Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Leo Februari 23, 2026 kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu inatarajiwa kuendelea Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Ndogo ya Dar es Salaam ambapo kwa leo upande wa mashtaka unatarajiwa kuwasilisha maombi ya ushahidi wa ziada kisha ushahidi kuendelea.
Tayari Lissu amefikishwa viunga vya Mahakama kuu na leo ushahidi ukiendelea kutolewa itakuwa ni zamu ya shahidi wa 16 Jamhuri (upande wa mashtaka).
Tayari Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu ameingizwa katika chumba namba 1, cha Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Ndogo ya Dar es Salaam kwa ajili ya kesi ya uhaini inayomkabili.
Wiki iliyopita tuliishia sehemu ya 119 na leo tunaendelea na sehemu ya 220
Mawakili wa Serikali wapo tayari na Majaji wana kila dalili ya kuingia muda wowote.
Anasimama Kalani anasoma case number.
Anasimama Renatus Mkude, tupo Ajuaye, Katuga, Thawabu Issa na Cathbert Mbiringe. Shauri lilipangwa kwa ajili ya kusikiliza Notice ya kuongeza mashahidi na ushahidi na sisi tuko tayari.
Majaji wanaandika kidogo.
Wanamuuliza Mshitakiwa.
Lissu anajibu na yeye kuwa yuko tayari.
Wanaitwa Upande wa Mshitaka/Jamhuri anasimama Katuga kuanza.
Lissu waheshimiwa Majaji nimepinga hiyo notice toka ijumaa kwahiyo ningesikilizwa.
Katuga Mheshimiwa Jaji utaratibu ni sisi kuiwasilisha ili yeye apinge kama ana hoja ya kupinga hii sio Application.
Lissu anasema Waheshimiwa Majaji hicho wanachoita notice sio notice kabisa na hakitambuliki kisheria.
Jaji sisi tulitaka waeleze nini kinaendelea tu.
Lissu: Kama ni hivyo sawa.
Katuga: Mnamo tar. 18/02/2026 kwa njia ya mtandao tulifile notice ya kuongeza ushahidi (notice to file additional statement of evidence) tuliifile kwa mujibu wa kifungu cha 308 cha CPA.
Pamoja na notice hiyo tuliambatanisha substance ya ushahidi huo, ushahidi huu haumleti shahidi mpya bali ni nyongeza ya Ushahidi wa ACP, Amin Mahamba.
Kwamba ushahidi huu haujakuwa committed Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu.
Notice hii inakuja kukidhi matakwa ya kifungu cha 308 cha CPA ambacho kinasema hakuna shahidi au maelezo ya shahidi vitatolewa Mahakamani unless viwe vimesomwa wakati wa mwenendo kabidhi (committal)
Kifungu hicho kinafafanua maana ya substance of evidence ikiwa ni pamoja na kitu chochote ikiwemo nyaraka na vitu vingine vinavyoshikika.
Kama ambavyo notice inajieleza, substance ya ushahidi kwamba Amin Mahamba alikuwa ni kiongozi wa timu ya upelelezi wakati wa uchaguzi wa 2025 na baada ya uchaguzi.
Na kile alichokipata kutokana na upelelezi ni kitu ambacho haukusomwa pale kwenye committal.
Ushahidi huo tumeupata na kuugundua wakati tumejiandaa kumuita ACP Amin Mahamba siku ya tarehe 16/02/2026 kwa mujibu wa kifungu cha 308 cha CPA hakijaeleza ni kwa jinsi gani notice itakuwa. Hata kwenye zile prescribed form zilizopo kwenye Sheria hii haijawekwa.
Kifungu hicho kinasema notice ieleze jina la shahidi, substance ya ushahidi na details za shahidi kiujumla kwa mujibu wa kifungu cha 308 (2) cha CPA.
Hivyo vyote tumefanya kwenye notice yetu kucover matukio ya tarehe 29/10/2025.
Anasimama Lissu, anasema waheshimiwa mbona kama anaendelea kufanya mambo ambayo hamjamuelekeza.
Katuga waheshimiwa kwani hiyo introduction iko chini ya Sheria gani? Sisi tunaintroduce kwa namna tunayoona ili mwenzetu.
Lissu: Asinifundishe Sheria, asijaribu kabisa kunifundisha Sheria, anaanzaje kufanya submission ya hiyo notice kabla uhalali wake haujaamuliwa.
Katuga: Waheshimiwa hakuna bingwa wa Sheria, mabingwa ni nyie tu Majaji.
Majaji wanateta pale juu.
Tunasubiri muongozo wao.
Sehemu ya 221
Jaji Ndunguru anasema yafuatayo: Tumesikiliza hoja zote hivyo vijembe vyenu msivilete.
Sasa mshitakiwa alisema anapingamizi na tukasema upande wa mashitaka walete open statement ili Mahakama iamue.
Mambo mengine ya kwamba imeambatana na nini na nini kipo wapi hayo sio mambo ya msingi.
Mshitakiwa endelea sasa, hawa upande wa mashitaka mmemaliza hapo, presentation ya notice na justification ya notice.
Watu wanacheka hapa 😂😂😂😂
Lissu amasimama, sasa Waheshimiwa Majaji kwa kuanzia niseme hivi waliyosema wenzetu.
1. Upande wa mashitaka unasema notice yao haileti shahidi mpya bali inaongezea ushahidi wa shahidi ambae ushahidi wake ulishatolewa kwenye committal.
2. Wamemtaja huyo shahidi kwa jina kabisa.
3. Wamesema wameleta viambatanisho vinavyotakiwa kwa mujibu wa kifungu cha 308(2) cha CPA.
Sasa baada ya kusema twende kifungu kinavyosema cha 308
A witness whose statement or evidence was not read during committal......
Kifungu kinasema shahidi mpya.
Kinachotakiwa kuletwa ni jina la shahidi wa ziada, huyu ndio anaweza kutolewa notice.
Wamesema wenyewe hawaleti shahidi mpya bali wanaongezea ushahidi wa shahidi aliyepo.
Sasa huyu shahidi ambaye tayari yupo na wamemtaja huyo Shahidi ACP Amin Mahamba.
Sasa waheshimiwa Majaji naomba niwaalike kwenye ukurasa wa 90 na 91 na 99 na 100 wa record ya committal proceedings na ukurasa wa 134 wa record ya Mahakama hii ambapo upande wa mashitaka ulitaja majina ya mashahidi wao.
Huyo Amin Mahamba yupo na mimi maelezo yake ninayo hapa sasa Waheshimiwa majaji hiyo notice inaingiaje mahakamani?.
Ushahidi wake tayari upo mahakamani na notice inatakiwa iwe ya shahidi ambaye maelezo yake hayakusomwa mahakamani.
Hii sio notice ya additional witness ni notice ya additional evidence ambayo haipo kisheria nimetafuta CPA yote hicho wanachosema hakipo.
Jambo lingine ni kwamba wanaleta ushahidi wa mtu aliyefanya upelelezi wa matukio ya uchaguzi mkuu 2025 sasa Majaji matukio ya tukio ya tarehe 29/10 mimi tayari niko mahabusu
Anasimama Katuga anasema tunapinga anaanza kujadili ushahidi wetu kama mtakubali ni sawa tu.
Lissu: Si ndiyo kayaleta haya mwenyewe wanakatazaje nisiyazungumzie?
Jaji Ndunguru: Mshitakiwa endelea.
Lissu: Amesema mwenyewe kwa mdomo wake hapa Mahakamani. Nilimwambia asibwabwaje sana. Akang'ang'ania kuanza kusema mambo ya tarehe 29/10 ndio maana na mimi nasema hayo ya tarehe 29 mimi nilikuwa jela.
Wanafikiri hayo yatawasaidia maana wanataka kugeuza mashitaka kwa kuleta mambo ya tarehe 29/10/2026. They can not amend the information through the back door. Kama mnataka ku amend information nendeni kwenye kifungu cha 294 ch CPA.
Hiyo wanayoiita notice haipo kisheria. Haitambuliki. Hiyo notice muifutilie mbali. Yaani notice na yaliyomo.
Na mwisho, Wahe. Majaji hiyo notice ikiachwa ikawa sehemu ya record ya Mahakama itafungua sanduku la pandora ambalo lina kila aina ya mambo mabaya ambayo sidhani kama itaweza kushughulika mambo hayo.
Wanataka tuzungumze mambo ya October 29 mtakuwa mmefungulia balaa na isije ikawa shida. Mkifungua huo mlango tutaenda huko. Tutazungumzia mauaji ya kimbali na tutaulizana nani aliyeua watanzania. Hii kitu haina mashiko. Are they ready? Mimi niko tayari. Isiruhusiwe ikiruhusiwa niko tayari?
Jaji tafadhali naomba tusiende huko.
Katuga aliambiwa na Lissu kuwa huwezi kunifundisha Sheria akakataaa. Baada ya Lissu kumaliza hapa. Katuga amekuwa mdogo sana yani. Ni kama anataka kulia.
Katuga anasimama anasema napaswa kufanya nini reply au rejoinder
Lissu anasema fanyeni reply halafu mimi ndio nitakuja kumaliza.
Wanakubaliana hivyo.
Sehemu ya 222
Katuga anasema kifungu cha 308 ni mlinzi wa kifungu cha 263 cha CPA ni kumfanya mshitakiwa awe aware na ushahidi wote anaokutana nao Mahakama kuu.
Ushahidi upo wa aina nne, real, documentary, testimonial na nyingine nimesahau nitaikumbuka.
Kwahiyo kwa maana ya aina ya shahidi nne zinatakiwa zioneshwe kwa mshitakiwa kabla ya kuwa committed kwenda High Court na kwakuwa kuna takwa hili la 263 kukawekwa kifungu cha 308 ambacho ni mlinzi sasa.
Kwamba hakutakuwa na ushahidi utakaoingia hadi uwekwe wazi basi prosecution wampe notice kuhusiana na ushahidi huo ni lini prosecution wamegundua huo ushahidi. Je mshitakiwa alikuwa na reasonable time kuupitia.
Kif. 308 (4) kinazungumzia substance or witness.
Kesi ya Remina Omary Abdul vs Jamhuri CA 189/2020 Mahakama ya Rufaa ilisema, INASEMA IF PART OF THE EVIDENCE IS NOT DISCLOSED.
Mahakama ili quote with approval maneno kuwa additional evidence is allowed.
Sisi tunasema mbali na statement yake kusomwa tunataka kuleta mambo mengine ambayo hayakujumuishwa.
Notice hii ina comply na tafsiri ya sheria na sio tafsiri ya mtu. Iko sheria na tunaomba ikubaliwe.
Katuga kuna maneno pia yamesemwa kuwa notice hii ikiachwa hizo sio hoja. Unamtisha nani? Naona kama anatutisha ni hoja ambayo itafungua pandora na hiyo pandora ni ipi?
Tunaomba mapingamizi yatupiliwe mbali.
Anasimama Mh. Lissu kumjibu Kituga.
Nimesikiliza majibu yao naomba niseme yafuatayo.
1. Kifungu cha 308 cha CPA kinahusu shahidi mpya. Shahidi mpya kimesema ni yule ambaye maelezo yake au substance ya maelezo yake haikusomwa kwenye committal. Kwahiyo kifungu hicho kinahusu shahidi mpya na sio ushahidi mpya. Suala ni shahidi wa ziada na sio ushahidi wa ziada wa shahidi ambae tayari maelezo yake yapo tayari.
2. Kwenye notice hii suala la kuamua sio reasonable au laa. Ni suala la kinacholetwa ni shahid mpya au laa.
3. Hiyo kesi ya Remina Omary Abdul waliyoleta si mara ya kwanza inazungumzwa kwenye Mahakama hii. Ililetwa kipindi kile cha Committal. Inahusu kifungu cha 263 tu. Ukurasa wa 32 ni kuhusu section 246 ambacho ni 263 ya sasa. Kwahiyo hiyo kesi inahusiana na mambo ya Committal basi kifanyeni kwa mujibu wa kifungu cha 308 cha CPA.
Mlango wa Amin Mahamba ulifungwa kwenye committal kama mnataka tafuteni shahidi mwingine sio Amin Mahamba.
Hoja ya kwamba hili ni pingamizi limeletwa pre mature nasema liko timely maana yanayohusika na kesi hii yalishakamilika na kuletwa Mahakamani.
Effect yake ni kunibadilishia shitaka maana shitaka langu ni la tar. 03/04/2025 haya ya October ni mambo mapya.
Mkiyaruhusu kwa kuruhusu notice hiyo na nimesema niko tayari, je wao watayaweza? Kwasababu ya October kuna genocide kuna mass killings, mass murder. Ya October ni magumu sana.
Pingamizi langu litalinda integrity ya shauri hili na mashauri haya. I'm only trying to help them wanafikiri kuna deal pale hakuna deal yoyote.
Angalieni kifungu cha 308 cha CPA.
Hii notice ifutiliwe mbali, naomba hivyo.
Majaji wanateta hapa.
Tunasubiri uamuzi wao kuhusu pingamizi hili.
Jaji Ndunguru amejadiliana na wenzake kwa muda mrefu sana hapa.
Anasema ili tuweze kuandika uamuzi na tutarudi kesho saa tatu asubuhi na tutaendelea na mashahidi wengine.