sajo
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 3,474
- 6,195
Wakili wa kujitegemea mkoani Iringa, Geofrey Mwakasege amefungua kesi ya Kikatiba katika Mahakama Kuu ya Tanzania (kanda ya Iringa) akitaka mahakama hiyo itamke kuwa mawakili wa kujitegemea wana haki ya kutangaza huduma za kisheria kwa umma kama zilivyo biashara nyingine. Katika kesi hiyo namba 23 ya 2021, amemshtaki Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) pamoja na Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS).
Wakili Geofrey anaitaka Mahakama hiyo kutamka kuwa Kanuni ya 127 (2) (a, b, c), (3) na (4) ya Kanuni za Maadili ya Kitaaluma kwa Mawakili za Mwaka 2018, inayowazuia kujitangaza kibiashara inakinzana na Katiba ya JMT (Ibara ya 13 na ya 22(1)). Msikilize na kumtazama hapa
Hivyo anaitaka Mahakama hiyo itamke kuwa kazi za taaluma ya sheria ni biashara kama zilivyo biashara nyingine kwa kuwa inalipiwa kodi na mawakili wanalazimishwa kuwa na mashine za EFD na hivyo inastahili haki zote zinazofurahiwa na biashara nyingine, ikiwa ni pamoja na uhuru wa matangazo. Mbadala, ameitaka mahakama kutamka kuwa kazi za taaluma ya sheria ni Huduma na hivyo ziondolewe mizigo ya kibiashara kama vile kulipa kodi na leseni za biashara ili ziwe sawa na Mahakama ambayo inatoa huduma za kisheria bila kulipa kodi.
Kesi hiyo inaenda kusikilizwa leo tarehe 04 Oktoba 2021 mbele ya Jaji Utamwa. Awali kesi hiyo ilipangwa kusikilizwa tarehe 21 Oktoba 2021.
Chanzo: Mwananchi (29.09.2021) na The Citizen (28.09.2021)
UPDATES:
Kesi haijasikilizwa bali imeahirishwa na kaimu naibu Msajili wa Mahakama Kuu mpaka Tarehe 21 Oktoba 2021 itakapokuja kwa ajili ya kusikilizwa. Imeahirishwa kwa sababu Jaji Utamwa aliyepaswa kusikiliza kesi yupo Mkoani Mbeya anakoendelea na vikao (session) vya Mahakama Kuu vitakavyochukua siku 14 kutoka leo.