Kesi ya Elizabeth Michael (Lulu), Mke wa Dk. Slaa ahitajika kufika mahakamani kutoa ushahidi

Kesi ya Elizabeth Michael (Lulu), Mke wa Dk. Slaa ahitajika kufika mahakamani kutoa ushahidi

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Kesi ya kuua bila kukusudia inayomkabili muigizaji wa filamu bongo Elizabeth Michael, (Lulu) imeendelea leo katika mahakama kuu jijini Dar es salaam, ambapo upande wa utetezi umeshindwa kuendelea kutoa ushahidi wake kwa kukosekana shahidi mwingine ambaye ni mke wa Dr. Slaa

slaa.jpg

Shahidi huyo aliyetajwa kuwa ni mke wa aliyekuwa katibu mkuu wa CHADEMA, Dk. Wilbroad Slaa, Bi. Jacqueline Mushumbusi ambaye yuko nje ya nchi, ushahidi wake umekataliwa kupokelewa na mahakama mpaka awepo mwenyewe au askari ambaye aliandika maelezo yake afike mahakamani kutoa ushahidi huo.

Hapo jana wakili wa mshtakiwa Peter Kibatala aliiomba mahakama iruhusu kupokelewa kwa ushahidi utakaotumwa na Bi. Mushumbusi, lakini mahakama imekataa ombi hilo ikisema upande wa utetezi hauwezi kusoma ushahidi huo na kutoa uamuzi wake wa kutaka shahidi awepo mwenyewe au askari aliyeandika ushahidi huo.

Kesi hiyo imeghailishwa mpaka kesho Oktoba 25, ambapo inatarajiwa askari aliyeandika ushahidi wa Bi. Jacquline Mushumbusi, kuwasili mahakamani hapo na kutoa ushahidi wake.

EATV
 
Mchumba wa Dr Slaa akatoe ushahidi kuhusu Mchumba wa Marehemu Kanumba!!!
 
20171024105115.jpg

Kesi ya kuua bila kukusudia inayomkabili muigizaji wa filamu bongo Elizabeth Michael, (Lulu) imeendelea leo katika mahakama kuujijini Dar es salaam, ambapo upande wa utetezi umeshindwa kuendelea kutoa ushahidi wake kwa kukosekana shahidi mwingine .

Shahidi huyo aliyetajwa kuwa ni mke wa aliyekuwa katibu mkuu wa CHADEMA, Dk. Wilbroad Slaa, Bi. Jacqueline Mushumbusi ambaye yuko nje ya nchi, ushahidi wake umekataliwa kupokelewa na mahakama mpaka awepo mwenyewe au askari ambaye aliandika maelezo yake afike mahakamani kutoa ushahidi huo.

Hapo jana wakili wa mshtakiwa Peter Kibatala aliiomba mahakama iruhusukupokelewa kwa ushahidi utakaotumwa na Bi. Mushumbusi, lakini mahakama imekataa ombi hilo ikisema upande wa utetezi hauwezi kusoma ushahidi huo na kutoa uamuzi wake wa kutaka shahidi awepo mwenyewe au askari aliyeandika ushahidi huo.

Kesi hiyo imeghailishwa mpaka kesho Oktoba 25, ambapo inatarajiwa askari aliyeandika ushahidi wa Bi. Jacquline Mushumbusi, kuwasili mahakamani hapo na kutoa ushahidi wake.
MKE WA DR.SILAA AITAJIKA KUTOA USHAIDI KESI INAYOMKABILI LULU.

Aisee, Kamanda Mshumbusi huenda akarejea nchini siyo? Karibu sana Mama
 
Nimezoea kuona kesi za watu maarufu kupigwa kalenda mara kwa mara, pengine husikilizwa siku moja tu kisha kupigwa kalenda.... Lakini hii ya lulu karibu wiki Sasa inasikilizwa
 
Kesi inapelekwa mpela mpela....hapo ni kusuka ama kunyoaa mtu

Ova
 
Back
Top Bottom