Kesi ya kutaka Muungano ufutwe yaanza rasmi Znz

Kesi ya kutaka Muungano ufutwe yaanza rasmi Znz

GHIBUU

JF-Expert Member
Joined
Jan 13, 2011
Posts
4,432
Reaction score
3,013
Zanzibar kesi inayotaka Muungano waTanganyika na Zanzibar ufutwe imefunguliwa katika Mahakama Kuu yaZanzibar. Kesi hiyo iliahirishwa jana MahakamaKuu ya Vuga mjini hapa na Mrajisi wa Mahakama Kuu ya Zanzibar, George Kazi hadi Agosti 23, mwaka huu.

Mrajisi aliahirisha kesi hiyo iliyofunguliwa na watu 1,950 wa Unguja na Pemba kwa vile Jaji Mkuu waZanzibar, Omar Othman Makungu hakuwapo. Kesi hiyo ya aina yake ambayo imepangwa kusikilizwa na Jaji Mkuu wa Zanzibar, inataka kubatilishwa kwa makubaliano ya muungano kati ya dolahuru za Zanzibar na Tanganyika.

Wadai katika kesi hiyo wakiongozwa na mwanaharakati Rashid Salum Adiy, wanadai kuwa hakuna hati ya makubaliano ya muungano inayodaiwa kusainiwa Aprili 22, mwaka 1964 siku mbili kabla ya siku ya muungano, Aprili 26. Wafunguaji kesi hiyo wanadai kuwa, mambo kadhaa yanayohusu Muungano yalikuwa batili na kwa hiyo wanaitaka Mahakama Kuu ya Zanzibar itamke hivyo iliiruhusu kuzaliwa kwa dola huru ya Zanzibar yenye mamlaka kamili.

Walalamikiwa katika kesi hiyo ni Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Baraza, Mwanasheria Mkuu wa Muungano na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mtaifa.

chanzo Mwananchi
 
Zanzibar. Kesi inayotaka Muungano waTanganyika na Zanzibar ufutwe imefunguliwa katika Mahakama Kuu yaZanzibar.

Kesi hiyo iliahirishwa jana MahakamaKuu ya Vuga mjini hapa na Mrajisi wa Mahakama Kuu ya Zanzibar, George Kazi hadi Agosti 23, mwaka huu.



Mrajisi aliahirisha kesi hiyo iliyofunguliwa na watu 1,950 wa Unguja na Pemba kwa vile Jaji Mkuu waZanzibar, Omar Othman Makungu hakuwapo.

Kesi hiyo ya aina yake ambayo imepangwa kusikilizwa na Jaji Mkuu wa Zanzibar, inataka kubatilishwa kwa makubaliano ya muungano kati ya dolahuru za Zanzibar na Tanganyika.



Wadai katika kesi hiyo wakiongozwa na mwanaharakati Rashid Salum Adiy, wanadai kuwa hakuna hati ya makubaliano ya muungano inayodaiwa kusainiwa Aprili 22, mwaka 1964 siku mbili kabla ya siku ya muungano, Aprili 26. Wafunguaji kesi hiyo wanadai kuwa, mambo kadhaa yanayohusu Muungano yalikuwa batili na kwa hiyo wanaitaka Mahakama Kuu ya Zanzibar itamke hivyo iliiruhusu kuzaliwa kwa dola huru ya Zanzibar yenye mamlaka kamili.




Walalamikiwa katika kesi hiyo ni Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Baraza, Mwanasheria Mkuu wa Muungano na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mtaifa.

chanzo Mwananchi
Hizi ni habari njema mno.....bora muungano ukufilie.mbali!!!!
 
kwanini wakati wa muungano Zanzibar ilipewa hadhi ya nchi mpaka kuitwe muungano wa nchi mbili?labda wangelifanya mkoa haya matatizo yasingetokea zanzibar ina hadhi ya mkoa na siyo nchi.
 
Very interesting case, I think it shall be a landmark among constitutional cases then a good precedence in our legal regime!
 
Mbona mmechagua njia ndefu hivo.
Kama mnae makamu wa rais anaesema wazi hataki muungano.
Mnae rais wenu mstaafu na mtoto wa mwasisi wa huo muungano hautaki muungano,
Mnae rais wenu wa sasa ambae anaogopa kusema hadharani kuwa hautaki Muungano.
Mnayo serikali yenu ambayo imeundwa na 90% ya watu ambao hawataki muungano,
Mnao wawakilishi wenu kwenye baraza lenu hawataki muungano.
Mnayo katiba yenu inayotamka wazi kuwa zenji ni nchi huru, na alama zote za nchi huru katiba yenu imewapa.
Mnalo jeshi lenu lile mmebadilisha jina mnaliita Kikosi maalum haliko kwenye muungano.

Sasa.......
Mahakamani mnafata nini?
Mahakama ambayo nayo kumbe si muungano.
Kwa nini msijitelezeshe tu, tusikie tukiamka kesho kuwa "Zanzibar imejitangazia Uhuru kutoka kwa ukoloni wa Tanganyika"??
Hii itakuwa habari njema kwa pande zote znazohusika.
 
Mi naomba washinde na maamuzi ya mahakama yaangukie katika Z'bar kuwa dola huru ili Watanganyika tujipange vizuri sasa.
hii kesi ya kutishia tanganyika,
hawataki muungano na hawataki kuuacha.
Ngumu kumeza, ngumu kutema,, ma kina yakhe bana
 
We GHIBUU,
Nani mwamlalamikia?
 
Last edited by a moderator:
Muuungano ukivunjika....
Watanzania bara itabidi tuitwe Watanganyika...

Tanganyika doesn't sound good as Tanzania

Maana ya Tanganyika:
Tanga means Kutanga tanga and Nyika means mwituni
Mtanganyika=> Mtu wa kutangatanga mwituni.....
Sitaki kuitwa Mtanganyika mm, bora Muungano usivunjike, Udumu Muungano Milele Daima
 
Bora hii kesi ilivyokwenda maana CCM wanaona wana hati miliki ya TZ wanachokitaka wao ndio kiwe. MA-Pinda wakubwa
 
Mbona mmechagua njia ndefu hivo.
Kama mnae makamu wa rais anaesema wazi hataki muungano.
Mnae rais wenu mstaafu na mtoto wa mwasisi wa huo muungano hautaki muungano,
Mnae rais wenu wa sasa ambae anaogopa kusema hadharani kuwa hautaki Muungano.
Mnayo serikali yenu ambayo imeundwa na 90% ya watu ambao hawataki muungano,
Mnao wawakilishi wenu kwenye baraza lenu hawataki muungano.
Mnayo katiba yenu inayotamka wazi kuwa zenji ni nchi huru, na alama zote za nchi huru katiba yenu imewapa.
Mnalo jeshi lenu lile mmebadilisha jina mnaliita Kikosi maalum haliko kwenye muungano.

Sasa.......
Mahakamani mnafata nini?
Mahakama ambayo nayo kumbe si muungano.
Kwa nini msijitelezeshe tu, tusikie tukiamka kesho kuwa "Zanzibar imejitangazia Uhuru kutoka kwa ukoloni wa Tanganyika"??
Hii itakuwa habari njema kwa pande zote znazohusika.

Kwanini Tanganyika isijitowe na kusema kuanzia leo Tanganyika ni huru?

Hivi Tanganyika ipo?
 
​Wakuu naomba mnisikilize:

Siungi mkono muungano wa serikali mbili kwa sababu hata tukisema tutatue kero za muungano wa haina hiyo leo; kesho zitakuja nyingine na nyingine. Kwa kifupi kero zake ni endelevu!


Mimi nadhani kilichotufanya tuungane kwanza ni kutaka kuonesha njia kwa mataifa mengine ya Afrika. Kuonesha njia ambayo baadaye ingetufikisha pale ambapo Afrika nzima ingekuwa moja. Nyerere alikuwa na haki na wajibu wa kuipoteza Tanganyika ili kuidhihirishia Afrika na dunia imani yake kwenye Muungano wa Afrika! Kipindi kile ilikuwa ni sifa kubwa sana kupigania Umoja wa Afrika.


Sababu ya pili ilikuwa ni ya kuhimarisha ulinzi na usalama kwa wakati ule!


Sababu zote hizo hapo juu hazina mashiko tena kwenye zama hizi za ubepari! Sasa kwa nini tuendelee kuishi imani zisizokuwepo!


Ikumbukwe kuwa zile juhudi za kuliunganisha bara la Afrika zilikufa hata kabla hazijafika mbali kwa sababu wengi wa waliokuwa wanaamini kwenye umoja wa Afrika walitoweka na mawazo yao!


Hata zile juhudi za kuziunganisha nchi za Afrika Mashariki hazina uhai tena. Sisi ni mashuhuda wa kifo chake kitakatifu; tunasubiria tu kitangazwe rasmi siku za usoni!


Nauliza maswali hapa: Ni kwa nini kuwepo na muungano ambao mshirika mmoja anakubali kupoteza ili kumwokoa mwingine? Hata kwenye ndoa haiwezekani ndugu ni lazima walete chokochoko mwenzi mmoja akitoweka!
Eti serikali tatu haiwezekani kwa sababu Zanzibar haina uwezo! Ni kwanini nchi ijione haina uwezo wakati ilitafuta uhuru wake ili ijiendeshe?


Kama kujiendesha kwake ni kwa kutegemea taifa lingine haioni kuwa ina uhuru wa bendera tu?
Kama Zanzibar wa hofu wakiungana rasilimali zake kama mafuta n.k zitapotea; je, Tanganyika yenye gesi, mafuta, wanyamapori, makaa ya mawe, madini ndiyo iendelee kujitoa sadaka???! Basi Tanganyika itakuwa ni nchi nzuri sana ya kuishi kwa sababu haina hofu ya kuishiwa rasilimali!


Endapo atajitokeza mtu wa kuainisha pasipo shaka mipaka ya mapato na matumizi baina ya Tanzania Bara, Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nitafarijika sana! Nasema hivi kwa sababu ninachokiona mimi ni kuwa chochote kipatikanacho Tanzania Bara ni faida ya wote na cha Zanzibar ni kwa faida ya Zanzibar tu pekee.


Je, hii inaonesha kuwa Tanzania Bara inajiamini kuwa yenyewe ndiyo yenye uwezo wa gharamia serikali ya muungano na inaona fahari kufanya hivyo?! Au labda kuna masuala mengine Tanzania Bara inanufaika nayo ambayo sisi wananchi hatujui!
Je, Zanzibar nayo inaona fahari tu kuhudumiwa kila kitu kwenye muungano na wala haioni kuwa Tanzania Bara imebeba jukumu zito? Na je Zanzibar isipotimiziwa mambo kadhaa watakuwa radhi kulalamika ilhali wamebebwa katika mambo mengi?


Nionavyo mimi kama tatizo ni gharama za kuendesha serikali tatu ambazo ndo halali ni sharti tutafute mfumo wa kudumu kutatua tofauti zetu! Tukumbuke kuwa upande mmoja wa muungano umeingia gharama kubwa kuhudumia serikali ya muungano kwa zaidi ya miaka 49 sasa! Au iaonekana Tanganyika hajichoka kulea muungano na Zanzibar nayo haijachokaa kubebewa!


Tusijidanganye; Tanzania ni jina! Nchi ni sisi wananchi! Na wananchi wa pande zote za Muungano wamechoka kulazimishiwa muungano wa serikali mbili! Tunaowaona wanatetea ni baadhi ya watawala ambao muungano uliopo sasa unawanufaisha kwa namna fulani.
Kama wananchi wengi wanadai muungano hauwatendei sasa inabidi tuseme imetosha tutafute kitakachotupa haki na usawa. Na hiki si kingine zaidi ya nchi zote kuungana na kuwa chini ya serikali moja itakayohakikisha kila raia anakuwa na haki sawa na mwenzake bila kujali atokako!


Ingependeza tuwe na serikali tatu kila nchi ijihudumie kwani kila nchi ilidai uhuru ili iwe huru! Lakini watu wanaeneza mawazo hasi ya ukubwa wa gharama!Umaskini na uvivu wa fikra! Ikumbukwe chochote kizuri ni sharti kiwe na gharama yake; tena gharama kubwa!
Kama tunakimbilia unafuu wa serikali mbili tufahamu wazi kuwa nafuu mara zote ni ghali zaidi na mara zote hazidumu!


Muungano wa serikali mbili vilio vya unyonyaji! Muungano wa serikali tatu tunaogopa gharama! Basi muungano unaotufaa ni wa serikali moja. Kama hatuwezi muungano wa serikali moja, muungano wowote ule utakaokuwepo aidha wa serikali mbili, tatu au zaidi hautatuliza kiu ya wananchi! Narudia tena: Tanzania ni jina; nchi ni wananchi!


Nashangaa nchi zenye watu zinaogopa kujiwekea mifumo ambayo itawastawisha na kumaliza chokochoko kwa visingizio visivyoisha! Ina maana pamoja na rasili mali tulizonazo viongozi wetu wanataka kututhibitishia kuwa hawawezi kuweka mifumo ya kuliendesha taifa kwa ustawi!


Hoja ya kuwa kuna udugu wa damu kati ya Tanganyika na Zanzibar ni hoja ya kibaguzi kwani uhusiano wa damu upo pia baina ya Tanganyika na nchi nyingine. Swali hapa: Ni kwa nini tusiungane na Kenya, Uganda, Msumbiji, Burundi, Malawi, Zambia, n.k kwa sababu hata huko wapo watanganyika wana ndugu zao?
Kama hoja ni udugu ni kwanini Zanzibar wanapochagua wabunge wa kuja kwenye bunge la Jamhuri wa Muungano, upande wa Tanzania Bara nao wasichague wawakilishi wachache kwenye Baraza la Wawakilishi ili kuukuza zaidi huo unaoitwa udugu???
Udugu unaonufaisha upande mmoja zaidi ya mwingine si mzuri jamani! Tuache propaganda. Kama tunaamini umoja ni nguvu utengano ni udhaifu basi tuungane tuwe nchi moja, serikali moja, rais mmoja na Tanzania moja ili tuwe ndugu kweli!


Watasema ni chuki lakini kama hatuwezi kumaliza tofauti zetu kwa kuunda serikali tatu au moja basi ni bora kila nchi ijendee kivyake! Hata Kenya na Uganda ni ndugu zetu lakini hatujaugana nao kutengeneza taifa la kusadikika!


Litakuwa ni kosa sana kuendelea kuwa na muungano ambao upande wa Tanganyika tu ndiyo unaendelea kupoteza historia yake wakati mshirika wake Zanzibar akibakiwa na ziada hata kama ni sawa na wilaya moja ya Tanganyika!


Wakuu; naombeni kuwasilisha hoja!
 
Sultan mwarabu wa Zanzibar huko Uk kisha kaa mkao wa kula. Sasa nyie wenye ngozi kama yangu tafuteni pa kwenda.
 
Hiyo bado ni trela move lenyewe halijaanza,kuna simba a.k.a B52 a.k.a UAMSHO zamu yao bado ikifika zamu yao nafikiria kila mtanganyika aliekuwa kichwa ngumu kuelewa ataelewa.
 
Back
Top Bottom