jmushi1
Platinum Member
- Nov 2, 2007
- 26,329
- 25,263
Kuna taarifa kwamba Amatus Liyumba, ambaye sasa anatajwa kwamba ametoroka na hajulikani hayumo, HAJATOROKA na kwamba alikuwa amejipumzikia akiangalia afya yake huku akijipanga kutimiza masharti ya dhamana ambayo yanaelezwa kwamba mawakili wake walifanya 'madudu' kwa kushirikiana na Hakimu Khadija Msongo.
Kwa taarifa hizo ambazo hadi sasa ni TETESI, Liyumba sasa anaweza kuibuka tena mahakamani kati ya kesho Jumatatu na Kesho kutwa Jumanne, kuwasilisha hati za ziada za dhamana zenye thamani sawa ama zaidi ya sh bilioni 54.
Kama hiyo ni kweli basi wiki ijayo tutakuwa na mjadala tofauti na tunaoendelea nao sasa.
Mods, mutaangalia kama haistahili mutaiunganisha kule!!!!!!!
Mboga moto ugali moto, yetu macho...Kama alivyosema cottonEyeJoe hapo juu...Inashangaza hapo sijui madudu yatakuwa yapi kati ya hizo bilioni 54 kupatikana,TAKUKURU kutoa donge nono ama hakimu Khadija na mawakili wa Liyumba.
Bado ni mauza mauza,lets wait and see.