mwakatojofu
JF-Expert Member
- Dec 17, 2008
- 326
- 227
Ahsante Mushi kwa Ushauri. Na kweli nimelala nikaamka na mawazo tofauti. Kwa sasa nakubaliana na wewe kwa 100%. Ni kweli kabisa Kikwete amemtorosha Liumba.
Tena nimegundua kwamba kwa muda huu Liumba kafichwa Ikulu! Tusubiri kidogo nasikia kuna njama nyingine zinafanywa na Kikwete kumtorosha yule aliyebaki, .... Kweka, i think!
Kikwete bwana, anatuzuga sana aisee Mushi. Mimi naona dawa ni kumshambulia hapa JF kwa kila aina ya tusi, mpaka aache huu usanii wake! Anatuona sisi hatuna akili kabisa aisee!
nikisoma hapo napata hisia humaanishi unachoandika. huelekei kukubaliana na maandishi yako.
dhahiri kabisa unamkingia kifua JK.
lakin mi naamin the best thing you can do here ni kushambulia hoja ya mtu na si mtu. kwamfano, kama mtu anasema kikwete kahusika kumficha liumba, basi ikabili hoja hiyo. uongelee jinsi isivyowezekana jk kufanya kitu kama hicho. kwamba labda hana uwezo. au ni msafi sana. au mcha mungu sana. au watoe ushahidi. au .......
hapo utakuwa unajenga. na hapo utakuwa unaelimisha. and who knows? utakuwa unafundisha wengine kuchangia hapa. lasivyo utakuwa unaleta ubishi wa simba na yanga mitaani kwetu