Kesi ya Liyumba, Utata na Maendeleo yake

Status
Not open for further replies.

Mboga moto ugali moto, yetu macho...Kama alivyosema cottonEyeJoe hapo juu...Inashangaza hapo sijui madudu yatakuwa yapi kati ya hizo bilioni 54 kupatikana,TAKUKURU kutoa donge nono ama hakimu Khadija na mawakili wa Liyumba.
Bado ni mauza mauza,lets wait and see.
 

Hapa nadhani umechemsha. Takukuru kama kitengo, kina mamlaka yote chini ya sheria ya kukamata na kushtaki kama Polisi. Kitengo hiki ni kama polisi lakini tofauti yake ni kuwa chenyewe kinajikita zaidi kwenye rushwa. sasa wewe huoni ajabu kama ingekuwa ni jukulu la Polisi kumsaka Liyumba ni vipi Takukuru ndiyo itowe fedha za zawadi ya kumpata na ni vipi iende kumsaka nyumbanio kwake na majumba ya marafiki zake?.

Yote haya yanafanyika chini ya Katiba ya nchi..
 
Yawezekana Hakimu Hadija aliamua kumpa nafasi jamaa akapumzike ( baada ya kula fungu lake) wakati akipanga mikakati ya kuweka sawa suala la dhamana yake then huku hakimu nae anatutia changa la macho kwa kutoa hati ya kukamatwa tena.

Mi bado naamini Liyumba yupo around na soon atajitokeza. Unajua kesi zinazohusisha wizi wa mapesa mengi huwa zinawatia watu wazimu kuanzia mahakimu, waendesha mashitaka n.k. Kwani kila mmoja anajua mtuhumiwa ana pesa na yeye kwa nafasi yake anaweza kupata chochote kitu na akabadili sura ya mchezo kiaina....This is Bongo bana!!
 

Mkuu halisi,

Mimi nakuamini kwa data za uhakika. Kama umesema tetesi basi hii habari ina ukweli zaidi ya asilimia 50.

Asante sana kwa muda wote kutupa habari za uhakika.
 
TK,
Haya maswala ya jukumu ni ujinga wa siasa zetu.. Chukulia Osama bin Laden unafikiria ni jukumu la CTU kumtafuta na sio vyombo vyote vya usalama nchini Marekani?.. iweje wamepeleka jeshi la nchi hiyo huko Afghabstan badala ya kuwa ni kazi ya CTU peke yao....
Kibaka anaweza kamatwa na Mgambo iwe leo fisadi!.. unataka kunambia itakuwa jukumu la mgambo kumtafuta kibaka aliyekimbia kuhudhulia mahakamani!
 


Hapa mnazidi nichanganya tu na wenda wengi wetu tumesoma lile somo la SIASA badala ya URAIA.

Swali je? polisi akishuhudia natowa rushwa nijukumu lake kunikamata ama ni jukumu la takuru.?
Na je kazi ya polisi nini haswa?
Mimi nafikiri Tukuru ni subset ya polisi nikimaanisha shughuli zote zinazofanywa na takuru polisi pia wanazifanya lakini sio shughuli zote za polisi takuru watafanya.
Ama wanawake wote ni binadamu lakini binadamu wote si wanawake.
wanawake= takuru
binadamu = polisi.
Kama uelewa wangu ndivyo sivyo tuelimishane zaidi
 
Mkuu halisi,

Mimi nakuamini kwa data za uhakika. Kama umesema tetesi basi hii habari ina ukweli zaidi ya asilimia 50.

Asante sana kwa muda wote kutupa habari za uhakika.

Hii ni sawa tu Mods wakiiunga na ile nyingine ya Sir Leem kwasababu ile nayo ina question mark na si kwamba ni confirmed kuhusu "Utoro" wake. Hii heading inasema "Hajatoroka" Na hapo hapo inasema "yupo yupo" Bottom line habari hii ilikuwa na mwelekeo wa lolote kuwezekana from the beggining...Ila i doubt,inawezekana kuna msuguano mkali wa ndani kwa ndani given the intensity of the issue.
 


Bob

"Huenda" TAKUKURU wana mamlaka sawa/sambamba na Polisi/ Magereza...lakini hilo bado halimaanishi kuwa Polisi wanahitaji OMBI kutoka TAKUKURU kabla ya kuanza kujihusisha na juhudi za kumtafuta MTUHUMIWA ALIYETOROKA MAHAKAMANI.

Waziri Masha kazi imemshinda...
 
Mkuu halisi,

Mimi nakuamini kwa data za uhakika. Kama umesema tetesi basi hii habari ina ukweli zaidi ya asilimia 50.

Asante sana kwa muda wote kutupa habari za uhakika.

Kuna maswali ya kujiuliza:

Je, Liyumba alitakiwa kurudi lini mahakamani baada ya kupewa dhamana?
Je, Masharti gani alipewa?
Je, Nani alitakiwa kuwasiliana naye na kila baada ya muda gani?
Je, Hati ya kukamatwa/kuitwa aliiona?
Je, sheria inasemaje kuhusu dhamana na mtu kuwa nje?
Je, hati nyingine 10 zenye utata zimeshahakikiwa ama bado?

Baada ya kujibu maswali hayo, tunaweza kukuta tunajichezea wenyewe akili
 
Yebo Yebo,
Bila shaka, PCCB wanayo mamlaka makubwa ktk kesi za mafisadi lakini mtu anapotoroka linakuwa ni swala la Fugitive!.. hii ni hatua nyingine kabisa ambayo inahusiana na vitengo vyote vya Usalama.. Liyumb alipoiba BoT ilikuwa ni mamlaka ya BoT kumchukulia hatua lakini pindi swala zima lilipoingia ktk Ufisadi na kufunguliwa mashtaka haikuwa jukumu la BoT tena ingawa wanahusika kwa kiasi kikubwa..
Vile vile PCCB walipomfikisha Liyumba mahakamani mbele ya sheria inabidi nao wafuate sheria na taratibu za mahakama nje ya matakwa yao.. Sasa kama Liyumba angekuwa Keko unafikiria PCCB wangeweza kwenda pale na kumtoa nje bila dhamana kwa sababu ni jukumu lao, wana maamuzi yote!.. Uamuzi wowote wa mahakama ni sheria nje kabisa ya uwezo wa PCCB.. dhaman ikataliwe au ikubaliwe sio kazi ya PCCB kwani hiyo ni hatua nyingine..Na sidhani kama kisheria lilikuwa jukumu la PCCB kuhakikisha kwamba Liyumba hatoroki..hawa jamaa zetu hapa wanajichanganya tu..
Navyofahamu mimi hakuna sheria inayompa jukumu mshtaka kumchunga mshtakiwa hasa baada ya kesi kuwakilishwa mahakamani...sijui labda nipewe somo hapa!

Liyumba kakimbia kutohudhuria mahakama - ni FUGITIVE hilo swala la Ufisadi linawekwa pembeni..maswala ya zawadi hata mimi naweza kuweka zawadi ya kumkamata mtu aliyeniibia simu lakini haina maana ni jukumu langu kisheria kumtafuta!
 
Hebu naomba nisaidieni...Hivi utaratibu huwa unakuwaje? inawezekana kupeleka hati ya dhamana wakati tayari ulishapewa dhamana? Kama Hakimu aliridhika na kiasi cha dhamana kilichotolewa mwanzo,kwanini akawasilishe hati zingine?
 
wakuu, yote kwa yote dhamani ya BILIONI 50 ni zaidi ya BILIONI 40 zilizonunua ndege na rada ambazo tunazipigia kelele!

In the event kwamba AMEWEZA kutimiza masharti hayo, basi itabidi tuhoji viashiria vya UN, WB, IMF etc vya kutuita sisi ni 'masikini wa kutupwa'!
 

Mkandara unayosema ni kweli. Pia inawezekana mojawapo ya masharti ya mdhamana ilikuwa ni kuripoti maybe kila wiki hapo mahakamani. Na inawezekana kutokutokea kwake bila ripoti ndipo wakasema ametoroka. Kiutaratibu siku ambayo hakuripoti mahakamani bila sababu za msingi na warrant inakuwa effective hapo hapo. Kwa wenzetu wanaingiza kwenye system na hata ukisimamishwa kwa kosa la traffic wanaweza kuona una warrant na wanakukamata. Sasa sijui ni rukhsa gani kina Masha waliyokuwa wakiizungumzia...Nadhani mtuhumiwa kama ni kweli katoroka basi ni mojawapo ya mbinu za kumwacha atokomee....Kama sivyo basi ni kweli tuna tatizo kubwa sana la uongozi na itakuwa ni kubwa kiasi cha kutisha.
 


Mkuu Mushi,

Sina shaka kabisa kuwa tuna MATATIZO YA UONGOZI Tanzania. Hili la Liyumba ni mfano mmoja tu.

Ukiangalia mtiririko wa matukio utaona kabisa watu wanabahatisha kwenye kazi zao;

- Liyumba hakutimiza masharti ya dhamana (mali au cash shs 55 Billionii); lakini yupo nje kwa Dhamana..!!

- Waziri anasubiri "ombi" la kumkaka atumie polisi kumtafuta Fugitive..!!

Safari yetu ni ndefu kiasi cha kuogopesha.
 
Hivi Liyumba ameshtakiwa na nani hadi MASHA aseme akipata maombi kutoka TAKUKURU anaweza akasaidia kumtafuta huyu LIYUMBA?
Masha bado anasisitiza kuwa haja pata ombi la kumtafuta MKULU lakini anasema kwa kuwa zote (TAKUKURU na WIZARA) ni idara za SERIKALI anaweza kusaidia.
HIVI,POLISI wakiona kibaka au mtu anataka au amefanya uhalifu hawawezi kumkamata hadi aliyefanyiwa uhalifu alalamike au kuomba msaada kwao?
MASHA ANATAKA TUMUELEWE VIPI?Kwamba yeye na wizara yake hawawezi kuzuia au kukamata mtu anaye shutumiwa kwa uhalifu wa aina yoyote?
 

Kiutaratibu mshtakiwa alitakiwa awepo rumande akisubiri siku ya kesi. Akaja na documents feki akapewa mdhamana. Kushindwa kutimiza masharti ya mdhamana ina maana kuwa mshitakiwa anahitajika back rumande.
Simply as that...Kazi ya kumrudisha rumande mtuhumiwa ni ya nani? Kama kesi ingekuwa haijafikishwa mahakamani bado,then thats a different issue na TAKUKURU bado wangeendelea kumfuatilia na RB yake....Kwahiyo suala la yeye kutafutwa lilitakiwa liwe efective toka siku aliyoshindwa kuripoti mahakamani hapo bila sababu ama udhuru kama masharti yanavyomtaka.
 
Kama yupo ni fresh na kama ndio hivyo inawezekana kuwa PCCB ilimuandaa mtu wa kula "donge nono"na usishangae ukasikia mtu wa karibu kabisa na mfanyakazi wa PCCB ndio ameibuka kinara na kuwezesha kukamatwa kwa LIYUMBA.
Hebu tuvute pumzi tuone "mchezo"huu wa kusisimua
 
hata kama akijitokeza na hati zenye thamani ya 55bilioni jumanne, bado atakuwa na kesi nyingine ya kujibu, kushindwa kutokea mahakamani alivyotakiwa kufanya hivyo, hivyo kwa jinsi publicity ya hili swala lilivyo, huenda mahakama ikafuta dhamna yake, mjue kuwa mahakama ina haki kufuta dhamana ya mshatakiwa inapokuwa na wasiwasi wa mwenendo wa mshatakiwa.

liumba na mawakili wake wanafahamu fika hili, haitawezekana kuonekana mahakamani jumanne kwa kuwa anajua kitakachomjiri.

kama itakuwa tofauti, basi ujue ile sinema inaendelea, huenda hata polisi wanajua aliko ndo maana maasha anasema hajaambiwa na mahakama amkamate.
 

- Mkulu Halisi,

Heshima mbele sana, wewe aminia tena 100%, lete habari mkuu tunakusoma kwa makini na ninajua kuwa uko ontop, endelea kuzitafuta tuwekee mkuu usichoke.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…