I got to know, kwa hiyo jamaa alikuwa ana kesi mbili??!! Na mwananchi nao, wameiandikaje hii habari wakati wanajua sisi hatuijui hiyo kesi nyingine?
Wanataka kuuza magazeti, si unajua tena njaa kitu kibaya?
kumbe mshikaji utapeli ni fani yake..................
njaa kwake tumboni ikishavamia kichwani ni hatali tupu, mwanaume anaweza kuwa shoga, mwandishi akawa mwongo, nkNdio tatizo la magazeti, yaani hawana mbinu nyingine ya kuuza magazeti yao zaidi ya hii ya kuwazuga watu kwa kichwa cha habari kingine.
Ha ha ha ha, hata mimi nashangaa. Sikujua kabisa kama alikuwa ana kesi mbili mahakamani. Napata shaka kwamba huyu bwana si mwaminifu kama ambavyo wengi wetu tumekuwa tukimdhania.
kumbe mshikaji utapeli ni fani yake..................
Kumbe ile Kesi ya Kova ya utapeli/rushwa ya 10m/- pamoja na mambo ya kumiliki pingu bado iko palepale?
Toto confusion, toto distruction. Waandishi wetu bana!! hata hiyo habari yenyewe kwenye Mwananchi haieleweki vizuri iwapo hiyo kesi ya Utapeli imefutwa au imeairishwa...haieleweki iwapo mwandishi amechanganya madesa katika kuripoti au lah hitimisho lakie lina utata....Hawa watu waandishi tabu tupu!
..........................
Mahakama yamfutia Muro kesi ya utapeli
Send to a friend Friday, 09 July 2010 20:58 0diggsdigg
Ummy Muya
Jerry Muro
KESI inayomkabili mtangazaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC1), Jerry Muro jana imefutwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinodoni baada ya mlalamikaji kuamua kumsamehe.
Mlalamikaji katika shauri hilo, alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Boneste General Enterprisess Ltd, Eduado Chamuhene ambaye alimshtaki katika mahakama hiyo, baada ya kutomalizia kumlipa fedha alizomkopa.
Wakati hakimu akijianda kuendelea na kesi hiyo, mlalamikaji alinyoosha mkono na kuomba kuliondoa shauri hilo, mahakamani hapo.
Mheshimiwa huyu kijana ni kama mtoto wangu ninamuonea huruma nimeamua kumsamehe, naomba uridhie uamuzi wangu,alisema Chamuhene. Hakimu Fimbo aliridhia ombo hilo, na kulifuta shauri hilo.
Katika shauri hilo, ilidaiwa na mlalamikaji mbele ya Hakimu Sundi Fimbo kuwa Februari 26 mwaka 2008, Jerry akiwa mfanyakazi wa ITV alifika nyumbani kwake eneo la Mabibo sahara akiwa na msichana mmoja aliyemtambulisha kama mke wake akimuomba amkopeshe Sh 1.5 milioni akatoe gari lake bandarini.
Chamuhene alisema alimpatia Jerry hundi ya Sh 1.5 milioni na kukubaliana kurudisha fedha hizo baada ya siku 60, lakini Jerry badala ya kukamilisha deni hilo, alilipa Sh milioni moja na kiasi kilichobaki hakukilipa.
Aliieleza mahakama kuwa baada ya muda kupita aliamua kumuandikia barua na kumpelekea ofisini kwake wakati huo,akiwa ITV na ilisainiwa katika kitabu maalum cha kupokeea barua, lakini hakutoa sababu yeyote na hakufanya mawasiliano ya aina yeyote.
Kabla Hakimu hajaahirisha shauri hilo, mshtakiwa ambaye aliwasili mahakamani hapo na kumuomba Hakimu ampatie muongozo wa kesi kutokana na yeye kutofahamu taratibu za mahakama ili mpatie wakili wake.
Mahakama yamfutia Muro kesi ya utapeli
kumbe kesi tofauti na hile iliotikisa jiji.walikuwa wana tania walivyo mkamata.
Katika hilo Wage alieleza kuwa alikubaliana na ombi hilo na Januari 29 mwaka jana, saa tano asubuhi alifikia katika mgahawa wa Califonia ulioko jijini hapa akiwa na dereva wake.
Alisema akiwa njiani alimpigia simu Murro ili aje aungane naye na baada ya dakika chache Murro aliwasili katika mgahawa huo akiwa na gari ndogo na akamweleza watafute meza nyingine ili wakae mbali na dereva wake na walipohamia kwenye meza nyingine ndipo Murro alipoanza kumueleza tuhuma za ufisadi zinazomkabili na kwamba anataka kuzitangaza kwenye kipindi cha Usiku wa Habari kinachorushwa na TBC1.
"Baada ya Murro kunieleza tuhuma hizo akaniambia mahojiano kamili yangefanyika katika Hoteli ya Sea Cliff kwani huko ndiko walikokuwa mabosi wake na kunitaka nimwache dereva wangu kwenye mgahawa huo nikapande gari lake twende nae Sea Cliff na nilifanya kama alivyonielekeza nikapanda na tulipokuwa njiani akampigia simu mtu akawa anazungumza naye na akanitaja jina langu… alivyokata simu nikamuuliza ni kwa nini alikuwa akitaja jina langu akasema alikuwa akizungumza na Kaimu Mkurugenzi wa PCCB (Kapama) naye pia atanihoji.
"Kitu kingine wakati nilipokuwa ndani ya gari hilo tukielekea Sea Cliff, Murro aliniambia yeye ni ofisa wa jeshi na ana nyota tatu na amechukua mafunzo nchini Marekani na Afrika Kusini na ana madaraka ya kunikamata… na baada ya hapo alifungua dashibodi ya gari lake akatoa pingu akaniambia nikimletea vurugu atanifunga na pingu na kisha akanionyeshea bastola pia akaniambia nikifanya vurugu atanifyatulia risasi ili kunidhibiti," alieleza.