kwa hiyo kwakuwa kashindwa ina maana inabidi awe anatoa taarifa za wateja coz kuzificha ni kosa kama ilivyoamuliwa leo.

Ni kama mwenye nyumba kuzuia polisi kumchukua mpangaji wake. Polisi wakimshtaki mwenye nyumba then akashindwa basi kesho wakija tena kumchukua mpangaji inabidi usizuie.
Sasa inakuwaje? Kama Hana uwezo wakuzipata?
 
Mkuu asante sana kwa huu Ufafanuzi wako ulioenda Shule ( Kidato ) ambao kwa ' Upopoma ' wangu nilishindwa Kuung'amua.Hata hivyo ngoja tusubiri Maelezo kamili juu ya hii Hoja yako nzito na iliyoshiba kutoka Kwake Mwanzilishi Maxence Melo au hata Uongozi wa huu Mtandao wetu pendwa wa JamiiForums. Umeifafanua katika hali ya Kufikirisha kabisa Mkuu na kuna ' angle ' fulani fulani ukiiangalia unaweza kudhani hivyo ulivyosema.
 
Hata mimi sio mwanasheria pia. Hii ilikuwa ni kesi namba 456 ya 2006, Jamhuri dhidi ya mkurugenzi wa Jf. Kama itatokea a post nyingine kabisa ambayo haiusiani na uzi uliosababisha kesi hii ikiwa polisi wanamhitaji mtoa mada(uzi) watafungua kesi nyingine tofauti na hii. Kama wakitaa kutoa ip address watag'g'ania kifungu kile kile cha 22(1) cha Cyber crimes Act,ambacho ni Obstruction to investigation.
Rufaa ni haki yao wanaweza kukatia na hapo itakuwa High Court. Na naendelelea kukumbusha precedence ni hukumu za High cout na Court of Appeal hizi ndio superior
Icourt of records hapa Tz.
Kuhusu Id ni gunuine kabisa.
Hivi JF walikataa kutoa details au walisema hawana uwezo wa kutoa details za wenye post?
 
ila Maxence strong sana,umepigana kiume kweli, mie ningeshatoa vijina vyenu zamaaaaaaaaaaaaaani 🤣 🤣 🤣 🤣
 
Kesi imeisha mkuu ila implication yake ndio mbaya kwetu JF.

Max kahukumiwa kwa kosa la kuzuia polisi kufanya kazi yao (kuficha taarifa za mteja wa JF). Kwa hiyo kwakuwa kashindwa ina maana inabidi awe anatoa taarifa za wateja coz kuzificha ni kosa kama ilivyoamuliwa leo.

Ni kama mwenye nyumba kuzuia polisi kumchukua mpangaji wake. Polisi wakimshtaki mwenye nyumba then akashindwa basi kesho wakija tena kumchukua mpangaji inabidi usizuie.
Dah!.. hii ni hatari sana huko mbeleni.
 
Hivi JF walikataa kutoa details au walisema hawana uwezo wa kutoa details za wenye post?
Mbona unaniuliza maswali ya kizushi? Mimi sina nakala ya hukumu. Subiri tuipate. Ila nilisoma kwenye gazeti moja ishu ilikuwa ni ip adress ya mtoa mada. Sasa sina uhakika kama Jf walikataa kutoa au vipi.Na wala sina uhakika kama walikuwa nayo au vipi.
 
Hapo Zaman kidogo JF palikuwa mahala pazuri sana kwa kutoa mawazo huru ya aina yoyote lakini Sasa kuna hii limetwa la kuingilia shughuli za serikali ama kupotosha umma ama kuchochea upotevu wa amani, tujifunze kusoma alama za nyakati tujue ni Kipindi gani Tupo na changamoto tulizo nazo kisiasa ili tusijingize matatizoni.

sisemi kuwa wanaharakati waache kupambana ila tu wawe tayari kwa lolote watazame vizuri ni nani wanamuona adui wa maendeleo na wanamkabili kwa namna gani.

hiki ni kipindi cha kuwa makini na muangalifu wakati unatoa maoni kuhusu chochote hasa pale maoni yanapoihusu serikali moja kwa moja.
IKiwa watu ambao wanaikosoa serikali Bungeni wanawekewa kila aina ya vizuizi, na ikiwa serikali imefunga uwanja wa wana siasa kuikosoa serikali kwnye mikutano ya siasa, na ikiwa magazeti yakiandika habari za kuikosa serikali yanafungiwa, ni wapi pengine Watanzania wanaweza kuikosoa serikali yao?

CAG alikosoa serikali ikawa shida, sembuse mimi na wewe? Tutapata wapi uwanja wa kumkosoa Magufuli na serikali yake kama sio JF?

KUmbuka kwamba serikali haipo pale kwa ajili ya mambo yao wenyewe, ipo pale kwa ajili ya wananchi. Kwa hiyo inapaswa kuruhusu wananchi waikosoe kwa uhuru kama kulingana na mtazamo wao,
 
Back
Top Bottom