Kesi ya Babu Seya na wanae - Ukweli ni upi haswa?

Rudi kwa kwa mwalimu wako binti
 
Nimeangalia furaha ya watu waliokuwa wamehukumiwa kwa kosa kubwa la ubakaji na ulawiti tena wa watoto wadogo nimeshindwa kupata jibu.
Jee habari za matendo ya Babu Seya kwa wale watoto zilikuwa za kugushi na kuwa walifanyiwa mchezo mchafu? Au ni kuwa kwa sababu ya ushabiki tuu basi Watanzania wanasahau machungu waliyopata wale watoto, wazazi wao na ndugu? Kweli taifa linaweza kufikia hali ya kutojitambua kiasi hicho?
Kwa nini sasa ukweli usiwekwe wazi maana ukisoma ile barua ya Papii kwa Rais alikuwa haombi msamaha bali anaomba waachiwe huku akisisitiza kuwa hata Mungu anajuwa hawakutenda kosa. Nani nchi hii anaweza kuwapa wenzie mashtaka makubwa kiasi kile ili familia ipotee daima? Jee mtu au kikundi hicho hakiwezi kuua kabisa?
Sasa ukweli (ambao kina watu wanaujua) uwekwe wazi kwa faida ya jamii ili kuepusha visasi.
 
Yote mawili yanatuhusu, ama tulidaganywa kuwa watuhumiwa walitenda kosa hilo au tulidanganywa kuwa watuhumiwa walionewa tu na kigogo mmoja. Lakini pia hatujitambui ndio maana kwa miaka yote hii tumekosa watu makini hasa waandishi wa habari wa kulichunguza jambo hili ili tupate ukweli hasa.
 
Asante Bob,umenisaidia mambo mengi.
 
Mahakama zote tatu ziliwakuta wana hatia, na historia itabaki hivyo kuwa walibaka watoto, ila walipata msamaha wa rais.
 
 
Ukweli unajulikana... Ila kama ni kweli walibaka na wakawalawiti watoto wadogo.... Mh. Rais itakua hakuzitendea haki familia za watoto hao. Aidha vyovyote iwavo, mimi cungi mkono kabisa wananchi kuwafanyia shangwe watu hao wakati wakitoka gerezan.... Maana ni iman yangu kua hakuna mwananchi anaeufaham ukweli wa suala hili... Kushangilia kuachiwa huru kwa watu hawani kutojitambua kuliko chupa mipaka.
 
hili swali ilibidi mjiulize siku ile Lowassa alipotangaza nia ya kutaka kuwaachia huru endapo angeshinda urais,zaidi ya hapo mnaonyesha unafiki tuu.....
 
Ndugu Chakaza hii ishu ya kesi ya akina babu Seya ilishajadiliwa sana humu. Tuseme wazi tu kesi yao kwa kiasi kikubwa ina kila dalili za kubambikiwa na ndio maana pengine jamii imefurahi kuona wameachiwa huru.
 
inafaa wale waliosababisha maisha ya mtu kupotea kwa miaka 14 wawajibishwe..............
 
Vyovyote itavyokuwa tatizo ni chama chenye kuongoza serikali ndio maana wanatumia udhaifu katiba yetu kila siku kutafanya malofa ndio maana hawa hataki kusikia wala kubadili katiba yetu kidumu chama tawala...
 
Mahakama zote tatu ziliwakuta wana hatia, na historia itabaki hivyo kuwa walibaka watoto, ila walipata msamaha wa rais.
Sawa kabisa, hivyo dhana ya kuwa in taifa la wasiojitambua inapata mashiko. Msamaha wa Rais hauna shida kwani anaweza kumsamehe yeyote lakini kama tuna hakika mahakama zilitenda haki basi hakukuwa na sababu ya kushangilia kuachiwa kwao bali ilitakiwa mambo hayo yaende kimya kwa ajili ya wahanga wa vitendo vile!
 
Sishangai watanzania kushangilia uovu.Ni kama huwa wanayayaona mambo kinyumenyume.Mnakumbuka ya David Jairo na waziri wake wa nishati kipindi kile?
 
Vyovyote itavyokuwa tatizo ni chama chenye kuongoza serikali ndio maana wanatumia udhaifu katiba yetu kila siku kutafanya malofa ndio maana hawa hataki kusikia wala kubadili katiba yetu kidumu chama tawala...
Huwa siamini sana hapa nchini kuna chama kinachoongoza serikali. Naona kuna serikali inayoongoza chama. Vyama ni kama jando tu,unapitia hapo kisha unaoa. Mke siyo wa jando wala ngariba,ni wako.
 
Unaanza kuleta siasa hapa!
sio siasa ni miaka mingapi toka hukumu itolewe??ni miaka mingapi toka mgombea mmoja atumie swala hili kama hoja ya kuingilia ikulu??kwani muda wote huo tulishindwa kutafakari mpaka leo wameachiwa huru ndo tunakumbuka kuanza kuulizauliza?effect yake ipo wapi kwa hivi sasa?
 
Karibu kwenye ulimwengu wa siasa za dunia,chochote kinawezekana,ushaidi unaweza ukatengenezwa,ajari pia zinatengenezwa,
Wakubwa wa nchi/dunia wanapokuwa na maslahi na jambo Fulani,chochote kinaweza fanyika,ile kesi ilikuwa na viongozi wakubwa nyuma yake,
Siku zote,vitu huwa viko tofauti na vinavyoonekana,
Boko haram,vita ya Congo,ni deception ya hari ya juu,kwa nchi kama USA,military industries,ni sekta inayoingiza pesa nyingi sana,sasa silaha zote wanazozalisha,watauza wapi,kama vita zitaisha pande zote za dunia,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…