Kesi namba 456 ya 2016 JamiiForums vs Jamhuri, Kisutu: Maxence Melo ahukumiwa Mwaka jela au faini ya Tsh. Mil 3. Mwenzake aachiwa huru

Mfano wewe ni bosi wangu na kuna ufisadi unaufanya nataka niwe whistle Blower nifanyaje ili usinitambue kama ni mie

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aidha Mike Mushi amekutwa hana hatia na kuwa aliungwa kwenye kesi kimakosa

DAH!
 
Kesi imeisha mkuu ila implication yake ndio mbaya kwetu JF.

Max kahukumiwa kwa kosa la kuzuia polisi kufanya kazi yao (kuficha taarifa za mteja wa JF). Kwa hiyo kwakuwa kashindwa ina maana inabidi awe anatoa taarifa za wateja coz kuzificha ni kosa kama ilivyoamuliwa leo.

Ni kama mwenye nyumba kuzuia polisi kumchukua mpangaji wake. Polisi wakimshtaki mwenye nyumba then akashindwa basi kesho wakija tena kumchukua mpangaji inabidi asizuie.
 
Wawaache watu wateme nyongo kwa uhuru bhana
 
Watoa taarifa za ufisadi ndio wanapigwa faini haya sawa kila lenye mwanzo lina mwisho...
 
Sasa inakuwaje? Kama Hana uwezo wakuzipata?
 

Mkuu asante sana kwa huu Ufafanuzi wako ulioenda Shule ( Kidato ) ambao kwa ' Upopoma ' wangu nilishindwa Kuung'amua.Hata hivyo ngoja tusubiri Maelezo kamili juu ya hii Hoja yako nzito na iliyoshiba kutoka Kwake Mwanzilishi Maxence Melo au hata Uongozi wa huu Mtandao wetu pendwa wa JamiiForums. Umeifafanua katika hali ya Kufikirisha kabisa Mkuu na kuna ' angle ' fulani fulani ukiiangalia unaweza kudhani hivyo ulivyosema.
 
Hivi JF walikataa kutoa details au walisema hawana uwezo wa kutoa details za wenye post?
 
ila Maxence strong sana,umepigana kiume kweli, mie ningeshatoa vijina vyenu zamaaaaaaaaaaaaaani 🤣 🤣 🤣 🤣
 
Dah!.. hii ni hatari sana huko mbeleni.
 
Hivi JF walikataa kutoa details au walisema hawana uwezo wa kutoa details za wenye post?
Mbona unaniuliza maswali ya kizushi? Mimi sina nakala ya hukumu. Subiri tuipate. Ila nilisoma kwenye gazeti moja ishu ilikuwa ni ip adress ya mtoa mada. Sasa sina uhakika kama Jf walikataa kutoa au vipi.Na wala sina uhakika kama walikuwa nayo au vipi.
 
IKiwa watu ambao wanaikosoa serikali Bungeni wanawekewa kila aina ya vizuizi, na ikiwa serikali imefunga uwanja wa wana siasa kuikosoa serikali kwnye mikutano ya siasa, na ikiwa magazeti yakiandika habari za kuikosa serikali yanafungiwa, ni wapi pengine Watanzania wanaweza kuikosoa serikali yao?

CAG alikosoa serikali ikawa shida, sembuse mimi na wewe? Tutapata wapi uwanja wa kumkosoa Magufuli na serikali yake kama sio JF?

KUmbuka kwamba serikali haipo pale kwa ajili ya mambo yao wenyewe, ipo pale kwa ajili ya wananchi. Kwa hiyo inapaswa kuruhusu wananchi waikosoe kwa uhuru kama kulingana na mtazamo wao,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…