GE2025 Kesi ya ACT Wazalendo na Mpina dhidi ya Tume INEC imefanyika kwa njia ya Mtandao

GE2025 Kesi ya ACT Wazalendo na Mpina dhidi ya Tume INEC imefanyika kwa njia ya Mtandao

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Kesi ya Luhaga Mpina wa ACT -Wazalendo dhidi ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) sasa inasikilizwa kwa njia ya mtandao.

Chama cha ACT-Wazalendo kimefungua shauri la maombi kuhusiana na uteuzi wa mgombea wake wa nafasi ya urais, Luhaga Mpina, baada ya INEC kumzuia kurejesha fomu yake ya kuomba uteuzi aliyokabidhiwa awali kuijaza.

Shauri hilo limefunguliwa Mahakama Kuu Masjala Kuu, Dodoma, jana Jumatano, Agosti 27, 2025, ambapo chama kimeiomba Mahakama hiyo iielekeze INEC kupokea fomu ya mgombea wao huyo kwa ajili ya uhakiki na uteuzi.

Mapema leo Agosti 28,2025 katika Mahakama Kuu Dodoma, Majaji walianzia kwenye kikao na Jaji Mkuu na baada ya kumaliza waandishi waliitwa na kuambiwa kuwa kesi itasikilizwa kwa njia ya mtandao.
Baada ya hapo kilitolewa kiunganishi kwa ajili ya kusikiliza mwenendo mzima wa kesi mbele ya majaji

Soma pia:



1756387328239.png


1756387274124.png



Chanzo: Mwananchi_official
 
..ACT shauri lao linasikilizwa chap chap.

..Chadema wakilalamika wanapigwa danadana na mahakama.
 
Mpaka hukumu itakapotoka, muda wa kurudisha fomu INEC utakuwa umeisha
 
abdul nonda kaona Picha anajichekesha, PUMBAV kabisa
 
abdul nonda kaona Picha anajichekesha, PUMBAV kabisa
huyu dogo simwelewagi na huo mdomowake ulivyo mkubwa nawala hana aibu anaboa sana kumwiga zitokabwe hata kuongea hata Katibu wao wanajitaka kuwa kama zitokabwe
 
Back
Top Bottom