Nyakijooga
JF-Expert Member
- Dec 9, 2018
- 524
- 829
Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi wa CHADEMA, Brenda Rupia, amemaliza kutoa ushahidi katika kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama hicho, Tundu Lissu.
Brenda amekamilisha kutoa ushahidi wake leo, Septemba 9, 2026, baada ya kumaliza sehemu zote za utetezi wake, ikiwemo kufanyiwa dodoso. Hivyo, anakuwa shahidi wa nne upande wa mshtakiwa kukamilisha kutoa ushahidi wake, akiwemo mshtakiwa mwenyewe.
Baada ya hatua hiyo, majaji wameahirisha shauri hilo kwa muda wa saa moja na nusu, hadi saa nane na nusu mchana huu. Baada ya hapo, shahidi wa tano upande wa utetezi atapanda kizimbani kuanza kutoa ushahidi wa kumtetea Lissu.
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, John Heche, ambaye ni miongoni mwa mashahidi waliotajwa na Lissu, anatarajiwa kuwa shahidi wa tano kuanza kutoa ushahidi wake. Hivyo, idadi ya mashahidi watano ambao hawakupingiwa na Jamhuri itakuwa imekamilika, kabla ya kusubiri uamuzi wa Mahakama kuhusu mashahidi wengine ambao Jamhuri iliwawekea pingamizi.
Pingamizi hilo lilitokana na kuibuka kwa mabishano ya kisheria kuhusu suala la kupelekewa wito wa kuitwa mahakamani ili kutoa ushahidi.
Ikumbukwe kuwa Lissu aliwasilisha orodha ya mashahidi 11 wa utetezi. Hata hivyo, Jamhuri, kupitia Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), ilipinga mashahidi saba kati yao, wakiwemo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan; Dkt. Philip Mpango, Makamu wa Rais Mstaafu; Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu Mstaafu; Camillius Wambura, Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP); Jenerali Jacob Mgunda, Mkuu wa Majeshi; pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Usalama wa Taifa.