Kesi ya ghorofa lililopromoka Kariakoo kuanza kusikilizwa leo. Watuhumiwa 3 wapelekwa mahakamani

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Baada ya takriban miezi miwili, kesi ya kuua bila kukusudia inayowakabili wamiliki watatu wa jengo lililoporomoka mtaa wa Mchikichi na Congo, eneo la Kariakoo, itatajwa Leo Januari 13, 2025 katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es salaam.

Kesi hiyo inasikilizwa na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Godfrey Mhini na washtakiwa wote wapo nje kwa dhamana na upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika.

Wamiliki hao, ambao wote ni wakazi wa Jiji la Dar es Salaam ni Leondela Mdete (49) mkazi wa Mbezi Beach, Zenabu Islam (61) mkazi wa Kariakoo na Ashour Awadh Ashour (38) mkazi wa Ilala, wanakabiliwa na mashitaka 31 ya kuua bila kukusudia katika kesi ya mauaji namba 33633/2024.

Kwa mara ya kwanza washtakiwa hao walifikishwa mahakamani hapo Novemba 24, 2024 na kusomewa kesi hiyo.

Manara.png

Source: Manara TV
 
Kuwashitaki wamiliki peke yao bila wakaguzi majengo pamoja na ma engineer ni kazi bure,wamiliki wao ndiyo wataalamu wa ujenzi kwani!!??mbona kama tunachezeana maigizo tu!!??
 
Back
Top Bottom