Kuna ndugu alikamatwa akiwa kwenye shughuli zake za kupasua Kuni kwenye mito mara nyingi huwa ni mtu wa kupasua kokoto mtoni au anapasua kuni anaenda kuuzia mama ntilie Pale Rau Madukani Moshi..
Sasa kuna siku alipeleka mzigo wakuni kuuza alipo toka kuuza akapitia shoka lake mahali anapo liwekaga akawa anarudi nalo mtoni kwenye kupasua nyingine .Akiwa njian aka kamatwa na police akafungwa pingu akarushwa kwenye gari ya polisi ndani ya gari hiyo akakuta kuna vijana wengine wa5, wote wakapelekwa Polisi central pale moshi mjini.. Akaomba simu yake ili apigie ndugu zake akanipigia mimi akaniambia Mdogo wangu nimekamatwa Niko police mpaka sasa sijaambiwa kosa langu ila nadhani ni mambo ya kuni hawa jamaa wako kwenye operation za kuzui uharibifu wa vyanzo vya maji.. Na mm nika mwambia serikali ina zuia shughuli kwenyw vyanzo vya maji.. Basi kwa kuwa mm niko dar nikapigia ndugu wa pale moshi ili wafuatilie..
Kulipokucha Dada yangu akapeleka chakula.. lakini pia akauliza kuhusu kosa la kak yake, Chaajabu shtaka likawa lingine kabisa.. akaambiwa ndugu yako amepiga mtu yule mtu akawa kajeruiwa alipo pelekwa hospital akafia uko kwenye matibabu.. hivyo anakesi ya Mauwaji.
Nilipopewa hii taarifa nilishangaa sana.. sasa ndugu wengine walipoenda kuomb kuongea naye hawaruhusiwi na aliyepewa nafasi ya kuongea naye tena kupitia tundu la ufunguo wa mlango wa sero.. Kaka aka mwabia mama yake mkasa mzima kuwa yeye alotoka kuuza kuni wakati anarudi aka kamatwa anashanga kuambiwa ame mzuru mtu maana hana uhasama na mtu wala hajawahi gombana na mtu.
Sasa ninacho omba ushuri nikuwa ndugu yangu yuko kituoni tagu tarehe 13 mpaka leo na nasikia wale wenziwe ndugu zao walienda waka watoa sasa tunashangaa ndugu yetu hatoki na kama nikosa hilo wanalosema amefanya Mpelelezi alisema walikuwa wa5 sasa ka mganda kaka yangu tu na ajabu bro anshangaa hiyo issue ya kujerui imetoka wapi..
Je kisheria hapa huu uonevu wa kubambikiana makosa uta tatulikaje Huyu mtunatoke maana hapo kituon naambiwa wana lala kwenye maji, watu wanaugua kuna vijan watatu wamezidiwa kwa mazingira machafu.. mbaya zaidi huduma ya kupeleka chakula kila siku ili hali mihususika anayepeleka chakul naye kachoka anataka kusafiri anshindwa .
Je hata kisheria anasaidiwaje??