Kesi ya Kubambikiwa Moshi Central Police

Kesi ya Kubambikiwa Moshi Central Police

Jojo123

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2013
Posts
432
Reaction score
703
Unyama huu nita andika Barua Kwa IGP nielezee kila kinacho endelea hapo Police na kila wanacho taka ili kumtoa mtu ambaye hausiki na kesi ana tesekea tu Central police..
 
Katoe pesa rushwa POLISI ili nduguyo atoke...au tafuta mwanasheria utoe pesa umlipe muende mahakamani na danadana za upelelezi na kuahirisha kesi na akifanikiwa atatoka ila baada ya kitambo kirefu hivi na HAKUNA FIDIA...
 
Hawa polisi wahuni dawa yao alikuwa Magufuli tu.
 
Mtapata cha mtema kuni hadi pale wote tutakapokubali kuwa tupo Misri na tukubali wote kwa Pamoja kudai nchi yetu ya ahadi.

Suala la kudai haki katika nchi hii halipaswi kuwa ni suala la Chadema au chama chochote cha upinzani bali linapaswa kuwa ni suala la kila mtu.

Unapoona watu wengine wanavunjiwa haki zao kisha ukakaa pembeni jua zamu yako inakuja.Hakuna alie salama.Watu watakuwa salama pale ambapo kila mtu atakuwa salama.
 
Kuna ndugu alikamatwa akiwa kwenye shughuli zake za kupasua Kuni kwenye mito mara nyingi huwa ni mtu wa kupasua kokoto mtoni au anapasua kuni anaenda kuuzia mama ntilie Pale Rau Madukani Moshi..

Sasa kuna siku alipeleka mzigo wakuni kuuza alipo toka kuuza akapitia shoka lake mahali anapo liwekaga akawa anarudi nalo mtoni kwenye kupasua nyingine .Akiwa njian aka kamatwa na police akafungwa pingu akarushwa kwenye gari ya polisi ndani ya gari hiyo akakuta kuna vijana wengine wa5, wote wakapelekwa Polisi central pale moshi mjini.. Akaomba simu yake ili apigie ndugu zake akanipigia mimi akaniambia Mdogo wangu nimekamatwa Niko police mpaka sasa sijaambiwa kosa langu ila nadhani ni mambo ya kuni hawa jamaa wako kwenye operation za kuzui uharibifu wa vyanzo vya maji.. Na mm nika mwambia serikali ina zuia shughuli kwenyw vyanzo vya maji.. Basi kwa kuwa mm niko dar nikapigia ndugu wa pale moshi ili wafuatilie..

Kulipokucha Dada yangu akapeleka chakula.. lakini pia akauliza kuhusu kosa la kak yake, Chaajabu shtaka likawa lingine kabisa.. akaambiwa ndugu yako amepiga mtu yule mtu akawa kajeruiwa alipo pelekwa hospital akafia uko kwenye matibabu.. hivyo anakesi ya Mauwaji.

Nilipopewa hii taarifa nilishangaa sana.. sasa ndugu wengine walipoenda kuomb kuongea naye hawaruhusiwi na aliyepewa nafasi ya kuongea naye tena kupitia tundu la ufunguo wa mlango wa sero.. Kaka aka mwabia mama yake mkasa mzima kuwa yeye alotoka kuuza kuni wakati anarudi aka kamatwa anashanga kuambiwa ame mzuru mtu maana hana uhasama na mtu wala hajawahi gombana na mtu.

Sasa ninacho omba ushuri nikuwa ndugu yangu yuko kituoni tagu tarehe 13 mpaka leo na nasikia wale wenziwe ndugu zao walienda waka watoa sasa tunashangaa ndugu yetu hatoki na kama nikosa hilo wanalosema amefanya Mpelelezi alisema walikuwa wa5 sasa ka mganda kaka yangu tu na ajabu bro anshangaa hiyo issue ya kujerui imetoka wapi..

Je kisheria hapa huu uonevu wa kubambikiana makosa uta tatulikaje Huyu mtunatoke maana hapo kituon naambiwa wana lala kwenye maji, watu wanaugua kuna vijan watatu wamezidiwa kwa mazingira machafu.. mbaya zaidi huduma ya kupeleka chakula kila siku ili hali mihususika anayepeleka chakul naye kachoka anataka kusafiri anshindwa .

Je hata kisheria anasaidiwaje??
IGP alikuwa Kilimanjaro last week, Akiwa kwenye masafara wake kuna eneo lenye Kona kali, mteremko na daraja kubwa ( daraja la kikavu) huko Kilimanjaro gari lake Lilinusurika kugongwa baada ya msafara kuovateki eneo la hatari na ambapo huwa kuna Ajali nyingi.

Ninashauri misafara ya viongozi izingatie alama Za barabarani vinginevyo tutazika viongozi wengi kwa sababu ya Ajali Za kizembe kwenye maeneo ya hatari.

Ni jambo la ajabu na la hatari kwa msafara wa IGP kutokuzingatia sheria za usalama barabarani.

IGP umesikia kilio cha Huyo mtanzania .
 
Back
Top Bottom