Kesi ya Kumtesa Dk Ulimboka yapigwa kalenda

Kesi ya Kumtesa Dk Ulimboka yapigwa kalenda

omujubi

JF-Expert Member
Joined
Dec 6, 2011
Posts
4,326
Reaction score
2,506
Kesi inayomkabili raia wa Kenya, Joshua Mulundi (21) aliyekamatwa na polisi Dar es Salaam kwa tuhuma za kumteka na kufanya jaribio la kumuua Mwenyekiti wa Jumuia ya Madaktari Tanzania, Dr. Stephen Ulimboka imeahirishwa hadi Agosti 7, mwaka huu.
Wakili wa Serikali, Mwanaisha Komba alimweleza hakimu Mkazi, Agnes Mchome kuwa kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya kutajwa na kwamba, upelelezi haujakamilika.
…
…
Hata hivyo kulitokea utata wa jina, umri wake na makazi ya mtuhumiwa huyo; wakati hati ya mashitaka mahakamani inadai ni Joshua Mulundi (21), mkiazi wa Murang'a nchini Kenya, taarifa ya Polisi inadai anaitwa Joshua Muhindi (31), mkazi wa Namanga nchini Kenya.

My take:
Hivi ni kwa nini Watanzania tusifikie sehemu kiazi kikaitwa kiazi!!!??
 
Ni kweli mkuu, tuacheni dhaifu na aitwe dhaifu kwa maana kweli ni dhaifu. Ila naamini malipo yote ni hapahapa duniani. Waache wanaowatesa na wawatese kwa maana mda si mrefu nao watatezwa.
 
Hivi kweli waandishi wetu wa habari za uchunguzi wamekubali kuwalisha WATZ habari za uongo za Jambazi Kova kuhusu huyo mtu wao wanaomwita Mkenya?.Kwa nini Wahariri wa habari wasiombe fedha kutoka MCT na ofisi za kufanya investigative journalism kwenda nchini kenya kupata ukweli wa jambo ilo.Mbona ni rahisi sana hata kama uchunguzi utafanyika kwa awamu.Mfano kusafiri hadi kenya maeneo hayo ya Nyeri,Murang'a au Namanga.Kupata background ya criminalism ya huyo mkenya wa Kova toka Interpol au CID kENYA,mAHAKAMA NA PRISONS ZA KENYA.SHULE ZAKE ALIZOSOMA YAANI mSINGI,SEKONDARI AU MILITARY TRAININGS ZOZOTE.
 
Afande Sele ana kazi kubwa ya kuandaa Filamu nyingine; kwani hii haiuziki mitaani.


MIZAMBWA
NABII MTARAJIWA!!!
 
ubalizi wa kenya nao utoe kali je huyu ni mkenya kweli?nionavyo mie huyu si mkenya ila wametudanganya tu ili kupunguza hasira za wananchi
 
ubalizi wa kenya nao utoe kali je huyu ni mkenya kweli?nionavyo mie huyu si mkenya ila wametudanganya tu ili kupunguza hasira za wananchi
ndio mkuu, na ukishajua kuwa umedanganywa huwa unafanya nini au ndio hasira zinapungua?

Jana niliona magazeti ya Tanzania Daima na Mwana Halisi yamechapisha habari ambazo wanasema ziko mahakamani lakini kikubwa zinapingana kabisa na haya maelezo yaliyotolewa na polisi.
Ninachotegemea, leo jioni/usiku ni kuona Kamanda Kova either akipinga hizo habari au basi 'akiwashukuru' kama alivyofanya kwa Mch. Gwajima kwa kyusaidia kutoa taarifa ambazo zitasaidia upelezi wao. Au kabisa kuwapa onyo la kuandika habari zilizopo mahakamani.
Mbali na hapo itakuwa ni kupoteza muda muhimu na gharama ambavyo ni vitu muhimu sana kwa Watanzania kutokana na umasikini uliotamalaki hivi sasa

 
wauaje wenyewe wako nje na isitoshe wanalipwa mishahara kutumia kodi zetu sisi ambao ndio tunanyanyaswa
 
Huyo wanamuonea tu, walomtesa mbona wanajulikana na hawajakamatwa?
 
Wakili wa Serikali, Mwanaisha Komba alimweleza hakimu Mkazi, Agnes Mchome kuwa kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya kutajwa na kwamba, upelelezi haujakamilika.

Waseme usanii wa kumbambikia kesi huyo jamaa haujakamilika. Wameshaumbuka vya kutosha kwa Ulimboka kutamka kwamba huyo aliyemteka anamfahamu na anafanya kazi Ikulu, lakini wao bado wanatumia pesa chungu nzima kujiumbua zaidi ili kumbambikia asiyehusika kesi isiyomhusu!!!
 
Back
Top Bottom