GE2025 Kesi ya Kikatiba dhidi ya Tume huru ya Uchaguzi (INEC) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuendelea leo Septemba 3,2025

GE2025 Kesi ya Kikatiba dhidi ya Tume huru ya Uchaguzi (INEC) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuendelea leo Septemba 3,2025

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
Chama cha siasa cha ACT Wazalendo kimetangaza kuwa kesi ya kikatiba iliyofunguliwa dhidi ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi na Mwanasheria Mkuu wa Serikali itaendelea kusikilizwa leo, tarehe 3 Septemba 2025, katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dodoma.Kesi hiyo, namba 21692 ya mwaka 2025, imefunguliwa na Bodi ya Wadhamini wa ACT Wazalendo pamoja na mgombea wao wa urais, Luhaga Joelson Mpina. Kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa na chama, kesi hiyo ilifunguliwa kwa hati ya dharura tarehe 27 Agosti 2025 na itasikilizwa mbele ya jopo la majaji watatu: Jaji Evaristo Longopa, Jaji John Kahyoza, na Jaji Abdi Kagomba.

ACT Wazalendo inaiomba Mahakama itoe amri muhimu dhidi ya kile wanachodai kuwa ni uamuzi batili wa Tume ya Uchaguzi kumuengua Mpina katika kinyang'anyiro cha Urais, Chama hicho kimesisitiza kuwa hatua ya Tume imekiuka Katiba na Sheria za nchi.Kesi hiyo itasikilizwa kwa njia ya Mtandao, na ACT Wazalendo imekaribisha Wanachama wake, Waandishi wa Habari, na Wadau wote wa haki na demokrasia kushiriki kwa njia hiyo. Katika taarifa yake, Naibu Katibu wa Idara ya Habari, Uenezi na Uhusiano na Umma wa ACT Wazalendo, Shangwe Ayo, amesema:"Tunasisitiza kwamba hatutachoka na hatupaswi kuchoka katika mapambano ya kuikomboa nchi yetu. Hila na hujuma za serikali na vyombo vyake vya dola dhidi ya wapenda haki hazitaturudisha nyuma. Tutaendelea kupambana na tutashinda!"

Soma Pia:
1756881527771.jpeg
 
Back
Top Bottom