Kesi ya Liyumba, Utata na Maendeleo yake

Kesi ya Liyumba, Utata na Maendeleo yake

Status
Not open for further replies.
Kwa hiyo uamuzi rasmi wa mahakama ni upi jamani? I am left hanging...
 
Liumba akiwasuta watu mahakamani leo.
LIYUMBA LEO.JPG
 
Katika yale malumbano ya MAHAKAMA NA BUNGE wengi walisema wengi walilalamika mallalamiko ya mh...na wengi walisema yuko wrong
sasa kuna hili saga la mh AMATUS LYUMBA......Hakimu mhusika alieamua kumpa DHAMANA mh KHADIJA...LEO HII HUYOHUYO KWA DOCUMENTS ZILEZILE ZILIZOLETWA HAPO MAHAKAMANI AMEWAKANA MAWAKILI WA LYUMBA NA KUSEMA

1))THAMANI HALISI YA NYUMBA BADO WANAIJADILI

2))PASSPORT ILIOLETWA IMEXPIRE 1997

3))DHAMANA HAIKUTOSHA KAMA INAVYOTAKIWA

LEO HII KWA MUDA ULEULE;MH KHADIJA ALITAMKA RASMI MH .AL.ARUDI RUMANDE MPAKA APO ATAKAPOKAMILISHA MASHARTI YA DHAMANA.DHAMANA IPO WAZI AKIFANIKIWA KUKAMILISHA

BINAFSI BADO NAJIULIZA MPAKA NITAKAPOELEKEZWA HUYU HAKIMU ANA AKILI TIMAMU;AMA ALITAKA KUWEPO KWENYE KUMBUKUMBU KWAMBA AL;IMTOA MTU KWA DHAMANA YA MILL800 BADALA YA BILLION 50

AMA NI YALE YALE ALIOKUWA AKITUELEKEZA MH SITTA MAHAKAMA IMEJAA UOZO RUSHWA ISIYO NA IDADI;;JE NI RUSHWA ILIYOMSHAWISHI MAMA HUYU KUTOA DHAMANA ....,,,,.... AMA NI KITU GANI,,HAYA MAMBO SI YA KUYAACHIA NA NDIO MAANA INATUONYESHA HATA NDUGU...ZETU WENYE HALI YA CHINI)UMASIKINI( WANAFUNGWA KWASABABU YA KUKOSA PESA ZA
KUWAHONGA HAWA MAHAAKIMU..HATA KAMA HUNA KOSA HALI MWENYE HELA AMESHAONYESHA TURUFU KWA HAKIMU..TENA YEYE NDIE ANAMSHURI HAKIMU AMFUNGE NGAPI!!!!

VERY SAD
WENU LBM
 
Kwanini mahakimu kama hawa wasifukuzwe kabisa.....wanawachafua mahakimu na fani nzima ya sheria.......
Uwiiiiiiiiiiiiiiiii
 
Duh! ama kweli Bongo mambo yake huenda kibongo bongo..
jamani msianze kutulaumu wachangiaji wa JF kwa sababu habari yenyewe ilikuja kuwa habari kutokana na Utata wa matangazo kati ya PCCB na Wizara ya mambo ya ndani..
Kumbukeni tu kwamba Wizara hii ilikana jukumu la kumtafuta mshtakiwa wakati sote tunafahamu ni jukumu lao...
Kitu cha kushangaza zaidi ni kwamba mtu huyu alikuwepo nchini na vyombo VYOTE vya USALAMA vilikana kuwa na taarifa yoyote ya mahala alipo mshtakiwa, jambo ambalo linatupa mashaka sana.. afhadhali wangekaa kimya tu kuliko kutuvuruga akili zetu..
Kisheria kamakweli ilikuwa hajulikani alipo na alitakiwa ku report siku za nyuma basi Liyumba kavunja sheria ya mahakama hata kama amejitokeza leo.Chini ya dhamana ni lazima mshtakiwa ijulikane ana reside wapi na movements zake..
 
Angalao aliliona jua kwa siku mbili tatu. Je wale ambao hawana mihela ya kuzunguka mbuyu wako wanateseka. Karibu tena Keko mzee. Bibi Aisha usichoke kupeleka chai na chakula. Katika daftari la mahudhurio pale Keko huyu mama hajakosa hata siku moja!!!! Unajua EPA wana speacial guests attendance book Keko!!!!
 
Hapa si bure. Kuna kilicho/kilichotaka kuendelea nyuma ya pazia ila kikabumbuluka. Yatajulikana tu baadaye.
 
Nasikia karudishwa tena KEKO,je hako kadhamana kamefutwa au anatakiwa akaongezee, au kafutiwa dhamana moja kwa moja?
 
Akiitwa Stephen Spielberg hapa lazima itoke movie itakayoshinda OSCAR!

Unaweza kufanya hivyo kwa kuwasiliana naye ni idea nzuri tu;na unaweza kutengeneza pesa na ukawa maarufu bila kutarajia.
Hata hivyo,siku zote watu husema mkono wa dola/serikali mrefu;nafikiri Amatus kwa kufikiria hivyo akaona isijekuwa kizazaa kingine bora ajisalimishe ni vile dau donge nono lilikwisha tangazwa ndiyo akzidi kupagawa.
 
Taarifa rasmi: Liyumba yuko mahakamani Kisutu tayari

AIBU kwa wale walio pandisha mashetani , povu la mdomo na munkari.
Hii ni uthibitisho kuwa Watanzania kwa mdomo ndo wenyewe!!!
Semeni sasa.
 
Some are trying to discredit the MEDIA AND JF.. Bado sana keeep on trying! Huu mchezo mchafu wa Serikali umeshtukiwa and if it wasnt for the media na midomo humu liumba angekula kona kweli!!
 
Mpaka hapa sijaona kosa la wana JF, hii ni kutokana na jinsi information zilivyokuwa zina-flow kutoka Mahakama ya Kisutu na PCCB. Ndiyo maana mada kuu ilikuwa na alama ya kuuliza kwamba je, jamaa ametoroka???

Tatizo lilianzia mahakamani baada ya mawakili wa serikali kudai kwamba ni nyumba moja tu tena yenye thamani ya milioni 800 ndio yenye sifa ya kuwekwa dhamana. Vitu vingine haviko kwenye surveyed areas ama ni mali inayohamishika (mifugo na vinginevyo).

Then tukasikia kwamba file la hiyo kesi limeenda Mahakama Kuu na lilirudishwa tena Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. Kilichoandikwa ndani ya hilo file hatujui.

Baada ya hapo tukaambiwa kwamba dhamana ya mtuhumiwa imefutwa na imeandikwa hati ya kumkamata ili arejeshwe mahakamani. Katika harakati za kumsaka nyumbani kwake PCCB hawakufanikiwa kumpata na ndipo wadhamini wake walishikwa wakiwa kazini/ofisini na kupelekwa mahakamani na walishinda hapo na kuambiwa warudi kesho yake wakiwa na mtuhumiwa. Kesho yake waliporudi wakaambiwa wasubiri mpaka 24/2 na wahakikishe kwamba wanaenda na mtuhumiwa. Sasa kwanini watu wasijiulize kama mtuhumiwa katoroka au la?

Kisheria Liyumba hata kama angekuwa nyumbani asingekubali kutoka hasa ukizingatia kwamba kulishaanza dalili za kulalamika tangu alipoachiwa mahakamani. Kujiweka nje nje kungempunguzia siku mbili tatu za kupumzika uraiani kwa kuwa anaelewa wazi kwamba alitoka Keko kwa kupitia kwenye tundu la sindano. The best option kwake ilikuwa ni kujificha na kusubiri mpaka 24/2 ifike then arudi kuendelea na kesi. Unajua ukiwa uraiani ni rahisi kufanya mipango ya kupata watu wenye asset za kuweka dhamana tofauti na ukiwa Keko, maana kuna wengine hata kwenda Keko kumsalimia wanaona soo kwa kuwa jamii inaangalia nyendo zao.

Wenye kosa ni wale ambao wali-confirm kwa 100% kwamba ametoroka,. Kwa wale waliokuwa wakihisi kwamba huenda ametoroka walikuwa sahihi, maana kama mtu hayuko nyumbani kwake na wameshindwa kumpata assumption number 1 ni kwamba anaweza kuwa katoroka/ameruka dhamana.
 
Tusilaumiane wakuu ila ukweli unathibitika baada ya critical thinking.

Tusubiri mahakama itatoa adhabu ipi kwa mheshimiwa hadija msongo maana kesho nasikia mh. Jaji jundu ameukwaa ujaji kiongozi na kesho anakula kiapo
 
Shaycas,

Masha amefanya false moves nyingi katika uwaziri wake lakini hapa nadhani utakuwa unamuonea. Nasema hivyo kwa sababu the whole thing ilikuwa bizarre confusion ambayo hata hakimu ilimchanganya.

Kabla TAKUKURU hawajatangaza zawadi, Masha angejuaje Liyumba ame jump bail na anatafutwa?

Na baada ya kutangaza zawadi, kama kweli Liyumba alijump bail mbona leo ameambiwa akikamilisha masharti atapewa dhamana?

Halafu kumbuka, Liyumba sio fugitive pekee ambae angekuwa anatafutwa na polisi, kwa hiyo kama TAKUKURU wangetaka polisi iwape special attention kwa huyu mtu, ilibidi waombe rasmi ili Masha aweze ku justify kuhamisha resources, ku divert human and financial resources za polisi kumtafuta Liyumba.

Ndio hicho ambacho nadhani Masha alikuwa anafikiria.

Sasa mtu juzi mnamtafuta na zawadi juu, leo anatokea mnamu offer tena bail, huyo ali jump bail huyo? Si ndio maana Masha alioona huu ni upuuzi.
 
Mlokuwa mnasema masha! masha! yaani masha ahangaike na huyu chokest!
 
AIBU kwa wale walio pandisha mashetani , povu la mdomo na munkari.
Hii ni uthibitisho kuwa Watanzania kwa mdomo ndo wenyewe!!!
Semeni sasa.

Mimi naona hututendei haki Watanzania, sijui ulitaka wote tuwaze, tufikiri, tutende kama wewe?

Liyumba alikabidhi passport iliyokwisha muda huku akibakia na passport mpya. Aliidanganya mahakama kuwa hana passport mpya. Mahakama ilipongundua kudanganywa ikatoa hati ya kukamatwa, askari walimtafuta wakamkosa. Sasa ulitaka Watanzania tubaki kimya? Fikiri kabla hujarusha shutma kwa jamii...
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom