Kesi ya Jerry Muro imeishia wapi?

Kesi ya Jerry Muro imeishia wapi?

hekimatele

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2011
Posts
9,890
Reaction score
2,795
Habari zenu wandugu jukwaani. Natumai wote tu wazima.
Nilikua napenda kujuzwa kwa yeyote mwenye tetesi na habari ya kesi ya Jerry Muro aliyekua mtangazaji wa TBC. Mda umeenda na sijajua imefikia wapi
Ahsanteni
 
Any one with info regarding this topic?
 
Inaendelea kuunguruma, ushahidi wa utetezi umeanza kutolewa.
 
Inasemekana Jamaa awana ushaidi wa kutosha wanatafuta jinsi ya kumaliza mambo
 
Huyo Wage nae ni fisadi no 1 ameiba pesa nyingi sana kwenye miradi ya bagamoyo kupitia dada yake Kombani..acha iishe kesi ya Jerry ije yake tunaisubiria kwa hamu sana ingawa nasikia mmoja walioshitakiwa ameoa mdogo wa JK.....
 
Huyo Wage nae ni fisadi no 1 ameiba pesa nyingi sana kwenye miradi ya bagamoyo kupitia dada yake Kombani..acha iishe kesi ya Jerry ije yake tunaisubiria kwa hamu sana ingawa nasikia mmoja walioshitakiwa ameoa mdogo wa JK.....

DUh Bongo zaidi ya uijuavyo tehetehe
 
Inasemekana Jamaa awana ushaidi wa kutosha wanatafuta jinsi ya kumaliza mambo

Sio kwamba hakuna ushaidhi wa kutosha

Ni sawa kumshtaki mtu aliyekuuzia cheni ya dhahabu feki wakati na wewe unajua ulimpa pesa bandia. teh teh teh

Si jeery Muro wala hao wengine wote ni wasanii tu.

sitashangaa kesi Jeery muro akifungwa miaka kdhaa then akapata msamaha. Nyuma ya pazia lazima wanaongea ili wayamalize kimjini mjini
 
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: contentheading, width: 100%"]Hukumu kesi ya Muro kusomwa leo
[/TD]
[TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: createdate"] Tuesday, 29 November 2011 20:32 [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD] 0digg

Nora Damian
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, leo inatarajia kutoa hukumu dhidi ya kesi ya kula njama na kuomba rushwa ya Sh10 milioni inayomkabili aliyekuwa Mtangazaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Jerry Muro na wenzake wawili.

Hatua hiyo itatekelezwa baada ya pande zote mbili kumaliza kuwasilisha hoja zao kwa maandishi kuhusiana na washtakiwa hao kama wana kesi ya kujibu au la.

Upande wa utetezi kupitia kwa wakili Richard Rweyongeza, uliwasilisha hoja zake mahakamani hapo na kutaka washtakiwa hao waachiwe huru kwa madai kuwa hawana kesi ya kujibu.

Rweyongeza alidai kuwa maelezo ya namna washtakiwa hao walivyokamatwa yana mkanganyiko na yanatofautiana.Alidai kuwa hata maelezo ya shahidi wa tatu Michael Wage ni kama hadithi na kwamba hakuna ushahidi unaoonyesha kwamba Januari 29, Wage na Muro walikuwa kwenye gari moja.

Alidai kuwa dereva wa Wage alikuwa shahidi muhimu katika kesi hiyo na angeweza kuisaidia mahakama lakini wanashangaa kwa nini hakuitwa.

Kwa upande wa Jamhuri kupitia kwa Mkurugenzi Msaidizi katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka, Boniface Stanslaus naye aliwasilisha hoja zake mahakamani hapo akitaka washtakiwa wote watiwe hatiani.

Alidai kuwa ushahidi wa upande wa mashtaka na utetezi wa washtakiwa hao umethibitisha kuwa washtakiwa walitenda makosa ya kula njama, kuomba rushwa na kujifanya ni watumishi wa Serikali.

Mbali ya Muro, washtakiwa wengine katika kesi hiyo Edmund Kapama na Deograthias Mgasa.
Washtakiwa hao wanakabiliwa na makosa ya kula njama, kuomba rushwa na kujifanya maofisa wa Serikali ambapo wanadaiwa kumuomba rushwa ya Sh10 milioni aliyekuwa Mhasibu wa Halmashauri ya Bagamoyo, Michael Wage.

Wanadaiwa kuomba fedha hizo ili wasitangaze tuhuma za ufisadi zilizokuwa zinamkabili Wage katika kipindi cha Usiku wa Habari kinachorushwa na TBC.

[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

 
Jerry Muro kaachiwa ni huru sasa............................................
 
Back
Top Bottom