Najiuliza tuchukulie kweli walitenda kosa kama mahakama ilivyoona, je kwa miaka hiyo waliokaa gerezani(nadhani ni zaidi ya kumi) jamii haijawasamehe kiasi wakiachiwa kwa msamaha wa Rais kuna ataelalamika? Kuna watu bado watakua hawana huruma kwa jamaa hawa? Muda wote waliokaa gerezani haujatosha kuwapa fundisho?
Inawezekana kwa wale watoto walio athirika wakaishi na msongo wa mawazo ya ukatili huo kwa muda mrefu kiasi lakini miaka zaidi ya kumi kwa kumuadhibu mtu kifungo jela sio inatosha na mtu anaweza kubadilika na kua raia mwema?
Binafsi naiona adhabu ya kifungo cha maisha ni ya ukatili na isiyofundisha kuliko hata adhabu ya kifo ambayo kwa duniani maumivu yake ni maramoja tu. Hivi ukimfunga mtu maisha utakua umemsaidia kubadilika? Hata hizi taasisi za kutetea haki za binadamu hawajawahi kutafakari jambo hili? Ni bora wangekatiwa kifungo hata cha miaka ishirini ambapo wanakua na matumaini siku moja watakuja kujumuika na binadamu wenzao uraiani wakiwa wametubu na kujifunza kuliko kujua na kuishi na uhalisia kwamba Dunia yako imeshafungwa na maisha yako hutaliona tena jua la matumaini ukiwa mtu huru, ni adhabu yenye kuogofya sana na haisaidii mtu kubadilika