Kesi ya Abdallah Zombe: Mashitaka, hatia, hukumu na yanayojiri

Kwa bahati mbaya mi si mwanasheria wala si mwandishi wa habari. Najiuliza Nikitarajia jibu lenu wanajamii. Hivi ile tume ya rais chini ya jaji Kipenka ilimdananya rais? Manake nahisi waandishi wetu inawezekana walimhukumu Zombe na wenzake kwa kuwa tayari Tume ya jaji Kipenka ilishawahukumu kiaina. Kipenka ni Jaji, na Masati ni Jaji. Jaji na Jaji wanapotofautiana, kwanini waandishi wetu wasikengeuke? Tusiwalaumu bure waandishi wetu! Natoa hoja!

Ndugu Chrispin samahani ( kwa nia nzuri) kama unaweza kusoma kiingereza ebu nunua The Citizen ya leo usome. Nimesoma magazeti karibu yote ya kiswahili lakini sijaona gazeti ambalo limetoa "summary' nzuri ya Kesi ya kina Zombe kama The Citizen. Kimsingi Tume ya Judge Kipenga haikuwa mahakama. Tume ilikuwa na wajibu wa kuchunguza kama kina Chighumbi wamekufa wakati wakipambana na Polisi au wameuawawa katika mazingira tatanishi. Tume ya Kipenka ikachunguza na kugundua kwamba Chugumbi na wenzake wameuwawa wakiwa mikononi mwa polisi. Hata katika hukumu yake Judge Masati anasema hawa marehemu waliuawa huko katika mstitu wa Pande na imebainika kwamba Bwana Mageni (mshitakiwa wa pili) alikuwepo na alishuhudia mauaji hayo ila Serikali imeshindwa kudhibitisha kwamba ni yeye aliyewaua au kuamuru wauwawe. Kimsingi kina Zombe na wengine wameachiliwa kutokana na ushahidi dhaifu ukiyowekwa mbele ya mahakama na si vinginevyo. Tume ya Judge Kipenka haikumdanganya Rais. Ilifanya kazi yake kama hadidu za rejea zilivyosema. Polisi na upelelezi dhaifu umepelekea Zombe na wenzake kupeta katika kesi ambayo inagusa hisia ya watu wengi.
 
lazima tukubali kuwa KALAMU YA MWANDISHI INA ATHALI KUBWA KATIKA JAMII. INAWEZA KUFANYA UPENDE KITU BILA KUJUA UBAYA WAKE AU HATA KUSABABISHA VITA KATIKA JAMII BILA KUJUA MNAGOMBEA NINI.

SASA LAZIMA JAMII IAMUE YENYEWE NA ISITUMIE MATAKWA YA WAANDISHI.
 
Hakika kila siku nimekuwa nasema kazi yetu sisi waandishi ni KUELIMISHA, KUIPASHA JAMII NA KUIBURUDISHA JAMII. Na wala hatutakiwi kabisa kuiamulia jamii ifate sisi kile tunachotaka.

Hakika mwandishi makini anatakiwa asiegemee upande wowote wa shilingi ili kutoa nafasi kwa wasomaji wawe huru kuamua. Na unapokuja kwenye issue yoyote aliyokuwepo kwene vombo vya sheria kama mahakama, waandishi wanatakiwa waandike kile tu kinachozungumzwa na hawapaswi hata kidogo kuongeza au kupunguza kitu. Hicho ingawa ni kinyume cha maadili ya kiuandishi vile vile ni kinyume cha Sheria za nchi za mwenendo wa mahakama.

Nikirudi kwenye kesi ya ZOMBE. Hakika waandishi karibu wa magazeti yote huko Tanzania walisha amua kumtia Zombe hatiani na kuionyesha jamii kuwa yeye ni muuaji na walisahau kabisa kuwa kuna taratibu za kimahakama na kisheria za kuthibitisha tendo zima.

Hakika hivi sasa bila shaka huko Tanzania wengi watalalama kuona kuwa jaji Masati amekosea au amependelea. Hiyo yote inatokana na vyombo vya habari kumuhuku,u Zombe kwa jamii kuwa yeye muuwaji.

Hakika ningependa kusema kuwa vyombo vya habari hususan magazeti YAMEUMBUKA KWENYE KESI YA ZOMBE. HII YOTE INATOKANA WENGI WA WAHARIRI KUTOKUWA NA TAALUMA SAHIHI YA HABARI AU KUTAWALIWA NA TAMAA YA FEDHA NA KUSHABIKIA UPANDE MMOJA BILA KUJUA SHERIA INAPIMA USHAHIDI WA PANDE ZOTE NA KUTOA HUKUMU.

Ingawa upande wa Serikali una nafasi ya kukata Rufaa, lakini nae zombe ana nafasi kubwa sana kuyashitaki magazeti yote yaliyokuwa yanaandika upendeleo katika kesi yake ikiwa pamoja na kuita kesi ya Zombe na wenzake badala ya kuita kesi ya watuhumiwa wa mauaji ya wafanabiashara wa morogoro.

HAKIKA WAANDISHI UCHWARA WA TANZANIA MTAIPELEKA PABAYA NCHI. SASA MMESHA MJENGEA ZOMBE NA WENZAKE MAADUI KATIKA JAMII.

Nasriyah Saleh Al-Nahdi.
Doha.
Qatar

Kuita kesi ya zombe ni selling point mkuu!
 
lazima tukubali kuwa KALAMU YA MWANDISHI INA ATHALI KUBWA KATIKA JAMII. INAWEZA KUFANYA UPENDE KITU BILA KUJUA UBAYA WAKE AU HATA KUSABABISHA VITA KATIKA JAMII BILA KUJUA MNAGOMBEA NINI.

SASA LAZIMA JAMII IAMUE YENYEWE NA ISITUMIE MATAKWA YA WAANDISHI.

Wewe kitu unacho shindwa kutofautisha ni "nini kinachotakiwa kuandikwa kutoka mahakamani". Mwandishi wa habari anaporuhusiwa kuingia ktk mahakama inamaana kesi husika siyo siri na anaruhusiwa kuandika yote kutokana na jinsi mahojiano yanavyo endeshwa. Na hili ndivyo magazeti yalivyokuwa yakiwasilisha ktk magazeti yao, sasa wewe unasema wameumbuka kwani waandishi ndo walimshitaki zombe??

Wewe ungetaka kujenga hoja yako hapa labda ungesema serikali pamoja na tume ya jaji kipenka ndo wameumbuka lakini siyo waandishi wa habari. Na unasahau kwamba magazeti yao lazima yauzike kutokana na incidences mabli mbali zinazotokea ktk jamii.

Hapo juu unasema jamii iamua yenyewe na siyo kutumia matakwa ya mwandishi? kwa mawazo yako unadhani jamii ianue nini? Kumfunga zombe au? Hii kesi aliyeshitaki ni Jamuhuri na siyo mtu mwingine, sasa jamii iamue kwa lipi??

Acha kukurupuka ndugu!!! jenga hoja ambazo unaweza kuzitetea!!!!!
 
Ndugu Chrispin samahani ( kwa nia nzuri) kama unaweza kusoma kiingereza ebu nunua The Citizen ya leo usome. Nimesoma magazeti karibu yote ya kiswahili lakini sijaona gazeti ambalo limetoa "summary' nzuri ya Kesi ya kina Zombe kama The Citizen. Kimsingi Tume ya Judge Kipenga haikuwa mahakama. Tume ilikuwa na wajibu wa kuchunguza kama kina Chighumbi wamekufa wakati wakipambana na Polisi au wameuawawa katika mazingira tatanishi. Tume ya Kipenka ikachunguza na kugundua kwamba Chugumbi na wenzake wameuwawa wakiwa mikononi mwa polisi. Hata katika hukumu yake Judge Masati anasema hawa marehemu waliuawa huko katika mstitu wa Pande na imebainika kwamba Bwana Mageni (mshitakiwa wa pili) alikuwepo na alishuhudia mauaji hayo ila Serikali imeshindwa kudhibitisha kwamba ni yeye aliyewaua au kuamuru wauwawe. Kimsingi kina Zombe na wengine wameachiliwa kutokana na ushahidi dhaifu ukiyowekwa mbele ya mahakama na si vinginevyo. Tume ya Judge Kipenka haikumdanganya Rais. Ilifanya kazi yake kama hadidu za rejea zilivyosema. Polisi na upelelezi dhaifu umepelekea Zombe na wenzake kupeta katika kesi ambayo inagusa hisia ya watu wengi.

Ni jaji Kipenka na siyo kipenga, tafadhali rekebisha hii.
 
Kutokana na watu wengi kutoijua SHERIA wamesikitishwa na wengine kufurahi kuwa zombe kashinda kesi.

Kilichotokea hapa ni mfululizo wa wanasheria wa serikali ama kwa uzembe au kwa MAKUSUDI wanakosa umakini katika kufungua na kuendesha kesi.

Katika watu wote tisa hakuna aliyewaua wafanyanyabiashara moja kwa moja ISIP.OKUWA walishiriki kwa kuwasaidia wauaji ambao ama kwa njama au UZEMBE wa serikali walijifanya kutotambua umuhimu wao katika kesi hii.

MAHAKAMA imetoka hukumu kuwa huwezi kumtia hatiani mtu aliyesaidia kufanya makosa wakati mkosaji mwenyewe hujamleta mahakamani..........

kwa hiyo wajameni tumtrafute muuwaji ili ZOMBE na wenzake wawajibishwe.
HIZI SHERIA NAZO BWANA UOZO mtupu, kwanini tusiwe na first au second degree murder? hizi changamoto zinawafumbua sana MIMACHO hawa watu wabadirishe sheria ili JUSTICE ya UKWELI ipatikane angalau kwa kiasi kidogo hapa duniani.....
 
Wewe kitu unacho shindwa kutofautisha ni "nini kinachotakiwa kuandikwa kutoka mahakamani". Mwandishi wa habari anaporuhusiwa kuingia ktk mahakama inamaana kesi husika siyo siri na anaruhusiwa kuandika yote kutokana na jinsi mahojiano yanavyo endeshwa. Na hili ndivyo magazeti yalivyokuwa yakiwasilisha ktk magazeti yao, sasa wewe unasema wameumbuka kwani waandishi ndo walimshitaki zombe??
.

Magezi.

Usikurupuke ndugu yangu na kutaka kudandia treni kwa mbele.

hebu soma hoja zangu vizuri sana kisha lete hoja.
Elewa kuwa mwandishi anatakiwa aandike kile tu anachosikia na sio kuandika hisia zake. na kama utapata bahati ya kusoma mwenendo wa kesi utaona waandishi wengi huko walikuwa wanaandika kiushabiki na kufata hisia zao na sio hali halisi.

Na kama utafuatilia vizuri hata Zombe aliwahi kulisema hilo kupitia kwa wakili wake Late moses Maira ( siku walipokuwa wanatafsiri Amri na Amri halali). sasa tatizo la kuandika kiushabiki ndilo hilo sasa jamii ilimuona Zombe ni muuwaji kitu ambacho sheria haikuliona hilo.

kama utapata bahati ya kusoma hukumu utaona Kwa kosa ambalo Zombe na wenzake wameshitakiwa la mauaji wao hawana hatia kabisa . ila kuna makosa kisheria wanaweza kuhusika kama kushiriki katika kadhia nzima. lakini sio wajibu wa mahakama kuwatia hatiani kwa kosa ambalo hawakushitakiwa nalo.

sasa kwa msingi huo wa waandishi wa Tz walishamtumbukiza na kuifanya jamii iamini kuwa Zombe na wenzake wameua HAPO WAMEUMBULIWA NA SHERIA

sasa ndugu yangu soma hoja zangu vizuri kabla hajachangia.
 
Upande wa mashtaka kwenye kesi ya kina Zombe unakata rufaa kupinga uamuzi wa mahakama.

2009Serikali yapinga hukumu ya kuachiwa akina Zombe
broken-heart.jpg
Na Wandishi Wetu

SERIKALI imesema haijaridhika na hukumu iliyowaweka huru watuhumiwa kwenye kesi ya mauaji ya kukusudia ya wafanyabiashara watatu wa madini na dereva mmoja na imeamua kukata rufaa kupinga hukumu hiyo.

Katika hukumu iliyosomwa na Jaji Salum Massati juzi, haikuweza kuithibitishia mahakama kuwa watuhumiwa hao tisa, akiwemo mkuu wa zamani wa upelelezi mkoani Dar es Salaam, Abdallah Zombe, walishiriki katika mauaji hayo na kwamba waendesha mashtaka walishindwa kuwafikisha mahakamani wauaji na hivyo kuagiza wasakwe.

Kaimu Mkurugenzi wa Mashtaka, Mary Lyimo alisema katika taarifa yake jana kuwa, ofisi yake imeamua kukata rufaa kupinga hukumu hiyo ambayo pia imepokewa kwa hisia tofauti na wananchi.

"Katika uamuzi huo, Mahakama Kuu ya Tanzania, baada ya kuuchambua ushahidi uliotolewa na misimamo mbalimbali ya kisheria, iliona kuwa upande wa mashtaka (Jamhuri) ulikuwa umeshindwa kuthibitisha mashtaka yake dhidi ya washtakiwa pasipo kivuli cha mashaka kama inavyotakiwa katika mashauri ya jinai," inasema taarifa yake.

"Hivyo iliamua kuwaachia huru washtakiwa wote waliokuwepo. Uamuzi huo umepokewa kwa hisia tofauti na umma. Ofisi hii inapenda kuufahamisha umma na kuuhakikishia kuwa hatukuridhishwa na uamuzi huo; hivyo sasa tunaanza mchakato wa kukata rufaa kwa kutoa Taarifa ya Nia ya Kukata Rufaa."

Upande wa mashtaka ulionekana kuyumba wakati wa majumuisho yake wakati ulipomwomba jaji kuwatia hatiani watuhumiwa na kwamba kama aliyekuwa mshtakiwa asingepatikana na hatia ya kuua bila ya kukusudia, atiwe hatiani kwa kushiriki kosa baada ya kosa, ombi ambalo Jaji Massati alilikataa kwa maelezo kuwa halimo kwenye mashtaka.

Wakati serikali ikijipanga kukata rufaa, wanasheria mbalimbali wamekuwa na mitazamo tofauti juu ya hukumu hiyo, wakiwemo ambao walisema kutotiwa hatiani kwa washtakiwa hao, ambao wote walikuwa askari wa Jeshi la Polisi, kumetokana na uzembe wa serikali katika kufanya uchunguzi na kuandaa mashtaka.

Naye wakili wa kujitegemea na mtaalamu wa masuala ya sheria, Profesa Abdallah Safari amesema kushindwa kwa serikali katika kesi hiyo ni kashfa.

Profesa Safari aliiambia Mwananchi kuwa, kuachiwa huru kwa watuhumiwa hao kunaonyesha kuwa kulikuwa na mapungufu makubwa ya kisheria katika pande zote zilizohusika na kesi hiyo.

Profesa Safari alisema inawezewekana Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) wa wakati huo aliamua kufungua kesi hiyo kwa kuzingatia taarifa ya tume ya Jaji Musa Kipenka kutokana na joto la shinikizo la kisiasa kwa wakati huo.

“Unajua tume hii iliundwa na Rais Kikwete... inawezekana DPP aliamua kuichukua taarifa hiyo kama ilivyo na kufungua kesi bila kuangalia zaidi mbinu za kisheria, alisema Safari.

“Siku zote lazima ieleweke kuwa duniani kote kesi haiendeshwi kisiasa, bali inaendeshwa na ushahidi uliopo,” alisema Profesa Safari ambaye aliwahi kugombea uenyekiti wa chama cha kisiasa cha CUF.

Mwanasheria huyo alisema Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) ndiye aliyekuwa na wajibu wa kuwakamata wauaji na kuwasilisha faili lao kwa DPP.

“Sijaziona nyaraka kutoka kwa DCI kwenda kwa DPP, lakini nahisi upelelezi haukufanywa vizuri,” alisema Profesa Safari na kuongeza kuwa serikali haikupaswa kushindwa katika kesi hiyo kwa kuwa ilikuwa na kila kitu.

“Hii ni sawa na mpishi kuwa na kila kitu, lakini ameshindwa kupika chakula kizuri, hivyo kuna umuhimu serikali ikajiangalia vizuri katika hili.”

Aliitaka serikali kutokata rufaa kwa jazba na badala yake ijiridhishe na ikiwezekana ijaribu kuomba msaada kutoka kwa wanasheria wengine wa kijitegemea wenye uwezo wa kupambana na kesi za namna hiyo.

Msomi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk Kennedy Gaston alisema: “Zombe alisema kulikuwa na majibizano ya risasi; alikataza miili ya marehemu kuchunguzwa huku akitaka izikwe mapema. Haya yote ni makosa ambayo yangeweza kumtia hatiani. Si lazima kukimbilia kosa moja la mauaji.”

Msomi mwingine wa UDSM, Lucy Eusebio alisema: “Katika kesi ya mauaji kuna mambo mawili, kuachiwa huru au kunyongwa hadi kufa, na kuna kanuni ya sheria inayosema ni heri kuwaachia wahalifu 100 kuliko kumfunga mmoja asiye na hatia.

“Kwa maana hiyo katika kesi ya mauaji inatakiwa ushahidi ujitosheleze kwa asilimia 100. Hata kama kutakuwa na asilimia 99 ya ushaidi unaoonyesha kuwa mtuhumiwa aliua, hiyo asilimia moja iliyopungua itaifanya mahakama impendelee mtuhumiwa.”

Wakili wa kujitegemea Anney Semu, alisema Jaji Massati ametoa hukumu hiyo kwa haki kwa sababu amefuata sheria na taratibu za kimahakama.

"Ila waendesha mashtaka walishindwa kuendesha kesi hiyo inavyopaswa kutokana na kwamba walikuwa wakisukumwa na hisia za wananchi ya kwamba Zombe ndiye aliyeua," alisema Semu na kueleza udhaifu wao kuwa ni kushindwa kuwachambua washtakiwa na kuwahusisha ipasavyo na mauaji hayo.

"Walichochanganya ni kushindwa kufuatilia kosa lilikuwa linasemaje, badala yake wakafuata hisia zilizochochewa na wananchi kuwa Zombe ndiye aliyeua."

Naye Profesa Issa Shivji alisema, hukumu hiyo imetokana na jaji huyo kutumia ushahidi uliotolewa mahakamani hapo.

"Majaji kazi yao ni kusikiliza ushahidi wa pande zote unaotolewa. Ikiwa ushahidi huo utaletwa kinyume, hukumu yake inaweza kuwa tofauti na kosa lenyewe," alisema Profesa Shivji.

Aliongeza kuwa kutokana na hali hiyo waendesha mashtaka wanapaswa kuwa makini ili kutoa ushahidi ambao unaendana na kosa lenyewe.

Wakati huo huo, Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam limeanza kujipanga upya kumtafuta polisi alinayedaiwa kutekeleza mauaji hayo yaliyofanywa mwaka 2006, Koplo Saad Alawi, ambaye alitoroka muda mfupi baada ya mauaji hayo.

Kamanda wa Polisi wa Kanda ya Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova aliliambia gazeti hili jana kuwa, kazi ya kumtafuta mtuhumiwa huyo ilianza mara moja baada ya hukumu hiyo.

“Tumeanza mkakati wa kumtafuta mtuhumiwa huyo kama mahakama ilivyotuagiza. Tutajitahidi kumsaka mahali popote mpaka atakapopatikana,” alisema Kova, ambaye wakati wa mauaji hayo alikuwa kamanda wa polisi mkoani Mbeya.

“Tunaheshimu agizo la mahakama, ndiyo maana tunaahidi kumtafuta ndani na nje ya nchi. Licha ya kwamba mtuhumiwa alikuwa akitafutwa tangu awali, kwa agizo hili tunaongeza nguvu zaidi,” alisema Kova.

Kova alisema moja ya mbinu itakayotumia
kumsaka mtuhumiwa huyo ni kuiomba jamii ishiriki katika kutoa taarifa za mahali alipo.

“Sikiliza... jeshi hili halijawahi kushindwa kumnasa mtuhumiwa na wale wanaotafutwa muda mrefu ndiyo tunawapata kirahisi, hivyo nina hakika tutampata,” aliongeza.

Akizungumzia askari ambao walifukuzwa kazi na baadaye kushtakiwa kwa tuhuma za kuhusika kwenye mauaji hayo, Kamanda Kova alisema polisi inaandaa utaratibu maalumu utakaotangazwa na makao makuu hivi karibuni.

Habari zinasema kuwa baadhi ya watuhumiwa walioachiwa huru wakati kesi hiyo ikiendelea, walikuwa wakilipwa nusu mshahara na sasa wamerejeshwa kazini.
Habari hii imeandaliwa na Hussein Kauli, Fredy Azzah, Patricia Kimelemeta na Jackson Odoyo
 
PICHA - Zombe na Wenzake Waachiwa Huru Kesi ya Mauaji
2839946.jpg

Zombe alipokuwa akitoka mahakamani leo Monday, August 17, 2009 4:24 PM
Washtakiwa wote katika kesi ya mauaji ya kikatili iliyokuwa ikimkabili aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Dar es Salaam, Abdallah Zombe, na wenzake 9, iliyokuwa ikiendelea kwenye mahakama kuu ya Tanzania WAMEACHIWA HURU. Picha za Zombe akiachiwa huru mahakamani mwisho wa habari hii. Jaji Kiongozi, Salum Masati, wa Mahakama Kuu ya Tanzania akisoma hukumu leo iliyochukuwa masaa sita, amewaachia huru washtakiwa wote wa kesi hiyo ya mauaji.

Katika kesi hiyo, Zombe na wenzake walikuwa wakituhumiwa kuwaua wafanya biashara wa madini Ephraim Sabinus Chigumbi, Sabinus Chigumbi (Jongo), Mathias Lung’ombe na Juma Ndugu aliyekuwa dereva teksi na mkazi wa Manzese Dar es Salaam, Januari 14, mwaka 2006 katika msitu wa Pande, Mbezi Luisi wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Akisoma hukumu hiyo leo Jaji Masati alisema kuwa washtakiwa wote hawana hatia kwakuwa hakuna ushahidi wa moja kwa moja unaonesha kuwa watuhumiwa hao walihusika katika kufanya mauaji ya wafanyabiashara hao.

Jaji Masati amesema kuwa amekosa ushahidi wa kuwatia hatiani pamoja na kusikilizwa kwa mashahidi wote 37.

Katika kesi hiyo iliyosikilizwa zaidi ya miaka miwili, jumla ya mashahidi 37 walifika mahakamani katika siku tofauti tofauti kutoa ushahidi juu ya mauaji hayo.

Washtakiwa katika kesi hiyo walikuwa ni Abdallah Zombe ambaye alikuwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Dar es Salaam, Bageni, Makele, WP 4513 Jane, D1406 Mabula, D8289 Michael, D2300 Abeneth, B1321 Rashid, D4656 Rajab na D1367 Philipo.

Mshitakiwa Lema alifutiwa kesi baada ya kufariki dunia kutokana na kusumbuliwa na maradhi akiwa gerezani ambapo alilazwa katika Hospitali ya Saratani ya Ocean Road.

Ilikuwa mshike mshike wakati Zombe alipokuwa akitoka mahakamani.

Gonga link chini kutazama picha za Zombe akiwa mahakamani na baada ya kuachiwa.

http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=2839946&&Cat=1
 
SERIKALI imesema haijaridhika na hukumu iliyowaweka huru watuhumiwa kwenye kesi ya mauaji ya kukusudia ya wafanyabiashara watatu wa madini na dereva mmoja na imeamua kukata rufaa kupinga hukumu hiyo.

Katika hukumu iliyosomwa na Jaji Salum Massati juzi, haikuweza kuithibitishia mahakama kuwa watuhumiwa hao tisa, akiwemo mkuu wa zamani wa upelelezi mkoani Dar es Salaam, Abdallah Zombe, walishiriki katika mauaji hayo na kwamba waendesha mashtaka walishindwa kuwafikisha mahakamani wauaji na hivyo kuagiza wasakwe.

Kaimu Mkurugenzi wa Mashtaka, Mary Lyimo alisema katika taarifa yake jana kuwa, ofisi yake imeamua kukata rufaa kupinga hukumu hiyo ambayo pia imepokewa kwa hisia tofauti na wananchi.

"Katika uamuzi huo, Mahakama Kuu ya Tanzania, baada ya kuuchambua ushahidi uliotolewa na misimamo mbalimbali ya kisheria, iliona kuwa upande wa mashtaka (Jamhuri) ulikuwa umeshindwa kuthibitisha mashtaka yake dhidi ya washtakiwa pasipo kivuli cha mashaka kama inavyotakiwa katika mashauri ya jinai," inasema taarifa yake.

"Hivyo iliamua kuwaachia huru washtakiwa wote waliokuwepo. Uamuzi huo umepokewa kwa hisia tofauti na umma. Ofisi hii inapenda kuufahamisha umma na kuuhakikishia kuwa hatukuridhishwa na uamuzi huo; hivyo sasa tunaanza mchakato wa kukata rufaa kwa kutoa Taarifa ya Nia ya Kukata Rufaa."

Upande wa mashtaka ulionekana kuyumba wakati wa majumuisho yake wakati ulipomwomba jaji kuwatia hatiani watuhumiwa na kwamba kama aliyekuwa mshtakiwa asingepatikana na hatia ya kuua bila ya kukusudia, atiwe hatiani kwa kushiriki kosa baada ya kosa, ombi ambalo Jaji Massati alilikataa kwa maelezo kuwa halimo kwenye mashtaka.

Wakati serikali ikijipanga kukata rufaa, wanasheria mbalimbali wamekuwa na mitazamo tofauti juu ya hukumu hiyo, wakiwemo ambao walisema kutotiwa hatiani kwa washtakiwa hao, ambao wote walikuwa askari wa Jeshi la Polisi, kumetokana na uzembe wa serikali katika kufanya uchunguzi na kuandaa mashtaka.

Naye wakili wa kujitegemea na mtaalamu wa masuala ya sheria, Profesa Abdallah Safari amesema kushindwa kwa serikali katika kesi hiyo ni kashfa.

Profesa Safari aliiambia Mwananchi kuwa, kuachiwa huru kwa watuhumiwa hao kunaonyesha kuwa kulikuwa na mapungufu makubwa ya kisheria katika pande zote zilizohusika na kesi hiyo.

Profesa Safari alisema inawezewekana Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) wa wakati huo aliamua kufungua kesi hiyo kwa kuzingatia taarifa ya tume ya Jaji Musa Kipenka kutokana na joto la shinikizo la kisiasa kwa wakati huo.

“Unajua tume hii iliundwa na Rais Kikwete... inawezekana DPP aliamua kuichukua taarifa hiyo kama ilivyo na kufungua kesi bila kuangalia zaidi mbinu za kisheria, alisema Safari.

“Siku zote lazima ieleweke kuwa duniani kote kesi haiendeshwi kisiasa, bali inaendeshwa na ushahidi uliopo,” alisema Profesa Safari ambaye aliwahi kugombea uenyekiti wa chama cha kisiasa cha CUF.

Mwanasheria huyo alisema Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) ndiye aliyekuwa na wajibu wa kuwakamata wauaji na kuwasilisha faili lao kwa DPP.

“Sijaziona nyaraka kutoka kwa DCI kwenda kwa DPP, lakini nahisi upelelezi haukufanywa vizuri,” alisema Profesa Safari na kuongeza kuwa serikali haikupaswa kushindwa katika kesi hiyo kwa kuwa ilikuwa na kila kitu.

“Hii ni sawa na mpishi kuwa na kila kitu, lakini ameshindwa kupika chakula kizuri, hivyo kuna umuhimu serikali ikajiangalia vizuri katika hili.”

Aliitaka serikali kutokata rufaa kwa jazba na badala yake ijiridhishe na ikiwezekana ijaribu kuomba msaada kutoka kwa wanasheria wengine wa kijitegemea wenye uwezo wa kupambana na kesi za namna hiyo.

Msomi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk Kennedy Gaston alisema: “Zombe alisema kulikuwa na majibizano ya risasi; alikataza miili ya marehemu kuchunguzwa huku akitaka izikwe mapema. Haya yote ni makosa ambayo yangeweza kumtia hatiani. Si lazima kukimbilia kosa moja la mauaji.”

Msomi mwingine wa UDSM, Lucy Eusebio alisema: “Katika kesi ya mauaji kuna mambo mawili, kuachiwa huru au kunyongwa hadi kufa, na kuna kanuni ya sheria inayosema ni heri kuwaachia wahalifu 100 kuliko kumfunga mmoja asiye na hatia.

“Kwa maana hiyo katika kesi ya mauaji inatakiwa ushahidi ujitosheleze kwa asilimia 100. Hata kama kutakuwa na asilimia 99 ya ushaidi unaoonyesha kuwa mtuhumiwa aliua, hiyo asilimia moja iliyopungua itaifanya mahakama impendelee mtuhumiwa.”

Wakili wa kujitegemea Anney Semu, alisema Jaji Massati ametoa hukumu hiyo kwa haki kwa sababu amefuata sheria na taratibu za kimahakama.

"Ila waendesha mashtaka walishindwa kuendesha kesi hiyo inavyopaswa kutokana na kwamba walikuwa wakisukumwa na hisia za wananchi ya kwamba Zombe ndiye aliyeua," alisema Semu na kueleza udhaifu wao kuwa ni kushindwa kuwachambua washtakiwa na kuwahusisha ipasavyo na mauaji hayo.

"Walichochanganya ni kushindwa kufuatilia kosa lilikuwa linasemaje, badala yake wakafuata hisia zilizochochewa na wananchi kuwa Zombe ndiye aliyeua."

Naye Profesa Issa Shivji alisema, hukumu hiyo imetokana na jaji huyo kutumia ushahidi uliotolewa mahakamani hapo.

"Majaji kazi yao ni kusikiliza ushahidi wa pande zote unaotolewa. Ikiwa ushahidi huo utaletwa kinyume, hukumu yake inaweza kuwa tofauti na kosa lenyewe," alisema Profesa Shivji.

Aliongeza kuwa kutokana na hali hiyo waendesha mashtaka wanapaswa kuwa makini ili kutoa ushahidi ambao unaendana na kosa lenyewe.

Wakati huo huo, Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam limeanza kujipanga upya kumtafuta polisi alinayedaiwa kutekeleza mauaji hayo yaliyofanywa mwaka 2006, Koplo Saad Alawi, ambaye alitoroka muda mfupi baada ya mauaji hayo.

Kamanda wa Polisi wa Kanda ya Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova aliliambia gazeti hili jana kuwa, kazi ya kumtafuta mtuhumiwa huyo ilianza mara moja baada ya hukumu hiyo.

“Tumeanza mkakati wa kumtafuta mtuhumiwa huyo kama mahakama ilivyotuagiza. Tutajitahidi kumsaka mahali popote mpaka atakapopatikana,” alisema Kova, ambaye wakati wa mauaji hayo alikuwa kamanda wa polisi mkoani Mbeya.

“Tunaheshimu agizo la mahakama, ndiyo maana tunaahidi kumtafuta ndani na nje ya nchi. Licha ya kwamba mtuhumiwa alikuwa akitafutwa tangu awali, kwa agizo hili tunaongeza nguvu zaidi,” alisema Kova.

Kova alisema moja ya mbinu itakayotumia kumsaka mtuhumiwa huyo ni kuiomba jamii ishiriki katika kutoa taarifa za mahali alipo.

“Sikiliza... jeshi hili halijawahi kushindwa kumnasa mtuhumiwa na wale wanaotafutwa muda mrefu ndiyo tunawapata kirahisi, hivyo nina hakika tutampata,” aliongeza.

Akizungumzia askari ambao walifukuzwa kazi na baadaye kushtakiwa kwa tuhuma za kuhusika kwenye mauaji hayo, Kamanda Kova alisema polisi inaandaa utaratibu maalumu utakaotangazwa na makao makuu hivi karibuni.
Habari zinasema kuwa baadhi ya watuhumiwa walioachiwa huru wakati kesi hiyo ikiendelea, walikuwa wakilipwa nusu mshahara na sasa wamerejeshwa kazini.
Surce:Gazeti la Mwananchi.
Isije ikawa danganya toto na hii....!
 
Wakati huo huo, Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam limeanza kujipanga upya kumtafuta polisi alinayedaiwa kutekeleza mauaji hayo yaliyofanywa mwaka 2006, Koplo Saad Alawi, ambaye alitoroka muda mfupi baada ya mauaji hayo.

Kamanda wa Polisi wa Kanda ya Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova aliliambia gazeti hili jana kuwa, kazi ya kumtafuta mtuhumiwa huyo ilianza mara moja baada ya hukumu hiyo.

Walikuwa wapi kumsaka muda wote huo? Tangu 2006 ndio wanaanza kumsaka sasa hivi??? They cant be serious!!!!!!
 
Jaji masati amefanya kile kilichopo kwenye taratibu na kanuni za kisheria,wasiwasi wangu ni hao wanasheria wa serikali.
 
Serikali yetu inatupiga changa la macho watakata rufaa lakini hakuna chochote kitakachoendelea wanakata rufaa kuwarizisha wananchi baada ya kuona wananchi wamehuzunishwa sana na kitendo cha wauuaji kuachwa huru sasa mi nauliza swali Zombe aliyetibitika kusababisha vifo hana hatia je wauaji wa Albino itakuwa vipi ?
 
Jaji masati amefanya kile kilichopo kwenye taratibu na kanuni za kisheria,wasiwasi wangu ni hao wanasheria wa serikali.

Hata mimi naungana na usemi wako kwamba inawezekana akawa ametoa hukumu kutokana na kanuni za kisheria lakini ! tatizo langu liko kwa serikali yangu iweje iundwe kamati ishindwe kuleta uchunguzi uliokamilika wenye mapungufu na vile vile iweje serikali ifungue mashitaka bila kupitia ukamilifu wa kamati na kutoa ushahidi ambao haujakamilika kama inavyoelezwa kama iko sahihi sasa selikali haioni kwamba inajiingiza kwenye aibu yani wao wameshindwa na waovu? mimi nalia na hii selikali yetu na ndiyo itakayotuangamiza sasa hivi ya zombe itakuwa kimya yanaanza ma maaskofu na wakina samweli sita na kinachompoza sita ni kuwa mkweli eti wanataka kumpokonya kadi bila hata vigezo vinavyoeleweka hawana hata aibu wanataka kufukia maovu yao wakae wakijua sas hivi hata sisi tuliokuwa tumelala tumeamka tunahitaji kujua haki zetu ziko wapi sasa ni muda muafaka.
 
huko ni kupoteza muda

Si kupoteza muda tu mpendwa wangu hujui ujanja wao we unafikiri nini kama kesi imekwisha posho watapata wapi lazima wakate rufaa wapate kutumbua vizuri kodi zetu kwa sababu ya kuendesha kesi ambayo at the end wao wanaonekana wajinga kwani wanashindwa kutoa ushahidi wa kujitosheleza wala hakimu si mtu wa kulaumiwa !
 
Walikuwa wapi kumsaka muda wote huo? Tangu 2006 ndio wanaanza kumsaka sasa hivi??? They cant be serious!!!!!!

Sio tu kutokuwa serious wanataka kuoneka wako bizy na kazi lakini hakuna lolote kwani ndugu yangu ni nani mjinga atangaziwe kwenye vyombo vya habari kwamba anatafutwa na selikali kisha ajiweke wazi ili akamatwe wao wenyewe wameaamua kuupoteza ushahidi basi watulie waangali mambo mengine ya umuhimu ya kufanya waachane na haya ya kupote time.
 
Hata hivyo ndugu zangu inashangaza saza iweje watuhumiwa 9 ambao hawana koza la mauaji wamekamatwa na kufikishwa kwenye chombo cha sheria lakini basi muuaji katoroka kivipi hatujui sisi wote mimi pamoja na wewe lingine aliyekuwa na ushahidi wa kutiwa hatiani hawa hawa 9 amekufa kivipi kwa njia gani ( IGIZO) mimi na wewe (GIZA) hivi haya yote yanaingia kweli akilini mwa watanzania ?
 
Back
Top Bottom