Kesi ya kugombea mirathi ya mwandishi wa habari mkongwe nchini, Betty Luzuka yaibua mapya Arusha

Kesi ya kugombea mirathi ya mwandishi wa habari mkongwe nchini, Betty Luzuka yaibua mapya Arusha

buswelu moja

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2014
Posts
226
Reaction score
180
KESI ya kugombea mirathi ya mwandishi wa habari mkongwe nchini marehemu Betty Luzuka imeibua mapya mahakamani mara baada ya ushahidi wa njia ya video kumuonyesha mke wa aliyekuwa ofisa mwandamizi wa jumuiya ya Afrika Mashariki ,Phil Makini Kleruu aitwaye Hilda Kleruu akichukua fedha za marehemu kabla na baada ya marehemu kuaga dunia.

Hilda, ambaye amefunguliwa kesi na kaka wa marehemu, Ssarongo Luzuka akimtuhumu kujimilikisha mali za marehemu bila kufuata utaratibu wa kifamilia na kimahakama mara baada ya marehemu kuaga dunia Agosti mwaka 2013 katika hospitali ya Shreee Hindu ya jijini Arusha baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Kesi hiyo ya mirathi inayovuta hisia za watu mbalimbali jijini Arusha ipo katika mahakama ya mwanzo ya Maromboso yenye nambari 222 ya mwaka 2013 inaitaka mahakama hiyo ipitie hukumu yake iliyotolewa Septemba 27 mwaka 2013 na hakimu Prince Gideon iliyompa ushindi kaka wa marehemu.

Hatahivyo,upande wa mdaiwa umepinga hatua hiyo kwa kutokuridhishwa na hukumu hiyo kutokana na kudai kuwa ana wosia halali alioachiwa na marehemu uliomilikisha mali zake zote ambazo ni nyumba tatu zilizopo maeneo ya Njiro,Olmatejoo na Pemba road,mamilioni ya fedha zilizopo katika akaunti mbalimbali pamoja na shamba lenye ukubwa wa zaidi ya ekari 3 lililopo eneo la Mkonoo mkoani Arusha .

Katika kesi hiyo iliyopo mbele ya hakimu wa mahakama hiyo,Moka Mashaga upande wa wadai wanaitaka mahakama kutupilia mbali wosia uliowasilishwa na mdaiwa kwa kuwa ni batili,umepikwa na kwamba sahihi ya marehemu imeghushiwa.

Ushahidi uliotolewa mahakamani hapo wiki iliyopita kwa njia ya video na upande wa mdai katika kesi hiyo aliiambia mahakama kuwa mdaiwa (Hilda) alikuwa akitoa fedha kwa nyakati tofauti katika benki ya CRDB tawi la Mapato jijini Arusha kwenye akaunti ya marehemu huku akitambua kuwa siyo msimamizi halali wa mali za marehemu hali ambayo iliwalazimu wao kufika polisi kutoa taarifa na hatimaye akaunti hizo kuzuiwa hadi kesi hiyo itakapomalizika.

Ssarongo, aliiambia mahakama hiyo kwamba yeye na dada yake Jully Luzuka ndiyo waliochaguliwa na familia kuwa wasimamizi wa mali za marehemu kupitia kikao cha familia kilichofanyika Septemba 27 mwaka 2013 na kisha baadaye kuthibitishwa na mahakama bila shaka na wakati hayo yakifanyika hakuna mtu yoyote aliyejitokeza kuonyesha ameachiwa wosia na marehemu.

Huku akijiamini Ssarongo aliiambia mahakama hiyo kwamba mdaiwa alichukua jumla ya kiasi cha sh,milioni 8 kupitia akaunti ya marehemu kwa nyakati tofauti ikiwemo siku ambayo marehemu aliaga dunia ambayo ni Agosti 8 mwaka 2013 ambapo kwa mujibu wa taarifa walizopatiwa na benki ya CRDB zinaonyesha siku hiyo alichukua jumla ya kiasi cha sh,milioni moja.

"Tulikuwa tukijiuliza maswali mengi je kuna hela za marehemu zimeanza kutoka?je kadi zake za benki ziko wapi ,tulihoji hizi laki nne mara laki mbili mara milioni moja kupitia simu yake ya mkononi zinatoka wapi? tukasema hii hapana ndipo tukaenda benki na polisi kuwajulisha kuomba waiblock(waizuie)"Ssarongo aliiambia mahakama hiyo

Hatahivyo,Ssarongo alienda mbali zaidi na kuiambia mahakama hiyo kwamba walishangaa marehemu dada yao baada ya kufariki ,Hilda Kleruu pamoja na mmewe Kleruu ghafla walijichagua kuwa wasimamizi wa mazishi ya marehemu dada yao bila kuwashirikisha ndugu ambapo Hilda alishika nafasi ya mweka hazina huku mmewe ambaye aliwahi kuwa mtumishi katika jumuiya ya Afrika Mashariki akishika nafasi ya mwenyekiti wa kamati ya mazishi.

Hatahivyo,shahidi mwingine katika kesi hiyo ambaye ni dada wa marehemu,Jully Luzuka yeye alijikuta akiangua kilio mahakamani hapo wakati akitoa ushahidi ambapo mbali na kuiomba mahakama hiyo iwatendee haki pia alisema kuwa katika kipindi chote alichougua marehemu hakuwahi kujulishwa na mdaiwa kwamba marehemu ni mgonjwa mahututi pamoja kwamba alikuwa akimuuguza nyumbani kwake.

Naye,shahidi mwingine ambaye ni mdogo wa marehemu,Theresa Charlote yeye aliiambia mahakama kwamba anakumbuka wakati wa kuanua matanga katika kikao cha familia hakuna mtu yoyote aliyejitokeza kusema kwamba ameachiwa wosia na marehemu pamoja na tamko la kumtaka mtu yoyote aliyeachiwa wosia huo kujitokeza.

"Nakumbuka wakati wa kuanua matanga kaka Ssarongo aliuliza je kuna mtu yoyote ameachiwa wosia na marehemu lakini hakuna hata mmoja aliyejitokeza kusema ana wosia huo"Charlote aliiambia mahakama hiyo.

Mara baada ya mahakama hiyo kusikiliza ushahidi huo hakimu anayesikiliza kesi hiyo aliamua kuihairisha hadi Julai 6 mwaka huu ambapo mashahidi wanne kutoka upande wa wadai watafika mahakama hapo kutoa ushahidi wao kabla ya mahakama hiyo kupanga tarehe ya hukumu.

Mwisho.

(pichani chini ni mwandishi wa habari mwandamizi nchini ambaye pia aliwahi kufanya kazi katika kituo cha mikutano cha kimataifa cha AICC mkoani Arusha marehemu,Betty Luzuka)
 

Attachments

  • B.JPG
    B.JPG
    23.2 KB · Views: 693
  • B2.JPG
    B2.JPG
    10.4 KB · Views: 712
Likitokea la kutoke hapo,
Utasikia kwamba Eti alikuwa na habari nzito ya uchunguzi ambayo ingefanya mabadiliko katika taifa hili,hahahah

Haya waje na hapo sasa wamsaidie Mwandishi mwenzao,sio wasuburi hadi matokeo ili wazue
 
Dar huyu mama kumbe alishafariki? Namkumbuka enzi hizo hapo AICC alikuwa mrefu smart sana nilikuwa navutiwa nae alikuwa mtaratiiibu mpaka nikajisemea na mimi nikianza kazi nitakuwa kama yeye, alikuwa hana makundi wala papara very cool, ana smile kichizi, enzi hizo nasoma tuition looh. R.I.P mama.
 
KESI YA KUGOMBEA MIRATHI YA MWANDISHI WA HABARI YAENDELEA.

Kesi ya kugombea mirathi ya mwandishi wa habari mkongwe nchini marehemu,Betty Luzuka juzi imeendelea katika mahakama ya mwanzo ya Maromboso ambapo shahidi mwingine katika kesi hiyo Michoro Christopher alitoa ushahidi wake mbele ya mahakama hiyo.

Kesi hiyo ya mirathi inayovuta hisia za watu mbalimbali jijini Arusha ipo katika mahakama ya mwanzo ya Maromboso yenye nambari 222 ya mwaka 2013 inaitaka mahakama hiyo ipitie hukumu yake iliyotolewa Septemba 27 mwaka 2013 na hakimu Prince Gideon iliyompa ushindi kaka wa marehemu.

Kaka wa marehemu aitwaye, Ssarongo Luzuka alifungua kesi hiyo akimtuhumu mke wa aliyekuwa ofisa mwandamizi wa jumuiya ya Afrika Mashariki ,Phil Makini Kleruu aitwaye Hilda kujimilikisha mali za marehemu bila kufuata utaratibu wa kifamilia na kimahakama mara baada ya marehemu kuaga dunia Agosti mwaka 2013 katika hospitali ya Shreee Hindu ya jijini Arusha baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Hatahivyo,upande wa mdaiwa umepinga kutokuridhishwa na hukumu hiyo kutokana na madai kuwa ana wosia halali alioachiwa na marehemu uliomilikisha mali zake zote ambazo ni nyumba tatu zilizopo maeneo ya Njiro,Olmatejoo na Pemba road,mamilioni ya fedha zilizopo katika akaunti mbalimbali pamoja na shamba lenye ukubwa wa zaidi ya ekari 3 lililopo eneo la Mkonoo mkoani Arusha .

Shahidi huyo aliieleza Mahakama hiyo kuwa mbali na kufamahamiana na marehemu tangu mwaka 2003 pia alikuwa rafiki wa karibu ambapo alikuwa akitunza funguo za nyumba za marehemu iliyopo maeneo ya Pemba road jijini Arusha.

Shahidi huyo aliiambia mahakama ya kwamba siku marehemu amefariki dunia katika hospitali ya mkoa ya Shree Hindu daktari wa hospitali hiyo alimwambia akatafute shuka nyeupe kwa ajili ya kumfunika marehemu ambapo alifika nyumbani kwa marehemu na kufungua chumba chake lakini cha ajabu alikuta chumba hicho kimevurugwa.

Martin,mbele ya hakimu anayesikiliza kesi hiyo,Moka Mashaga alisema kuwa mbali na kushuhudia chumba hicho kuvurugika pia alikuta funguo za kabati la nguo za marehemu zimeshamishwa mahala zinapokuwa jambo ambalo si la kawaida.

Alisema kuwa mara baada ya kufungua kabati la nguo za marehemu kwa lengo la kutoa shuka hilo alikuta begi la marehemu lililokuwa linahifadhi vyeti vyake vya shule,mikataba ya nyumba,hati za nyumba pamoja na fedha mbalimbali halionekani na ndipo alipoingiwa na mashaka na kuhisi huenda limeibiwa.

Shahidi huyo alienda mbali zaidi na kusema kuwa mara baada ya kufanikiwa kupata shuka la kumfunika marehemu ndipo alipomtafuta kaka wa marehemu,Ssarongo na kumweleza kuhusu tukio hilo ambapo alipojibiwa kuwa suala hilo litazungumziwa katika kikao cha familia.

Hatahivyo,shahidi huyo aliiambia mahakama hiyo kwamba mbali na tukio hilo pia aliwahi kushuhudia siku marehemu akiwa nyumbani enzi za uhai wake akipokea kadi mbili za pongezi kwa siku yake ya kuzaliwa kutoka kwa familia ya Kleruu na mkewe.

Shahidi huyo alisema kuwa katika kadi mojawapo mke wa ofisa huyo(Hilda) aliandika ujumbe wa kuomba kukopeshwa na marehemu kiasi cha sh,milioni 4 na kwamba atazirudisha ikibidi anaweza kufika nyumbani kwa ajili ya kuandikishiana jambo ambalo marehemu hakulitekeleza.

Mara baada ya kusikiliza ushahidi huo hakimu anayesikiliza kesi hiyo aliamua kuihairisha hadi mnamo Julai 13 mwaka huu ambapo ataita pande mbili katika kesi hiyo kuja kukamilisha ushahidi wao kabla kupanga tarehe ya hukumu.

(pichani chini ni mwandishi wa habari mkongwe nchini,marehemu Betty Luzuka ambaye pia aliwahi kuwa mtumishi wa kituo cha mikutano cha kimtaifa(AICC) Arusha.

Mwisho.
 

Attachments

  • betty 1.JPG
    betty 1.JPG
    23.5 KB · Views: 708
  • betty 2.JPG
    betty 2.JPG
    10.4 KB · Views: 692
Nilikuwa sifahamu Dada Betty amefariki!! Alkuwa kaokoka kweli, pamoja na uzee wake alikuwa always anaitwa Dada Betty..... She was also a member of FGBMF hata huyo aliechukua mirathi namfahanu ngoja nipate derails vizuri
 
Interesting nawafahamu sidhani ka da Betty alimuachia huyo Dada Mali, na sidhani pia kama alitaka kaka yake achukue Mali zake
 
Wadau wa JF, ile kesi ya kugombea mirathi ya mwandishi wa habari mkongwe nchini, Betty Luzuka inataraji kusikilizwa kesho katika mahakama ya mwanzo ya maromboso mbele ya hakimu,Moka Mashaga.

Kesi hiyo ya mirathi nambari 222 ya mwaka 2013 ilifunguliwa na kaka wa marehemu, Sarongo Luzuka ambaye hapo awali mahakama hiyo ilimpa ridhaa ya kuwa msimamizi wa mirathi ya marehemu betty lakini ombi hilo lilipingwa na mke wa aliyekuwa ofisa mwandamizi wa jumuiya ya afrika mashariki(EAC), Philip Kleruu aitwaye Hilda kleruu akidai kwamba marehemu alimwachia wosia uliommilikisha nyumba tatu, shamba lililoko mkonoo, na mamilioni ya fedha katika benki tofauti hapa nchini.

Kesi hii imevuta hisia kwa wakazi wa mji wa Arusha kutokana marehemu alikuwa mwandishi maarufu na baadaye kufanya kazi katika kituo cha mikutano cha kimataifa cha AICC hapa Arusha upande wa itifaki.

Kesho nikiwa mahakamani wadau wa JF nitawaletea updates zote pamoja na picha mbalimbali hivyo mkae karibu na jukwaa hili kwani kesho hakimu mashaga ameita kesi kwa ajili ya (cross examonation) kabla ya kupanga tarehe ya hukumu.

Mtakumbuka hapo awali shahidi wa mwisho, Michoro Christopher ambaye alikuwa rafiki wa marehemu wiki iliyopita alitoa ushahidi wake mbele ya mahakama hiyo ambapo alisema kuwa alimfahamu marehemu miaka kumi iliyopita na siku anafariki hospitalini daktari alimwambia ya kwamba akachukue shuka jeupe kwa ajili ya kumfunika marehemu na ndipo alipoenda nyumbani kwa marehemu na kumkuta msichana wa kazi ambaye alimpatia funguo za chumba cha marehemu na ghafla alipofungua chumba hicho alikuta kimevurugwa jambo lililomshtua.

Shahidi huyo wa mwisho katika kesi hiyo aliiambia mahakama kwamba mara alipofungua kabati la nguo za marehemu alikuta begi lililokuwa limehifadhi vyeti vya shule vya marehemu,mikataba ya nyumba,hatimiliki za nyumba mbalimbali na fedha halipo na kuhisi huenda msichana wa kazi au hilda kleruu wameliiba.

Ndugu wadau wa JF, kesho msikae mbali nitawaletea taarifa zote mahakamani.

Mwisho.
 
Interesting. Hebu tupe mkasa mzima
atuambie, huyo marehemu hakuacha watoto, na huyo anayetaka mali alipewa kwenye huo wosia kama nani? kama rafiki tu na watoto wapo au hawapo au alipewa kama nani. wakati mwingine wosia huwa unakuwepo na kutokana na ulivyoandikwa unafanywa kuwa batili kama haukufuata misingi sahihi ya uandishi wa wosia. na wapo mahakama ya mwanzo ambayo haipokei mawakili wa kujitegemea hivyo najua hapo primary magistrates mambulula ni kuangalia nani ana pesa. aanze mapema kujiandaa na kukata rufaa.
 
Ni kwamba marehemu hakuacha mme wala mtoto,huyo hilda kleruu ni binamu wa marehemu na mmewe kabila lake ni mchaga wa marangu,lakini siamini katika dhana ya ukabila kwani kuna wachaga wenye roho safi tu baadhi yao lkn.asanteni mwenye dukuduku au swali aulize nitamjibu kama swali lake linajibika.asanteni
 
Ndugu wadau wa JF tunaomba watu wenye taarifa kuhusu hawa watu wazimwage hapa hawa ni PHIL MAKIN KLERUU na mkewe HILDA KLERUU.

Katika kufuatilia kidogo kupitia google tumempata bwana Kleruu na kujua kwamba aliwahi kuwa mtumishi katika jumuiya ya afrika mashariki(EAC) iliyopo Arusha kabla ya kufukuzwa kazi kwa tuhuma za ufisadi .

Alikuwa na cheo cha Senior Officer for estate management east african court na alihusishwa na ufisadi wa wizi wa ujenzi wa vifaa katika jengo la makao makuu ya EAC.

Mke wake ana club eneo la Kisongo jijini Arusha ni shombeshombe fulani hivi.

Kwa sasa wanandoa hawa wanakabiliwa na kesi ya mirathi nambari 222 ya mwaka 2013 katika mahakama ya mwanzo ya maromboso kwa hakimu moka mashaga.

Jamani wenye data mtumwagie hapa please kwani kesi wanayokabiliwa nayo Arusha ya kugombea mirathi ya marehemu Betty Luzuka,ambaye aliwahi kuwa mwandishi wa habari mkongwe imekuwa gumzo na inavuta hisia.
 
Ndugu wadau wa jf tunaomba wenye cv au taarifa za hawa watu hapo juu wazimwage hapa jukwaani,kwani kesi wanayokabiliwa nayo ya kugombea mirathi ya marehemu betty luzuka ambaye aliwahi kuwa mwandishi wa habari imekuwa gumzo na kuvuta hisia arusha katika mahakama ya mwanzo ya maromboso,ipo chini ya hakimu,moka mashaga.

wenye data zimwageni hapa kwani huyu kleruu tumeambiwa aliwahi kufanya kazi EAC makao makuu Arusha kabla ya kufukuzwa kazi kwa tuhuma za ufisadi.
na mkewe anamiliki club eeneo la kisongo Arusha ni shombeshombe.
 
kwani will iloachwa inasemaje,je ni valid kisheria,lifestyle ya marehemu ilikuaje enzi za uhai wake?
 
na chanzo cha kifo chake ni nini tena iaije ikawa walimkolimba ili wapate mali hasa huyu Kleruu ndio nina wasiwasi nae sana
 
Mkuu Buswelu ,una uhusiano gani na hii kesi au upande wowote wa kesi hii?
 
Last edited by a moderator:
Phil Makini Kleruu ni supporter mkubwa wa CHADEMA Arusha. Anawafadhili Nadhani kwa kigezo cha Uchaga zaidi.
Alikula hela za ujenzi wa makao makuu ya EAC mpaka leo jengo hilo linavuja.
Alifukuzwa kazi EAC kwa kujimilikisha samani za ofisi ya bunge la Jumuiya.
Kifupi ni kwamba yuko tayari kufanya lolote apate pesa
 
na chanzo cha kifo chake ni nini tena iaije ikawa walimkolimba ili wapate mali hasa huyu Kleruu ndio nina wasiwasi nae sana

wosia ulioachwa bado una utata kwani kaka wa marehemu anasema ni feki,lkn mke wa kleruu anasema wosia huo ni real kabisa na umemmilikisha mali zote za marehemu kwani uliandikwa na kusainiwa na marehemu kabla ya kifo chake mbele ya wakili mwandamizi nchini,wilfred mirambo maarufu kama"chief mirambo" kwa wanaoishi arusha wanamjua.

kuhusu chanzo cha kifo kimetajwa ni msongo wa mawazo ila kuna utata kwani kaka wa marehemu ametaka mwili wa dada yake ufukuliwe na kufanyiwa uchunguzi kwani ana wasiwasi kwamba huenda aliuwawa,kwani muda wote mtu aliyekuwa akimuuguza ni hilda kleruu nyumbani kwake.

kuhusu maisha ya marehemu enzi za uhai wake ni,kwamba alikuwa mcha mungu ,anapenda kusaidia watu ,mkarimu,mcheshi,mtu anayejituma,sio mlevi na mpenda anasa,kwa wakazi wa arusha wanamkumbuka pale aicc jinsi alivyokuwa mcheshi.
 
Ze heby sina uhusiano wowote zaidi maslahi yangu kuangukia kwa marehemu kwani aliwahi kuwa mwandishi wa habari fani ambayo ninaisomea kwa sasa,pia ni kisa kilichonivutia sana hadi nimeona nifuatilie hadi mwisho.
 
Back
Top Bottom