Kesi ya Agnes Doris Liundi - Nini hasa kilitokea?


You are right, subjective interpretation is a problem. Just like many of Tanzanian judges do, especially where there are some interest involved. Likewise appealling system is there to make sure there is checks and balance, very unfortunately it doesnt work with our political courts here in Tanzania
 
mkuu watu kama nyie huwa mna visa vingi na vya kutosha nakushauri uviwasilishe kwa wanaohusika kama mtambuzi wavirushe hewani
 
Wanasheria bana,hamkosagi maneno.Haya bana.

Wakikosa maneno wanasema "Masharti na Vigezo kuzingatiwa". Hapo unakuwa umeingia mkenge bila kujijua!

Asante "Mtambuzi kwa kunikumbusha hii kesi. Ilisikitisha sana wakati ule na bado inasikitisha. Kuna mengi ya kujifunza hapo hususan kwenye mahusiano. Ndoa inataka, pamoja na mambo mengine, uvumilivu, subira na imani. Yote yanapatikana katika Upendo.
 
Nilibahatika kukutana na mzee Liundi baada ya kustaafu maeneo ya kinondoni baada ya kutambulishwa na jamaa yangu.Mwenyezi Mungu anampigania maisha yanasonga mbele kila jambo hutokea kwa sababu maalum na ni Mola pekee ajuaye sababu husika za tukio.Mzee Liundi,mwanao Taji na mama Taji yaliyopita si ndwele tugange yajayo na kwa mapenzi yake Mola atawafanikisha.
 

Ronn M ........Lakini pia Agnes Doris Liundi alikata rufaa na hakushinda na Mheshimiwa Jaji akakubaliana na hukumuya Mahakama Kuu..............
Hapa naomba kuelimishwa, katika kesi ya Asha Mkwizu Mheshimiwa Jaji Bahati, alinukuu maelezo ya Mheshimiwa Jaji Makame aliyehukumu kesi hii ya Agnes Doris Liundi ambapo alirejea kesi moja iliyowahi kutokea nchini Uingereza, lengo lilikuwa ni kuelezea dhana ya "diminishing responsibility"

Naomba ninukuu kipengele hicho hapa chini..............

"Hata hivyo Mheshimiwa Jaji Bahati alieleza kwa kirefu juu ya dhana ya "diminishing responsibility." Akizungumzia dhana hiyo alitolea mfano kesi ya mwaka 1978 ya Jamhuri dhidi ya Agnes Doris Liundi. Mheshimiwa Jaji Makame, J. Alirejea kesi ya Uingereza ya R.v. Julia Everton ambapo sheria hiyo kwa kule Uingereza inayo nafasi, ambapo mtuhumiwa huyo aliwekwa chini ya uangalizi kwa muda wa miaka mitatu. (Probation)Jaji aliendelea kusema kwamba, kwa Tanzania hatuna sheria hiyo, na itakuwa ni kinyume na taaluma yake kwenda nje ya mipaka yake."

Mwisho wakunukuu...............

Hapo kwenye BOLD ndipo ninapotaka kupazungumzia.............Je kulikuwa na haja gani kwa Mheshimiwa Jaji Makame J, kurejea kesi ya Uingereza wakati hata hivyo hakuwa na uwezo wa kuhukumu wa kufuata hukumu ya kesi hiyo..............?

Baada ya kesi hiyo, Je, Bunge letu tukufu liliwahi kukaa na kurejea sheria hiyo ili iende na wakati kama ilivyoshauriwa na wataalamu wa tiba pamoja na Mheshimiwa Jaji......?
 
Hebu tumsubiri mtaalamu wetu Ronn M atujibu........


Labda nijibu hili la jury trial kwanza, Mfumo wa Jury unatumika kwa nchi za wenzetu! Sasa

hapa mara nyingi wanachukuliwa watu wasio wanasheria lakini wanasikiliza mwenendo wa kesi

tangu mwanzo mpaka mwisho! Lengo lao hapa ni kusema nani ana hatia kwa mwenendo

mzima. Uamuzi wao unakuwa wa mwosho.

Kwa hapa Tanzania hatuna jury system, wapo wazee wa baraza wanaoitwa assessors. Hawa

wanakaa katika kila kesi mahakama ya mwanzo na kwa baadhi ya kesi mahakama kuu

zikiwemo kesi za mauji! Hawa huwa wanakuwa watatu na Judge/Hakimu huwa anawasikiliza

wameamuaje! Ikiwa jaji anasababu ya kutofautiana nao kwa mahakama kuu, anatoa sababu

na uamuzi wa mwisho unakuwa wa jaji.

Kwa sababu hiyo nadhani kesi ya Doris walikuwepo wazee wa baraza na sio jury maana

Tanzania hatuna
 


Katika kuamua kesi kuna majaji wa aina mbili, Bold Spirits and Timorous Souls. Bold Spirit ni

wale majasiri. Hawa wanakuwa tayari kutafsiri sheria katika namna ambayo haki inatendeka. Hii

ina maana kama sheria haiko sawa au inaleta 'undesired results' which are against justice, yeye

atatafsiri katika namna inatakayo leta haki. Ni kama vile anatunga sheria mpya! Alikuwepo Lord

Denning wa uingereza na hapa Tanzania kina Mwalusanya na Lugakingira wamekuwa na mfano

huo (Rejea kesi za Mtikila, kesi za wafanyakazi kadhaa waliofukuzwa kazi for 'public interest',

Kesi ya Daudi Pete(on Bail) nk!

Timorous Soul hawa ni wale wanaofuata sheria kama ilivyo. Hata kama it will lead to so

unreasonable and absurd results.

Utagundua hawa majaji wetu wamekuwa waoga kuleta mabadiliko katika sheria. Mfano ni Justice

Bahati ambaye unaona anaonesha kuwa nchi nyingine wamefuata mtindo huo lakini yeye

anaamua kutokufuata! Ni kama vile anaogopa!

Sina kumbukumbu kama Bunge letu limebadilisha hilo, lakini kwa Sheria ya Makosa ya Jinai

(Penal Code Cap 16) ambayo ni current version, mabadiliko hayo hayapo. Hivyo ndo kusema,

bado sheria hiyo haijaingizwa hapa Tanzania. Si rahisi sana kwa serikali kufanya marekebisho

yenyewe maana 'ilishinda' kwenye kesi hiyo. Njia nzuri ni kwa Mahakama kutamka kuwa sheria

hiyo inatumika Tanzania (na hivyo bunge kuiweka katika vitabu vya sheria) au Law Reform

Commission kupendekeza mabadiliko hayo!
 
huyo dokta hauli /specialist ea psychos si ndio ambae baadae mkewe alimpiga hawara wa mumewe vinondo akamzika nyumbani....rejea kisa chako kimoja ch mauaji ya mke wa dk hauli....MTAMBUZI
 
Umeona eeh. Hii case mi nilikuwa naijua mama alishawahi kutusimulia (alikuwa inspector those daysl); ila nimesoma yoote a mpaka z maana ya kusimuliwa ni ya kusimuliwa; material fact mengi yanaachwa kwenye simulizi. Mfano mi nlichokuwa najua aliamua kujiua na wanawe kwa sababu baba alikuwa hajatulia kumbe sivyo.

 
Somo nililojifunza ni kuwa mama zetu walikuwa na mapenzi ya kweli; kila nkiangalia kizazi chetu wa kujiua eti kisa mume hamtaki simuoni.

huyo dokta hauli /specialist ea psychos si ndio ambae baadae mkewe alimpiga hawara wa mumewe vinondo akamzika nyumbani....rejea kisa chako kimoja ch mauaji ya mke wa dk hauli....MTAMBUZI
 
Kama wewe hujui basi sidhani kama yeye atajua maana katika utafiti wako ulioufanya walau jury na jurors wangetajwa tu.
Nyani Ngabu Ukweli ni kwamba sikupata nakala ya kesi ya Mahakama Kuu bali nilipata nakala ya kesi ya rufaa na ndio sababu imekuwa kama haijajitosheleza, hakuna maelezo ya mashahidi na pia ushauri wa wazee wa baraza kama ilivyokuwa kesi ya Asha Mkwizu Hauli...........Kwa bahati mbaya juhudi zangu za kupata Kesi ya mahakama kuu hazikuzaa matunda. naomba radhi kwa hilo.
 
Last edited by a moderator:
nyumba kubwa Ni kweli wengi walikuwa wanajua hivyo na hata baadhi ya wasomaji kwenye kesi ya Asha Mkwizu niliyoiweka humu majuma kadhaa yaliyopita wali- comment hivyo........... Nilipoisoma kesi hii ndipo nilipoujua ukweli na kutokana na maombi ya wasomaji wengi wa JF nikaona ni vyema niiandike ili ku- clear hiyo assumption
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…