Kesi ya kutaka Heche afikishwe Mahakamani yaahirishwa hadi Novemba 10, 2025, IGP na wenzake wafika mahakamni

Kesi ya kutaka Heche afikishwe Mahakamani yaahirishwa hadi Novemba 10, 2025, IGP na wenzake wafika mahakamni

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Kesi namba 26287/2025 iliyofunguliwa dhidi ya Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini na wenzake ikitaka kufikishwa mahamani kwa Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara John Wegesa Heche imeahirishwa mpaka jumatatu ya novemba 10, 2025.

Kesi hiyo iliitwa kwa mara ya kwanza leo Novemba 7, 2025 katika Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Ndogo ya Dar es Salaam mbele ya Jaji Bwegoge ambapo upande wa mlalamikaji uliieleza mahakama kuwa mteja wao anapaswa kuletwa mahakamani haraka baada kuwa anashikiliwa karibu takribani tatu na Jeshi la Polisi bila kushtakiwa ikiwa ni kinyume na sheria.

Wakili Mwandamizi Mpale Mpoki aliieleza mahakama kuwa mteja wao anapaswa kiachiwa kwa dhamana au kama wanaomshikilia wanadhani ana makosa basi wamfikishe mbele ya mahakama na kumshtaki kwa mujibu wa sheria.

Upande wa Jamhuri ulieleza mahakama kuwa unahitaji muda ili kuweza kuandaa na kuwasilisha kiapo kinzani hivyo wapate muda.

Hata hivyo Wakili Mpoki aliieleza mahakama kuwa kwa kujali uhuru wa mteja wake ni vyema mahakama ikazingatia maombi yao ya kutaka kuachiwa kwa mteja wao au kufikishwa mahakamani.

Hivyo kesi hiyo imeahirishwa mpaka jumatatu ya Novemba 10, 2025 saa nne na nusu.


​
 
Back
Top Bottom