Kesi ya Babu Seya na wanae - Ukweli ni upi haswa?

Kesi ya Babu Seya na wanae - Ukweli ni upi haswa?

Nawawekea hapa uamuzi kamili wa Majaji wa Mahakama ya Rufani nchini inayowahusu Babu Seya na Papi Kocha. Nimearifiwa kuwa Rais Magufuli alifanya mazungumzo na Babu Seya jana Ikulu, Dar es Salaam.

Jisomee kwa umakini, utulivu na uelewa kuwahusu watu hawa waliosamehewa na Rais. Naiweka nyaraka hiyo hapa. Jisomeeni halafu mtafakari.

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Nairobi, Kenya)
Acha fix zako hapo mkoa wa Pwani ndio Nairobi?!!...... Tunakuona ujue!
 
Mtu mmoja anatuover power wote
Ndio raha ya kuwa rais ndio maana watu huwa wanapambana sans
 
Mkuu tulia, JPM hajawafutia hukumu. Ila kawasamehe kwa mamlaka aliyopewa na katiba.
Hukumu iliyoka wakapayikana na hatia na wakakaa jela, wamesamehewa!
Wewe unataka tusome tena makaratasi ya hukumu tena sijui kurasa ngapi, huo muda wa kusoma irrelevants tunautoa wapi??
 
Ushahidi wote uliopo ni kwamba ni kweli hao Nguza na wanawe walifanya huo ufirauni. Sijui sababu yao ya kufanya hivyo ilikuwa nini. Wanaharakati wa haki za watoto na za binadamu walishiriki pia kwenye hiyo kesi, na kuna mafaili ya kutisha sana. Watoto waliofanyiwa hivyo wapo na walitoa ushahidi, ambao kisheria ili kulinda haki za mtoto aliyelawitiwa na kumkinga dhidi ya unyanyapaa, haipaswi kufanywa hadharani na wala majina yao hayatolewi kwenye vyombo vya habari. Mafaili ya Muhimbili walikopimiwa hao watoto na ripoti za madaktari zipo. Yaani hii ilikuwa soo, hawakuwa na jinsi ya kukwepa.

Na huy si wa kwanza. Miaka ya mwisho ya 1980's alitokea fundi mshona nguo akiitwa Ali Maumba, alikuwa akiwafanyia watoto mchezo huohuo, na alilawiti zaidi ya 100, ila wengine wazazi wao waliwazuia wasijitokeze ili kukwepa aibu kwa familia zao. Ile kesi Maumba alihukumiwa kifungo, lakini alipokata rufaa alishinda kutokana na ushahidi "dhaifu" wa madaktari. Na ile kesi ya Maumba hadi leo inatumika kama reference ya kuwakumbusha madaktari umuhimu wa "ushahidi wa kitaaluma" (expert witness) kuandikwa vizuri. Rafiki zangu wanaharakati wamei-cite mara nyingi sana kwenye papers zao.

Hii ya kina Babu Seya, wanasheria walijaribu sana wakakosa pa kutokea. Na hata wakati wa rufaa, haikuwezekana, akaendelea kubaki hatiani.

Hizo habari za kuwasingizia kina nani sijui ni uvumi tu, kungekuwa na ukweli tungeshapata japo chembe ya ushahidi. Hao mnaowataja wakati huo hawakuwa na mamlaka yoyote dhidi ya mahakama, na hata katika kesi hakuna wakili au yeyote aliyeleta ushahidi wa kuwahusisha. Kama ni rushwa, sijui ni rushwa gani watu wangetembeza kila mahali kuanzia kwa watoto wa shule ya msingi, walimu wao, wenyeviti wa serikali za mitaa, askari polisi kwenye posts hadi kwa waendesha mashtaka, wanaharakati wa haki za watoto, mawakili, wafanyakazi wa idara za hospitali (wauguzi, watu wa records, maabara,madaktari, ili ati wote wafoji habari zinazoendana), hakimu mkazi kisutu, majaji wa mahakama kuu, majaji waheshimiwa sana wa mahakama ya rufaa, woote hao utawahonga vipi? Kazi ya ku-organize na ku-stage plot kama hii ni kubwa na haiwezi kuwa siri, lazima ziwepo flaws, hata kama ni fiction unatunga wasomaji wataona tu uongo ulipo!

Kwa hiyo sioni cha kujadili kuhusu Babu Seya na wanawe, alipata haki yake ya fair trial, akawa convicted, na sheria ikachukua mkondo wake. Akatumia pia haki yake ya appeal, nako hatukusikia malalamiko ya unfair trial, akabakia guilty as charged. Basi.

..... Nilitegemea baada ya msamaha wa rais Babu seya na wanawe wafanye mambo matatu, Kwanza wamshukuru Munngu kwa kupata msamaha, Pili wamshukuru rais kwa kuwasamehe, Tatu wawatangazie watanzania kuwa hakukuwa na ukweli kwenye ile kesi hivyo walionewa!
Sinashaka wamemshukuru Mungu, Jana wamekwenda kumshukuru rais, wamefanya vema sasa nawasubiri wakanushe kuwa hawakuwahi kushiriki kwenye lile kosa. Nilichowasikia wakisema ni kuwa, wanashukuru kwa kusamehewa na kuhakikishia umma kuwa watakuwa wananchi wema" Kauli hii inaonyesha kuwa kabla ya hapo hawakuwa wema ndiyo maana walipatikana na hatia. Sio dhambi kama ulionewa ukakiri ili watu wajue dhulma zilizopo
 
..... Nilitegemea baada ya msamaha wa rais Babu seya na wanawe wafanye mambo matatu, Kwanza wamshukuru Munngu kwa kupata msamaha, Pili wamshukuru rais kwa kuwasamehe, Tatu wawatangazie watanzania kuwa hakukuwa na ukweli kwenye ile kesi hivyo walionewa!
Sinashaka wamemshukuru Mungu, Jana wamekwenda kumshukuru rais, wamefanya vema sasa nawasubiri wakanushe kuwa hawakuwahi kushiriki kwenye lile kosa. Nilichowasikia wakisema ni kuwa, wanashukuru kwa kusamehewa na kuhakikishia umma kuwa watakuwa wananchi wema" Kauli hii inaonyesha kuwa kabla ya hapo hawakuwa wema ndiyo maana walipatikana na hatia. Sio dhambi kama ulionewa ukakiri ili watu wajue dhulma zilizopo

Hawa walitenda kosa. Hata kama kulikua na figisu lakini KOSA lililowapeleka jela walilitenda.
 
..nchi hii imekuwa kama nyumba iliyokosa watu wazima.

..inawezekana vipi mbakaji watoto akatumbuiza mbele ya Mawaziri na Wabunge?

..kwenye dunia hii ya utandawazi tunajenga picha gani huko nje kwa viongozi wetu kuenenda namna hii.

..halafu Papii Kocha mbakaji anajitamba kwamba ni mwana-CCM. chama ambacho kinasifika kuwa ni CHAMA CHA UKOMBOZI AFRIKA.

..Je, hii CCM ya Papii Kocha, ndiyo ileile ya Mwalimu Nyerere, Rashidi Kawawa, Moringe Sokoine, Aboud Jumbe,Thabit Kombo Jecha, Hassan Nassoro Moyo, na wengine tunaowaenzi?

..Halafu tukiitwa "shit-hole" country tunakasirika.


 
Tatizo ni kujitangaza kuwa mwana CCM au kuwa mbakaji aliyesamehewa?
 
Tatizo ni kujitangaza kuwa mwana CCM au kuwa mbakaji aliyesamehewa?

..CCM ya Mwalimu Nyerere, Rashidi Kawawa, Moringe Sokoine, Aboud Jumbe, Thabit Kombo Jecha, Hassan Nasoro Moyo?

..unaweza vipi kuruhusu mbakaji watoto ndani ya chama kilichoasisiwa na miamba hao niliowataja hapo juu?
 
Narudia tena swali, tatizo ni kujitangaza kuwa ccm, kutumbuiza mawaziri au kuwa mbakaji aliyesamehewa, wewe mrwanda awamu ya Kikwete uliipenda sana serikali yake sababu hakuwa anapatana na Kagame au labda ulikuwa mnufaikaji.
Sasa huyu ngosha kupatana na paka kagame umekuwa na kihoro sana. Shithole mwenyewe.
 
Shithole musicians (first definition of shithole) from a shithole country (second definition of a shithole) are performing their music in front of ministers.

Zifuatazo ndizo tafsiri za shithole....
1. Kinyeo cha mwanadamu
2. Mambo/Kitu/Mtu/sehemu ya hovyo hovyo
3. Tundu la choo.
 
..CCM ya Mwalimu Nyerere, Rashidi Kawawa, Moringe Sokoine, Aboud Jumbe, Thabit Kombo Jecha, Hassan Nasoro Moyo?

..unaweza vipi kuruhusu mbakaji watoto ndani ya chama kilichoasisiwa na miamba hao niliowataja hapo juu?
Unadhani hao uliowataja hawakuwa na uchafu/ dhambi? Hakuna mkamilifu, tusamehe na kusahau, ili maisha yaendelee.
 
Ccm ya sasa hata hao wenye kusimamia misingi ya chama wamejitenga nayo kutokana na aina ya siasa za kishamba zinazofanywa na Jpm na Chakubanga.

Huo msamaha wa hao wabakaji unaonekana ulikuwa na malengo ya kisiasa nyuma yake
 
Back
Top Bottom