Toto confusion, toto distruction. Waandishi wetu bana!! hata hiyo habari yenyewe kwenye Mwananchi haieleweki vizuri iwapo hiyo kesi ya Utapeli imefutwa au imeairishwa...haieleweki iwapo mwandishi amechanganya madesa katika kuripoti au lah hitimisho lakie lina utata....Hawa watu waandishi tabu tupu!
..........................
Mahakama yamfutia Muro kesi ya utapeli
Send to a friend Friday, 09 July 2010 20:58 0diggsdigg
Ummy Muya
Jerry Muro
KESI inayomkabili mtangazaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC1), Jerry Muro jana imefutwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinodoni baada ya mlalamikaji kuamua kumsamehe.
Mlalamikaji katika shauri hilo, alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Boneste General Enterprisess Ltd, Eduado Chamuhene ambaye alimshtaki katika mahakama hiyo, baada ya kutomalizia kumlipa fedha alizomkopa.
Wakati hakimu akijianda kuendelea na kesi hiyo, mlalamikaji alinyoosha mkono na kuomba kuliondoa shauri hilo, mahakamani hapo.
Mheshimiwa huyu kijana ni kama mtoto wangu ninamuonea huruma nimeamua kumsamehe, naomba uridhie uamuzi wangu,alisema Chamuhene. Hakimu Fimbo aliridhia ombo hilo, na kulifuta shauri hilo.
Katika shauri hilo, ilidaiwa na mlalamikaji mbele ya Hakimu Sundi Fimbo kuwa Februari 26 mwaka 2008, Jerry akiwa mfanyakazi wa ITV alifika nyumbani kwake eneo la Mabibo sahara akiwa na msichana mmoja aliyemtambulisha kama mke wake akimuomba amkopeshe Sh 1.5 milioni akatoe gari lake bandarini.
Chamuhene alisema alimpatia Jerry hundi ya Sh 1.5 milioni na kukubaliana kurudisha fedha hizo baada ya siku 60, lakini Jerry badala ya kukamilisha deni hilo, alilipa Sh milioni moja na kiasi kilichobaki hakukilipa.
Aliieleza mahakama kuwa baada ya muda kupita aliamua kumuandikia barua na kumpelekea ofisini kwake wakati huo,akiwa ITV na ilisainiwa katika kitabu maalum cha kupokeea barua, lakini hakutoa sababu yeyote na hakufanya mawasiliano ya aina yeyote.
Kabla Hakimu hajaahirisha shauri hilo, mshtakiwa ambaye aliwasili mahakamani hapo na kumuomba Hakimu ampatie muongozo wa kesi kutokana na yeye kutofahamu taratibu za mahakama ili mpatie wakili wake.
Mahakama yamfutia Muro kesi ya utapeli