Kesi ya Lulu: Polisi asema alikuta chupa ya Jack Daniel na Panga kwenye tendegu la kitanda

Donatila

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
7,772
Reaction score
22,598
lulu+pic.jpg

Daktari amesema alipompima Kanumba kiwango cha sukari kilikuwa cha kawaida lakini alipompima shinikizo la damu hakupata kabisa mapigo ya moyo.

Daktari Paplas Kagaiya aliyekuwa akimtibu msanii maarufu wa fani ya uigizaji filamu nchini, Steven Kanumba ametoa ushahidi Mahakama Kuu akieleza hali aliyoikuta alipokwenda nyumbani kwa msanii huyo.

Mbali na Dk Kagaiya, askari Polisi aliyemtia mbaroni msanii wa kike Elizabeth Michael, maarufu Lulu, pia ametoa ushahidi mahakamani hapo leo Ijumaa Oktoba 20,2017.

Lulu ambaye yuko nje kwa dhamana anadaiwa kumuua Kanumba bila kukusudia kosa analodaiwa kulitenda Aprili 7,2012, Sinza Vatican jijini Dar es Salaam nyumbani kwa Kanumba.

Akiongozwa na Wakili wa Serikali, Batilda Mushi kutoa ushahidi, Dk Kagaiya amesema alipofika nyumbani kwa Kanumba alikuta akiwa ameanguka na alimpima kiwango cha sukari na shinikizo la damu.

Amesema kiwango cha sukari kilikuwa cha kawaida lakini alipompima shinikizo la damu hakupata kabisa mapigo ya moyo, hivyo alishauri Kanumba apelekwe Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Dk Kagaiya amesema daktari katika kitengo cha dharura Muhimbili alipompima Kanumba aliwaeleza alikuwa tayari ameshafariki dunia.

Baada ya kupewa maelezo hayo, amesema walikwenda kutoa taarifa Kituo cha Polisi cha Selander Bridge.

Shahidi huyo alipoulizwa na wakili wa Lulu, Peter Kibatala kama kuna vitu vyovyote alivyoviona eneo la tukio chumbani kwa Kanumba, ikiwemo chupa ya pombe alisema hakutambua chochote.

Katika hatua nyingine, askari Ester Zefania kutoka Kituo cha Polisi Msimbazi akitoa ushahidi amesema alikwenda kumkamata Lulu alfajiri, eneo la Bamaga kwa msaada wa Dk Kagaiya, ambaye walikuwa wakiwasiliana kwa simu.

Akijibu swali la wakili Kibatala kama alimpeleka Lulu hospitalini kwa matibabu, shahidi huyo amesema ni kweli alimpeleka hospitali.

Hata hivyo, Zefania amesema Lulu hakumueleza kuwa alipigwa na Kanumba na wala hakuona majeraha. Alijibu hayo baada ya kuulizwa swali na wakili Kibatala.

Zefania amesema aliagizwa na mkuu wake wa kazi ampeleke Lulu hospitalini lakini hakujua alikuwa ana matatizo gani.

Pia Afisa wa Polisi ametoa ushahidi wake kwa Mahakama wa hali ya Mazingira waliyoikuta chumbani kwa marehemu Kanumba, ambapo ASP Ester zefania ameileza Mahakama kuwa alipoingia chumbani kwa Kanumba alikuta kitanda kimevurugika kama kimetumika, stuli iliyokuwa na chupa ya Sprite, glass yenye kinywaji.Pia chupa ya Whisky aina ya Jack Daniel na kwenye tendegu la kitandana kulikuwa na Panga.

Kesi hiyo inayosikilizwa na Jaji Sam Rumanyika itaendelea Jumatatu Oktoba 23,2017 kwa upande wa mashtaka kukamilisha ushahidi wake.
 
Duh soo sad, may Kanumba the great soul rest in peace. Elizabeth Michael a.k.a Lulu wishes if she would had turned the hands of time.

But all in all kitu ambacho marehemu anataka kiwe, ndicho Mungu awezeshe ili roho yake iweze kuendelea kupumzika kwa amani.
 
Naomba kuuliza waungwana. Hivi kesi hii kuchukua muda mrefu hivyo kusikilizwa ni kwamba ni ushahidi tu ndo unaotafutwa au ni intelijensia yetu kuwa dhaifu katika masuala mazima ya kimahakama?? Tafadhali kwa mwenye uelewa na hili naomba majibu?
 
Duh son sad, may Karumba the great soul rest i peace. Lulu wishes if she would had turned the hands of time.

But all in all kill ambacho marehemu anataka kiwe Mungu awezeshe ili soho yake iweze kuendelea kupumzika kwa amani.
ulikuwa unakimbizwa wakati unaandika au? maana narudia baadhi ya maneno hayana connection mkuu
 
Naomba kuuliza waungwana. Hivi kesi hii kuchukua muda mrefu hivyo kusikilizwa ni kwamba ni ushahidi tu ndo unaotafutwa au ni intelijensia yetu kuwa dhaifu katika masuala mazima ya kimahakama?? Tafadhali kwa mwenye uelewa na hili naomba majibu?
Mkuu mbona huyu miaka mitano ni michache ukienda magerezani kuna watu wana kesi za mauaji toka mwaka 2000 na mpaka Leo hawajaukumiwa.

Tatizo ni wapelelezi wetu kuwa slow huku mahakama kuu kukiwa na majaji wachache wanaosimamia kesi za mauaji.
 
Naomba kuuliza waungwana. Hivi kesi hii kuchukua muda mrefu hivyo kusikilizwa ni kwamba ni ushahidi tu ndo unaotafutwa au ni intelijensia yetu kuwa dhaifu katika masuala mazima ya kimahakama?? Tafadhali kwa mwenye uelewa na hili naomba majibu?
kuna vitu vingi vinachangia kesi kuchelewa kumizika na kutolewa hukumu.kama kukosekana ushahidi,mashahidi kutotokea mahakamani hivo kesi kuhairishwakutokamilika kwa upelelezi..kukosekana uahahidi,mlundikano wa kesi nyingi mhakamani hivo utaskia kesi inapigwa kalenda hadi miezi miwili ijayo au mitatu ndo itasikilizwa tena nk.

ila keai ya huyu dada kuna mambo mengi yalijitokeza..ni haya
-alidanganya umri..akikuwa jila ataopoulizwa anasema ana miaka 18..tangu akiwa na miaka 15.anaingia club na kulewa huko..amaenda uhamiaji anapewaje sihui passport eti ana miaka 18,visa anapewa,gari anaendesha.na mengineyo
so siku alivopatwa na huu msala na kukamatwa akiandikiahwa polis akasema ana miaka 18.
akapelekwa mahakama.ghafla babake akaibuka akasema mwanangu ni mtoto..ashtakiwe kama mtoto hajafika 18..nimemzaa1995..2012 hiyo ana miaka 16 na ndo anakaribia kufikisha 17.
so ukaibuka mvutano..ashtakiwe wapi..mahakama ya watoto au watu wazima!?
mahakama na polis wanasema tunamtambua kama mtu mzima wa miaka 18..baba mtu na wakili kibatala wanamtambua kama mtoto na kuweka pingamizi...so badala ya kusikiliza kes ya mauaji wakaanza kwanza kesi ya wapi akaahtakiwe..kama mtoto au mtu mzima..hii ilipelwkea hata yeye lulu kukaa segerea kama mahabusu kwa miezi tiaa hadi alipoombeqa dhamana akapata kwa million 20 ndo akarudi uraiani kwa masharti...uongo qake ulimcost mwnyewe.
-pili akiwa uraiani alikuwa anapewa tarehe anahudhuria.tukashangaa ghafla kimyaa..inaaemekana alipata tajiri wa madini aliwnda kuhonga pesa za kutosha kesi ipotezewe..na ikawa hivo lakini faili bado lilikuwepo.

hivi majuzi magufuli aliteua jaji mkuu mpya..huyu jaji alivoingia kazini akakuta mlundikano wa kesi nyingi.haikufurahisha.halafu mahakimu,mawakili na wafanyakazi wengineo ndo walikua wanatarajia kuingia likizo.huku kuna kesi si chini ya mia nne..na kuna mahabusu wana hata miaja mitano wako jela wanasubiri keai ziishe ..akawapiga atop hakuna cha likizo wala mjomba ake likizo..mpaka mmalize hivo viporo vya kesi.
wakapewa na budget..kazi ikaanza..
so kwa sasa ni bampa to bampa hadi kesi zote ziishe..hakuna kiporo.
kila siku zinasomwa kesi nyingi tu sema hazina umaarufu..
hii ndo imefika..na ukiangalia ilianza alhamis..ikaaikilizwa tena ijumaa..inatarajiwa tena jtatu..hii inamaanisha keai itaisha ndani ya mwez huu huu na hukumu itatolewa.

kama aio amri ya huyu jaji kesi ingeskilizwa miaka kumi ijayo.
 
[emoji122] [emoji122] [emoji122] [emoji122] [emoji122] [emoji122] [emoji122] kwa hizo sababu umenifungua pakubwa mdau. Asante sana kamanda, Kweli hii ndo Tanzania bhana. Ngoja tusubiri tutasikia mengi.
 
Back
Top Bottom