Kesi ya Freeman Mbowe na hukumu ya mahakama tatu

Kesi ya Freeman Mbowe na hukumu ya mahakama tatu

kamili

JF-Expert Member
Joined
Feb 10, 2011
Posts
1,217
Reaction score
853
Mengi yameongelewa kwenye kesi hii ya Mbowe na tuhuma za ugaidi (wao wanasema makosa ya ugaidi). Kesi hii imevuta mahakama tatu, na mbili kati ya hizo zimeshatoa hukumu ni moja tu ndio bado haijatoa hukumu kama ifuatavyo.

1. Mahakama ya uhujumu uchumi
Mahakama hii inaongozwa na inasikilizwa na jaji ambaye ni mteule wa mshindani mkubwa wa mh. Mbowe katika uwanja wa siasa (yaani mh. rais). mahakama hii itafikia uamuzi baada ya kupokea ushahidi kutoka kwa polisi ambao ni wateule wa mshindani wa kisiasa wa Mbowe. (yaani mh. Rais) na akipatikana na hatia atafungwa katika gereza ambalo wakuu wake wote wameteuliwa wa mshindani mkubwa wa kisiasa wa Mbowe. Na akiachiwa huru itatamkwa na wateule wa mshindani wake mkuu wa kisiasa (Mh. rais).

Haijulikani hukumu ya mahakama hii, lakini mara mbili mh. Rais ametoa kauli ambazo zinaashiria kuwa ana uhakika usio mashaka kuwa Mbowe ni gaidi. Na bila ya shaka ushahidi huo ameupata kutoka kwa watu aliowapa vyeo kwa nafasi yake ya urais. Lakini pia mkuu wa Polisi aliutangazia umma kuwa Mbowe ni gaidi na akasema anayefikiria Mbowe ni Malaika afike mahakamani. Bahati mbaya watu walipofika mahakamani wengine waliishia mahabusu?

Mahakama hii bado haijatoa hukumu kwani bado inasililiza ushahidi na utetezi. tutege sikio tuiache mahakama ifanya kazi yake.

2 . Mahakama ya Umma
mahakama hii inaongozwa na nafsi za watu wote wenye akili timamu. watu hawa wametawanyika dunia nzima. watu hawa si wateule wa kiongozi yeyote duniani. kesi ya Mbowe haiwafanyi wale au wasile. Watu hawa wanasukumwa na dhamira njema nafsini mwao. Watu hawa wamefuatilia kesi hii nukta kwa nukwam

Wamewaona mashahidi (polisi wetu) wakitoa ushahidi, wameona vielelezo vilivyowasilishwa mahakamani, wameona maamuzi ya mh. jaji katika mapingamizi madogo madogo, wamesikiliza maelezo ya watuhumiwa (polisi wetu wanawaita wavunja sheria), wamewaona mashahidi wa watuhumiwa. Mahakama hii ya umma baada ya kusikiliza mpaka shahidi wa nane wa upande wa mashitaka (ambao ni wateule wa mshindani wa kisiasa wa Mbowe) na kusikiliza maelezo ya baadhi ya watuhumiwa, tayari mahakama hii ya umma imeshatoa hukumu. Hukumu ya mahakama hii haiandikwi popote, wale haisomwi popote kwani itabaki kwenye nasfsi zao milele. hukumu ya mahakama hii si lazima ifanane na ya mahakama ya uhujumu uchumi, lakini ni hukumu ya haki. lakini pia inaweza ifanane na hukumu ya mahakama ya uhujumu uchumi lakini ikatofautiana lugha. Mahakama hii huenda ikawa ndio mahakama kubwa zaidi ya haki kuliko zote, lakini uamuzi wake hubaki nafsini na haina jela.

3. Mahakama ya Mungu
Sina hakika kama washtaki, majaji, mashahidi wote na washitakiwa kama kweli wanaamini uwepo wa Mungu muumba wa vyote. Hata hivyo waamini au wasiamini ijulikane tu ipo mahakama kubwa kushinda zote nayo ni mahakama ya Mungu mwenyewe. Yeye ajua kila kitu hata kabla havijatokea. Yeye amfahamu mwovu hata kabla hajatenda, yeye amfahamu mwongo hata kabla hajaongopa, yeye aweza mwazibu mtu adhabu kali kabisa lakini ni MWINGI WA HURUMA NA REHEMA. Anasemehe mara nyingi kuliko kuadhibu, na akiitoa adhabu hutoa ndogo kabisa na hakawii kuifuta. Mahakama hii tayari inayo hukumu, na mahakama hii inayo hukumu ya mshitakiwa, inayo hukumu ya mshitaki, inayo hukumu ya mashahidi, inayo hukumu ya majaji. Mahakama hii itawatolea hukumu wote. Ole wao wale watakaoongopa, ole wao wenye niaBahat

Bahati mbaya hakuna ajuaye hukumu hiyo kwa sababu haitangazwi kwenye vyombo vya habari, lakini ole wao watakaopatikana na hatia na mahakama hii.
 
Back
Top Bottom